Netanyahu: Sikumvuta Trump vitani na Iran

Netanyahu: Sikumvuta Trump vitani na Iran

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amekanusha kwamba alimburuza Rais wa Marekani Donald Trump katika vita dhidi ya Iran, akidai kuwa yeye ndiye mshirika mdogo katika uvamizi huo wa pamoja wa Israel na Marekani nchini Iran.

Netanyahu vile vile amesema anaona kuwa vita hivyo na Iran vitafikia mwisho haraka kuliko inavyofikiriwahuku akidai kuwa wameusambaratisha uongozi wa jamhuri hiyo ya Kiislamu.

1773990299532.png
Hata hivyo Netanyahu, ametangaza kuwa jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhoofisha uwezo wa kijeshi wa Iran katika kipindi cha siku 20 tangu kuanza kwa vita hivyo.

Akizungumza na wanahabari, Netanyahu amepuuza ripoti za upotoshaji na kusisitiza kuwa Israel inashinda vita hivyo kwa kuifuta misingi ya uzalishaji wa silaha nchini Iran.

Netanyahu amebainisha kuwa tofauti na operesheni zilizopita, mashambulizi ya sasa yamelenga "moyo" wa viwanda vya Iran ili kuhakikisha hawawezi kuunda tena makombora au silaha za nyuklia.

Amedai kuwa mamia ya vifyatulia makombora yameharibiwa, na akiba ya makombora pamoja na droni imepunguzwa kwa kiasi kikubwa.

Netanyahu says Israel did not 'drag' the US into the Iran war and says Israel 'acted alone' on Iranian gas fields

Israeli Prime Minister, Benjamin Netanyahu, said nobody can tell Trump 'what to do' and added that the US president asked him to hold off on any future gas field attacks.
 
Kobaz haziamini macho yao kwamba jamaa yupo hai 😂

Jamaa alitoa video za Ai ili kuwapa imani kobaz 😂
 
Hii kauli inakinzana na ile aliyoitoa Marco Rubio... Netanyahu ni kiongozi mmoja mjanja Sana, mafunzo Yake ya kimedani anayatumia vizuri.
 
Back
Top Bottom