Neno la leo: Ukiona unaogopwa jua kuwa huna haki ndani yako

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,702
36,124
Habari!

Mara nyingi utasikia watu au mtu akijitapa kuwa anaogopeka aidha kazini au mtaani kwake.

Iko hivi, kama unaogopeka na mtu yeyote jua kuwa haki haimo ndani yako. Ukiona nchi ina wananchi wanaowaogopa Askari basi jua kuwa hiyo nchi haina haki. Mume akiishi kwa kumwogopa mke wake basi jua kuwa hiyo nyumba haki imetoweka. Ukiogopwa na mke wako au watoto wako basi jua kuwa nyumba yako haina haki. Haki imetoweka.

Watumishi wakimwogopa boss wao jua kuwa hiyo ofisi haki imetoweka.

Note: Si jambo jema kuogopwa na mtu yeyote yule hapa duniani, awe fukara au tajiri, mtoto au mkubwa.
 
2057375_IMG_20190511_212352.jpg
IMG_20210211_163750.jpg

IMG_20210211_163809.jpg
 
Ni kweli mkuu, kuogopwa siyo sifa ni tatizo kama vile kuwa na kitambi (obesity)
Mkuu kwani kitambi ni tatizo,mi nafurahi kuwa nacho kwanza kinanisaidia kufuta kioo cha hii smart phone,pili ukivaa tai inaonekana,tatu sisi wakiristu kuwa na kitambi sio shida kwani Siku tukifa hatukamuliwi.

Sijawahi kujuta kuwa na kitambi aka public opinion.
 
Back
Top Bottom