Net budget TSH 10 Million. Je, naweza agiza na kumiliki IST kutoka nje?

kayanda01

JF-Expert Member
Feb 14, 2014
1,081
907
Hello wanaJF wote.

Title inajieleza. Nimedunduliza ili kununua kausafiri. Nina TSH 10 Million net. Je, naweza imiliki Toyota IST kwa kuagiza kutoka nje? Kujumuisha gharama zote na ushuru wa TRA.

Kama inawezekana, nitumie kampuni gani ya kuagiza magari?

Nataka IST yenye specs zifuatazo:

✓ Production year 2005 (minimum);
✓ Km 90,000 (maximum);
✓ White or Pearl (rangi);
✓ 4WD (CBA ncp65);
✓ Fog lights;
× Isiwe na Rear Spoiler ×(no rear spoiler).
Xxxxxxxxxxxxxxxxxxx

Ni hivyo wakuu. Sijawahi kumiliki gari, na pia ni layman kwenye uelewa wa ubora wa magari. Hivyo, napokea ushauri wowote wenye tija kuhusiana na mada hii.

Naombeni mawazo yenu na ushauri. Ahsanteni.
 
Mkuu, ingia kwenye website za kuuza magari, https://www.japanesevehicles.com/?gclid=EAIaIQobChMI457I_9ze4gIV1JTVCh02hQr_EAAYAiAAEgJ_2PD_BwE, angalia price ya ist uitakayo huko, kisha uingie kwenye website ya tra, https://gateway.tra.go.tz/umvvs/ uingize hizo details za gari, kisha utapata majibu ya kodi zote unazopaswa kulipa, mpaka gari iwe barabarani..

Nimekuwekea website moja hapo ya magari.. ila zipo nyingi tuu.. Huko utapata majibu mazuri..

Shukrani mkuu
 
Nimetoka kuangalia sasa hivi kuna Toyota Progres ya mwaka 2000, ambayo imetembea only 45000km tuu.. Price ya kununulia na kulipa ushuru hapa bongo mpaka itoke ni chini ya 10M.. Unaweza kuingia na kuiangalia https://www.japanesevehicles.com/vehicle_details.php?vid=200039&lang=en
Weeeee unataka kumdanganya mwenzio afunge ndoa na jini.
Inaonekana hujui magari.
Au hujamuelewa alivyotaka ist?
Hiyo progress inafaa kama una sheli home.
Ndio maana bei yake ni cheap.
 
Weeeee unataka kumdanganya mwenzio afunge ndoa na jini.
Inaonekana hujui magari.
Au hujamuelewa alivyotaka ist?
Hiyo progress inafaa kama una sheli home.
Ndio maana bei yake ni cheap.

Upo sahihi Mkuu. Nimechagua IST sababu ya fuel efficiency. Ila ninahitaji IST yenye'4WD'.... sijuwi kama una utofauti wa ulaji wa mafuta kwa gari yenye '4WD'. Ahsante
 
Bos IST kuagiza mpk ufike kuanzia 11 kwendelea
Me nikushauri agiza then hela inayobaki weka bank uendelew kuichanga taratibu mpk gar ifike hautakosa 1m ya kuongezea itoke bandari bos

Haya mkuu. Itabidi nitafute tena hiyo M 1 ya kuongeza.
 
Hiyo unazungumzia muuzaji yuko bongo. Mwenzio anataka kutoka Japan straight. Na iwe ma sifa alizoomba kama 4wd. Binafsi naona 10M haitoshi. 12M sawa. Ila 4wd napo atahenya sana

Mkuu, 4WD nitahenya sana kivipi, upatikanaji wake? Ama ulaji wa mafuta?
 

Similar Discussions

9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom