Asimilia 82 ya Wanafunzi Wakosa Mikopo 2015/16
Zaidi-ya wanafundi 50,000 watashindwa kuendelea na masomo ya elimu ya juu kutokana na kushindwa kupata mikopo kutoka katika Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB).
Hayo yamebainika ikiwa ni siku tatu tangu HESLB kutoa majina ya wanafunzi waliofanikiwa kupata mikopo kwa mwaka wa masomo 2015/2016, huku idadi kubwa ikiwa haimo katika majina hayo.Katika mwaka huu wa masomo bodi ya mikopo imeweza kuwapatia mikopo wanafunzi 12,000 pekee sawa na 17.1% ya waombaji zaidi ya 70,000, hivyo kufanya idadi ya wanafunzi waliokosa mikopo kufikia asilimia 82.9 ya waombaji wote.