Net budget TSH 10 Million. Je, naweza agiza na kumiliki IST kutoka nje?

kayanda01

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
1,086
913
Hello wanaJF wote.

Title inajieleza. Nimedunduliza ili kununua kausafiri. Nina TSH 10 Million net. Je, naweza imiliki Toyota IST kwa kuagiza kutoka nje? Kujumuisha gharama zote na ushuru wa TRA.

Kama inawezekana, nitumie kampuni gani ya kuagiza magari?

Nataka IST yenye specs zifuatazo:

✓ Production year 2005 (minimum);
✓ Km 90,000 (maximum);
✓ White or Pearl (rangi);
✓ 4WD (CBA ncp65);
✓ Fog lights;
× Isiwe na Rear Spoiler ×(no rear spoiler).
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Ni hivyo wakuu. Sijawahi kumiliki gari, na pia ni layman kwenye uelewa wa ubora wa magari. Hivyo, napokea ushauri wowote wenye tija kuhusiana na mada hii.

Naombeni mawazo yenu na ushauri. Ahsanteni.
 

Shukrani mkuu
 
Weeeee unataka kumdanganya mwenzio afunge ndoa na jini.
Inaonekana hujui magari.
Au hujamuelewa alivyotaka ist?
Hiyo progress inafaa kama una sheli home.
Ndio maana bei yake ni cheap.
 
Weeeee unataka kumdanganya mwenzio afunge ndoa na jini.
Inaonekana hujui magari.
Au hujamuelewa alivyotaka ist?
Hiyo progress inafaa kama una sheli home.
Ndio maana bei yake ni cheap.

Upo sahihi Mkuu. Nimechagua IST sababu ya fuel efficiency. Ila ninahitaji IST yenye'4WD'.... sijuwi kama una utofauti wa ulaji wa mafuta kwa gari yenye '4WD'. Ahsante
 
Bos IST kuagiza mpk ufike kuanzia 11 kwendelea
Me nikushauri agiza then hela inayobaki weka bank uendelew kuichanga taratibu mpk gar ifike hautakosa 1m ya kuongezea itoke bandari bos

Haya mkuu. Itabidi nitafute tena hiyo M 1 ya kuongeza.
 
I

Inatosha sana kuna kuna siku nimeona jamaa wanauza mpaka 9m na laki kadhaa na hiyo ni bei pamoja na usajili lakini bila bima
Hiyo unazungumzia muuzaji yuko bongo. Mwenzio anataka kutoka Japan straight. Na iwe ma sifa alizoomba kama 4wd. Binafsi naona 10M haitoshi. 12M sawa. Ila 4wd napo atahenya sana
 
Hiyo unazungumzia muuzaji yuko bongo. Mwenzio anataka kutoka Japan straight. Na iwe ma sifa alizoomba kama 4wd. Binafsi naona 10M haitoshi. 12M sawa. Ila 4wd napo atahenya sana

Mkuu, 4WD nitahenya sana kivipi, upatikanaji wake? Ama ulaji wa mafuta?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…