Neno La Leo: Ulaya Mgeni Jembe Siku Ya Kwanza! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Ulaya Mgeni Jembe Siku Ya Kwanza!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jul 28, 2010.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jul 28, 2010
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Na Maggid Mjengwa,

  Jana nilifika Sweden saa tano na nusu asubuhi nikitokea Dar. Mwenyeji wangu alinipokea Uwanja wa ndege. Alikuja na gari yake inayotumia gesi inayotokana na mabaki ya mazao. Gharama ya gesi hiyo ni nusu ya gharama ya diseli. Sweden kuna vituo vya kujazia gesi ya magari.

  Gari lake lina nafasi kubwa nyuma. Ni gari analotumia zaidi kubebea mazao yake kupeleka kwa wateja wake. Analitumia pia kwa matumizi ya nyumbani.Nilipofika nyumbani kwake tukaandaa chakula cha mchana pamoja kisha tukaanza safari ya kwenda shambani kwake. Afrika tunaimba ” Mgeni siku ya kwanza mpe pilau na kachumbari, siku ya pili mpe… siku ya tatu… mpaka siku ya ngapi sijui ndio umpe jembe akalime! Kwa mkulima wa Ulaya, mgeni jembe unapewa siku ya kwanza! Rafiki yangu Par ana shamba la eka moja na nusu la kilimo cha mboga bila kutumia madawa ( Organic farming).

  Nitakaa nyumbani kwake kwa siku mbili, jana na leo. Nitamsaidia katika kazi za shambani kwake lakini pia nina mengi nitakayojifunza. Miaka miwili iliyopita alianza ‘kama mchezo vile’. Alikuwa na kabustani kadogo nje ya nyumba yake. Nakumbuka kumwona akivuna kidebe cha lita nne za mboga kila siku. Alianza kwa matumizi ya nyumbani. Jirani wakapenda pia awauzie. Per aliona haraka soko la kilimo hicho. Bidhaa zinazotokana na kilimo cha organic zina bei nzuri sana Ulaya na Marekani.

  Per Akafanya bidii ya kazi. Akaongeza mavuno. Hatimaye akaamua kuacha kazi yake ya kuajiriwa. Akafungua kampuni yake ya kilimo. Leo ana wateja 60 wanaoagiza bidhaa zake kwa kupitia intaneti. Ndio, amefungua soko lake la kwenye mtandao. Mteja anaingia, anaagiza mboga anazotaka, kisha analipa kwa njia hiyo pia. Anachofanya Per ni kutumia gari lake, kila baada ya majuma mawili, kusambaza mboga hizo kwa wateja wake mpaka milangoni. Na mara moja kwa mwezi, Per anasimama sokoni na gari lake akiuza mboga hizo. Anafanya hivyo ili kutangaza biashara yake kwa wengine. Idadi ya wateja wake inaongezeka. Mapato yake kwa mwaka ni shilingi za Kitanzania milioni mia tano na zaidi. Anafikiria kuajiri watu wa kumsaidia huko anakokwenda.

  Mkulima Per anatukumbusha simba yule anayehangaika kutwa nzima mbugani kuwinda panya pori wakati simba ana uwezo, kasi na sababu za kumwinda mnyama swala. Mnyama ambaye si tu ni mlo mtamu kwa simba, bali ni mlo wenye kumpa heshima simba mwenyewe. Kwamba mara nyingi tumekuwa ni watu wa kuridhika na vidogo sana wakati tuna uwezo wa kufanya makubwa. Mkulima Per Eklund ni mfano wa kuigwa.

  Na hilo ni Neno La Leo.
   
 2. Rose1980

  Rose1980 JF-Expert Member

  #2
  Jul 28, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 5,701
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 0
  dah kweli
  usisahau kunibebea matembele,mchunga,mnamvu na fiwi uko asi zinapatikana eehh?
  ntakusubir airport kuchukua mzgo wangu manake usje enda kariakoo kuvinunua....nataka vay ulaya ulaya!!!!!!
   
Loading...