Netanyahu: Iran sasa ni dhaifu

Netanyahu: Iran sasa ni dhaifu

Kuna watu wa propaganda kama nyie?

Mkaleta had 10points eti Marekani kazikubali

Mkaja na propaganda et NETANYAHU amekufa

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣


Kuna watu wanapenda kudanganywa na wajanja wameshajua namna ya kuwadanganya ili wapate followers.

Haya walidai kwamba Marekani imepiga magoti mbele ya Iran. Huko Islamabad hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa, wametoka kapa. Muda wowote wanaweza kurudi kwenye uwanja wa vita.

Kachanganyikiwa kama wewe



View: https://www.youtube.com/watch?v=s0KDOjsIHJg&t=16s
 
Kumbe upo mbali sana uelewa. Nikupe shule ndogo:
Kwenye vita, mwenye nguvu anakupiga ili baadaye mkae mezani ukubali matakwa yake ukiwa kwenye hali dhaifu, ukijua kuwa ukikataa unarudia kwenye hali ya hatari.

Hata mataifa yaliyokuwa makoloni, yalipambana kwa vita, lakini mwishoni walikaa na nchi watawala mezani ili kufikia maafikiano ya mwisho. Hata Putin anaipiga Ukraine, huku akiwa ameweka mapendekezo yake kama Ukraine inataka vita iishe. Hata Tanzania ilipoizidi uwezo Uganda, kilichofuatia ilikuwa ni kuwataka waganda waweke utawala mpya ambao si adui kwetu. Israel inaipiga Lebanon, lakini baada ya kuona imekwishaidhoofisha, imeitaka Lebanon waende kwenye mazungumzo, huku Lebanon ikiwa dhaifa, na hivyo Israel italazimisha matakwa yake ya kutaka Hezbollah wanyang'anywe silaha. Hata ukiwa na nguvu, hakuna vita ambayo utapigana na Taifa jingine, ukalishinda, halafu baada ya hapo mkawa katika utulivu bila ya mazungumzo ya mezani yatakayoondoa uhadama. Marekani inaipiga Iran ili idhoofike, halafu ilazimishe matakwa yake. Lakini kama Iran inaona bado ina uwezo wa kupigana, itaendelea, ili wakienda kwenye mazungumzo, isiende ikiwa dhaifu. Kitu ambacho Marekani na Israel hawatataka, hivyo kuna uwezekano wataendelea kuipiga mpaka ifike Iran ione kuendelea na vita ni kuangamia, na hivyo aheri kuridhia matakwa ya Marekani ili kujiokoa.

Kwenye haya mazungumzo ya sasa, Marekani iliamini kuwa tayari Iran ipo dhaifu kiasi cha kukubali chochote ili nchi iwe salama. Lakini Iran inaona bado inaweza kuendelra kupigana.
Baada ya kuangamiza viongozi wakuu wa Iran wa kidini na kijeshi na kuchakaza miundombinu mikuu ya kijeshi ya Iran, Trump aliwapa amri moja tu: anataka unconditional surrender! Kama aliyopata Venezuela. Hakukuwa na mazungumzo. Huyo ndio Trump.

Bahati mbaya Iran sio Venezuela. Alishangaa kuona drones na makombora ya bei rahisi yakishambulia bases na properties za maana za US huko nchi za Ghuba na kupenya iron dome ya Israel. Kisha wakadhibiti pito la Hormuz na kuweka “kibanda cha tozo” (toll booth) na kuanza kukusanya US2m kwa kila meli wanayoiruhusu kupita. Meli zlizolazimisha kupita zilipigwa makombora. Bei za oil zikapanda. Hofu ya kiuchumi ikatanda US na duniani. Hilo ndilo jibu alilopata toka Iran. Akashtuka sana. Hakutegemea.

Nani anaongoza mashambulizi huko Iran? Hamjui. Waongee na nani? Hajui. Wote waliokuwa wanaongea nao wamewaua! Walioonekana kuwa na hekima na simile wamewapuuza na kuwaua sasa wanahangaika na vichaa wasiojulikana.

Trump sio mtu wa kuongea na watu wanyonge na masikini. Hata ndani ya nchi yake na ndani ya serikali yake. Anaabudiwa. Viongozi wa Ulaya/NATO anawasemea mbovu kila wakati. Alimdhalilidha Zelenskyy vilivyo WH. Anaowaheshimu hapa duniani ni Putin, Xi, na Kim.

Pakistani wamejitolea kuleta muafaka. Iran walidai timu ya US iongozwe na VP JD Vance ndio watashiriki. Trump akakubali. Haijawahi tokea US kupangiwa mjumbe wake kwenye mazungumzo.

Anyway, yameshindikana. Hakuna haja ya maneno mengi. Sasa tunasubiri kuona jinsi US na Israel watakavyoichakaza Iran hadi kurejea zama za mawe (Stone Age) kama wengi mnavyotarajia.
 
Kuna watu wa propaganda kama nyie?

Mkaleta had 10points eti Marekani kazikubali

Mkaja na propaganda et NETANYAHU amekufa

🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣


Kuna watu wanapenda kudanganywa na wajanja wameshajua namna ya kuwadanganya ili wapate followers.

Haya walidai kwamba Marekani imepiga magoti mbele ya Iran. Huko Islamabad hakuna makubaliano yoyote yaliyofikiwa, wametoka kapa. Muda wowote wanaweza kurudi kwenye uwanja wa vita.

Sisi Makobaz uongo ni suna Muddy pia alikuwa muongo na tapeli ndo tunapita humo humo. Kwa mjomba wetu
 
Benjamin Netanyahu:

“Iran inaingia kwenye mazungumzo ikiwa ni dhaifu kuliko wakati wowote katika historia ya utawala wa Kiislamu. Walitaka kutunyonga, lakini sasa sisi ndio tunawanyonga wao.”

11, April 2026

Akiwa katika vyombo vya habari aliwaambia watazamaji wake kuwa usitishaji wa mapigano wa wiki mbili ni "hatua njiani" tu kuelekea malengo ya Israeli.

Islamabad

Wakati wajumbe wa Iran wakijaribu kuonyesha msimamo mkali kwenye meza ya mazungumzo kule Pakistan, Netanyahu alitaka dunia (na soko la mafuta) ijue kuwa Iran inapigana kutokea kwenye kona, siyo kutokea kwenye nguvu.

Kujibu Hatua ya Trump: Hotuba yake ilikuja muda mfupi baada ya Donald Trump kutangaza kupitia Truth Social kuwa jeshi la Marekani limeanza kusafisha Mlango-bahari wa Hormuz na kuzamisha mashua 28 za Iran.

Alichokimaanisha kwa "Dhaifu"

Netanyahu alifafanua udhaifu huo kwa kusema:

1. Iran imepoteza miundombinu muhimu ya nyuklia katika mashambulizi ya Aprili 8 na 9.

2. Makamanda wake wakuu wa IRGC wameuawa (ikiwemo vifo vya hivi karibuni vya marubani na makamanda wa intelijensia).

3. Uchumi wa nchi hiyo unategemea kuachiwa kwa zile Tsh trilioni 15.5 zilizoko Qatar ili kuepuka machafuko ya ndani ya nchi.

Onyo la "Kidole Kwenye Kitufe"

Licha ya kusema Iran ni dhaifu, alisisitiza kuwa Israeli haijaweka silaha chini. Alisema: "Hata kama wanazungumza Islamabad, kidole chetu kiko kwenye kitufe cha shambulio. Hatutakubali makubaliano yoyote yanayoiacha Iran na uwezo wa kutengeneza bomu la nyuklia."

Leo Islamabad imeamka nje ya makubaliano ya pande mbili kufikiwa. Hivyo kauli ya Netanyahu ya kurudi vitani imehakikishwa.
Kama iran dhaifu anaogopa nn kwenda ardhini,,, na yy ndio dhaifu zaid maana sio kipondo kile
 
Nani anaongoza mashambulizi huko Iran? Hamjui. Waongee na nani? Hajui. Wote waliokuwa wanaongea nao wamewaua! Walioonekana kuwa na hekima na simile wamewapuuza na kuwaua sasa wanahangaika na vichaa wasiojulikana.
😁😁😋😋Labda Ni majini ndiyo yanayopigana.
 
😁😁😋😋Labda Ni majini ndiyo yanayopigana.
Inawezekana kwa wanaoamini katika hayo madude.

Kazi ngumu sana kupigana na watu wasioogopa kifo wala wasio na tamaa ya Maisha ya dunia hii. Ni kama kupigana na "majini"😁

Kule Afghanistan Soviet Union walikimbia baada ya miaka tisa ya kuangamiza maelfu ya wapiganaji wa Mujahideen. US walikimbia baada ya miaka ishirini ya kupambana na Taliban pamoja na kuua maefu yao.

2003 US waliingia Iraqi kwa mbwembwe wakaichakaza kwa makombora (desert storm/shock and awe). Wakasambaratisha utawala wa Saddam Hussein. Wakampitisha kwenye Kangaroo court akanyongwa. Wakatangaza ushindi mwaka huohuo (Mission Accomplished). Kabla hawajakaa sawa wakajikuta wakikabiliana na kundi la ISIS lililowapeleka puta hadi 2011 walipoamua kubwaga manyanga na kuondoka Iraq haraka sana wakiacha civil war. Hata Wakristo wachache waliokuwa huru kuabudu wakati wa Saddam Hussein ndio ikawa mwisho wa jamiii hiyo.

Tuone Trump atafika wapi na hayo majitu. Wao wanasema: you have the watches, we have the time (wewe unamiliki saa, sisi tuna muda).

Kajiletea tabu ya bure kwa kumuendekeza Netanyahu. Hakujiuliza kwa nini Netanyahu na ubabe wake wote amehangaika kutafuta support ya US miaka 40 ili kuipiga Iran na kukakataliwa na maRais wote wa US kabla ya Trump.
 
Back
Top Bottom