Neno La Leo: Tunaangamia Kwa Kukosa Hekima! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Tunaangamia Kwa Kukosa Hekima!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by maggid, Mar 13, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,

  MFALME Suleiman aliambiwa ndotoni aombe kitu chochote kwa Mola wake, naye akajibu; " Ewe Mola wangu, nipe mimi mtumwa wako moyo wa adili ili niwahukumu watu wako, na kupambanua mema na mabaya, maana ni nani awezaye kuwahukumu hawa watu wako walio wengi?"

  Hivyo basi, Mfalme Suleiman alichagua hekima. Maana, ni Mfalme Suleiman huyo anayekaririwa na vitabu vya dini akitamka, kuwa; " Watu wangu wanaangamia kwa kukosa hekima".

  Naam, hekima ndilo jambo lililo bora kabisa kwa mwanadamu kuwa nalo. Mwanadamu aliyepungukiwa hekima ana hasara kubwa maishani. Hekima ni tunu na kipaji ambacho Mwenyezi Mungu amewajalia waja wake, ili nao waweze kupambanua na kuamua kati ya yaliyo mema na maovu. Duniani hakuna shule ya hekima.

  Nakumbuka nilipokuwa kijana mdogo nilitamani sana kilimo. Marehemu babu yangu alimiliki ardhi kubwa kijijini kwetu Nyeregete, Mbarali. Nilimwomba anipe ardhi ya kulima, naye alinipa kipande kidogo cha ardhi, chapata robo eka.

  Akaniambia huku akinionyesha kwa mikono; " Hapa utachagua mwenyewe, ama ulime mpunga au mahindi". Kisha akanikabidhi jembe kubwa jipya mfano wa kopa. Hakunipa mpini, na jembe halikunolewa. Nikamwomba anisaidie na vyote viwili, mpini na kunolewa jembe. Naye akanijibu; " Mpini utautafuta mwenyewe, na jembe hunolewa ardhini". Kwangu mimi, ile inabaki kuwa shule kubwa ya juu ya nini maana ya maisha na namna ya kupambana ili kuishi.

  Naam. Duniani hakuna shule ya hekima. Kuwa na hekima ni kuwa na tunu, kuwa na kipaji ambacho binadamu hujaliwa nacho. Na mwingine atajiuliza; hekima ni nini? Ni ule uwezo wa mwanadamu kuwa na maarifa ya kufahamu kipi cha kufanya, kwanini afanye, wapi na kwa wakati gani. Hivyo basi, hekima ni maarifa, tunaangamia kwa kukosa maarifa, kukosa hekima. Na tuitafute hekima. Na hilo ni Neno La Leo.

  Maggid,

  Dar es Salaam
  Machi 13, 2011
  mjengwa
   
 2. Magogwajr

  Magogwajr JF-Expert Member

  #2
  Mar 13, 2011
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Usichakachue bible na kuweka hekima japo umeionyesha kuwa na same meaning bt ni maarifa nt hekima
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Mar 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  ni kweli hata ufisadi umeongezeka sana kwa kua kila mtu amekosa hekima!si mwananchi wala si kiongozi cha muhimu kila mmoja ashike hatam kwa nafasi yake kutokomeza hali hii
   
 4. Jilanga

  Jilanga JF-Expert Member

  #4
  Mar 13, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mtumishi yuko nyote mpo sawa ilg tu kina kusumbua wewe yawezekana unatumia version moja tu! Ambayo iliandikwa kwa kiswahili cha kisasa! Yawezekana walichakachua ktk kufasiri! Ukisoma Bible Ya Kingereza hawasemi maarifa bali wameandika (wisdom) busara/hekima katika matumizi ya jina na kitenzi!
  Yote ktk yote kinachomata hakuna aliyepotoza kati yenu ila tu ni umaskini wa maneno/misamiati ktk lugha ya Kiswahili na tofauti ktk fasiri/tafsiri!

  MUNGU AWABARIKI NYOTE, AWAINUE KTK MAPITO YENU! AWAONGEZEE HEKIMA ILI MWENENDE SAWA SAWA NA MPENZI YAKE! Amen!
   
 5. Mlachake

  Mlachake JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2011
  Joined: Oct 13, 2009
  Messages: 2,919
  Likes Received: 608
  Trophy Points: 280
  Asante majid, Tatizo umeacha walio na hekima wakuelewe!
  hakuna mpumbavu atakaye elewa hapa.
   
Loading...