Neno X-mass limenichanganya

jerry jofrey

New Member
Dec 26, 2015
3
0
CHRISTMAS ni MUUNGANO wa maneno mawili yaani CHRIST & MAS.

Hapo zamani, siku ya Tarehe 25 December, ilikua siku ya Kusherehekea MITAMBIKO YA KIPAGANI kabla MWANA WA MUNGU, YESU KRISTO hajazaliwa.

Baadae mwaka 533 AD, Mtakatifu Constantine, aliyekua Mkuu wa Kanisa la WARUMI, ambalo siku hizi linajulokana kama Kanisa la Katoliki (Kanisa la kwanza), aliibadili siku hiyo isiwe tena ya MITAMBIKO YA KIPAGANI badala yake siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa MKOMBOZI MWANA WA MUNGU YESU KRISTO na kuiita siku ya kusanyiko la KRISTO yaani CHRISTMAS.

1. CHRIST ni neno la kiingereza ambalo tafsiri yake ni KRISTO yaani MASIA au MPAKWA MAFUTA au ALIYETENGWA KWA KAZI MAALUMU.

2. MAS ni neno la KIYUNANI ambalo maana yake ni KUSANYIKO.

Kwa hiyo maana ya neno CHRISTMAS ni KUSANYIKO la KRISTO. Kwa WAKRISTO wanaoamini siku hiyo, wawe makini sana na neno X-MASS!

Inaaminika kuwa, baada ya siku hiyo ya kukumbuka kuzaliwa kwa YESU KRISTO, kupata umaarufu, neno X-MASS, lilikuja baadae sana na lililetwa na wapinga KRISTO ambao waliamua kufuta neno CHRIST kwa kuweka alama ya "X" yaani hakuna KRISTO. Hiyo ilibadili maana kwa kusomeka X-MASS.

X-HAKUNA na MASS-KUSANYIKO, hivyo X-MASS, maana yake ni HAKUNA KUSANYIKO LA KRISTO! Yaani HAKUNA CHRISTMAS!

Sasa, Kama wewe ni Mkristo hutakiwi kutumia neno X-MAS, badala yake tumia neno CHRISTMAS. MUNGU awabariki muwe na CHRISTMAS Njema sio "X-MASS"..
 
Siyo kweli. X-Mass ni mkusanyiko wa viongozi kumi wa juu wa kanisa waliokaa kubadili vitabu vilivyokuwapo. Baada ya majadiliano marefu ni vitabu gani vitumike vya injili na gano jioya ndipo ikafikiwa kwamba waviweke mezani kisha waombe na vitabu vitakavyokutwa viko chini ya meza vitafutwa. Ndipo asubuhi walipoamka na kuingia kanisani kweli walivikuta vitabu kadhaa viko chini. Kuanzia siku hiyo vitabu vilivyokutwa chini havitumiki hadi leo........mojawapo ni injili ya Barnaba. Lakini wakati wanaingia kanisani kuangali vitabu alivyovishusha Mungu chini ya meza walikuta nyayo za binadamu ameingia na kutoka......hiyo ndio kumbukumbu mnayotakiwa kuizingatia...
 
Tetete hapa ndipo wanaponipa raha wakatoliki na wakatorika.wakristo sana wasiotaka kuhoji na kupata mantiki ya imani yao na wakristo wampendao mungu wao lakini wapo tayari kudadavua na kutaka kuyaelewa vyema maandiko na taratibu za kumjua kumwamini na kumfwata vilivyo muumba wao
 
Ukimchunguza sana bata waweza shindwa mla! Ila mfugaji mzuri huandaa mazingira mazur ya bata wake ili akimla asikie raha ya ukweli ya bata! Ngoja tuone mazingira sahihi ya ufugaji bata huyu, je anafaa kuliwa?
 
Imani ni zaidi ya maandishi na matamko, cha mhimu kwako ni je sukukuu ya noel Ina maana ktk maisha yako ya kiroho?
 
Mazingira yanapo kuwa bora. Ya ufugaji kamwe huwezi shindwa kumla bata ambae ulimfuga kwa maandalizi bora kwakujua yakwamba nitegemeo lako kumla baadae
 
Back
Top Bottom