mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 343
- 359
KATMANDU NEPAL
Kikundi hasimu cha chama tawala cha Kikomunisti cha Nepal (NCP), kinachoongozwa na Pushpa Kamal Dahal na Madhav Kumar kimefanya maandamano kwa kuwasha mwenge huko Kathmandu dhidi ya uamuzi wa Waziri Mkuu, KP Sharma Oli wa kuvunja Bunge.
Jumuiya ya wanafunzi ya NCP, Umoja wa Kitaifa wa Wanafunzi wa Nepal (ANNFSU) ulifanya maandamano ya mwenge katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu ambapo makada waliimba kaulimbiu yao dhidi ya Waziri Mkuu Sharma Oli na uamuzi wake ulio kinyume na Katiba.
Waliomba pia kufanikisha mgomo wa kitaifa.
Kikundi cha Splinter kinachoongozwa na Dahal na Nepal, Jumatano iliyopita kilifichua mipango yao mipya ya maandamano ambayo waliyaitisha kuanzia Alhamisi.
Kikundi hasimu cha NCP pia kimepinga hatua ya serikali ya kuwaapisha kwa siri wajumbe wapya walioteuliwa katika vyombo mbalimbali vya kikatiba.
Jumatano iliyopita, Jaji Mkuu Cholendra Shamsher Rana aliwaapisha watu zaidi ya 40 katika vyombo mbalimbali vya kikatiba mbele ya Rais wa nchi hiyo, Bidya Devi Bhandari.
Kufuatia kuvunjwa kwa Bunge, wajumbe wapya walioteuliwa katika Taasisi za umma za kikatiba, walikula kiapo cha kazi na usiri bila kusikilizwa kwa Bunge.
Hatua hiyo imekuja baada ya kundi pinzani la chama tawala cha NCP kumuondoa Oli kutoka kwenye chama hicho wakati wa machafuko ya kisiasa yanayozidi kuongezeka kufuatia uamuzi wake wa kuvunja Bunge.
Wakati huohuo, baada ya kuvinja Bunge, Waziri Mkuu pia alipendekeza uchaguzi mkuu kufanyika Aprili 30 na Mei 10, mwaka huu.