Neno La Leo: Ni Heri Sumu Ya Nyoka! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Ni Heri Sumu Ya Nyoka!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, May 20, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  May 20, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,


  Kusoma ni burudani pia. Wikiendi hii nasoma kitabu hicho pichani, Gamba La Nyoka, mwandishi ni Euphrase Kezilahabi. Kumbe, hata miaka hiyo kuna walioliona na kulijadili ‘ gamba la nyoka!’


  Ni kitabu kinachokurudisha msomaji nyuma kwenye historia. Unakiona kijiji ambamo wanakijiji wake wamekumbwa na mkanganyiko wa njia ipi ya kuifuata.


  Wakiongozwa na mwenyekiti wao wanabaini hila na ghilba za viongozi wa Serikali, na Chama pia. Wanaamua kufanya mkutano wa siri kujadili mustabakali wao. Wamehakikisha, kuwa mkutano utafanyikia katikati ya pori, na kuwa ‘ vijibwa’ vya Serikali wakiwa na maana ya polisi wasijue chochote.


  Swali, ni hili, yawezekana jambo hilo likawa siri hata wakifanyia mkutano porini?
  Na hapa nanukuu maneno yaMwenyekiti wao wa kijiji anayesema haya wakiwa kwenye mkutano wa siri katikati ya pori;


  ” Ndugu zangu Wanakijiji. Kama miti inatoa sauti itingishwapo na upepo, na majani hutoa milio wakati wa upepo mkali, hapana shaka, jambo tutakalolijadili hapa litakuja julikana. (CCJ, Nape, Mwakyembe, Mpendazoe na Sitta?!)


  Mwenyekiti anaendelea kusema; " Ndugu zangu, mwanadamu hana wema. Usimwone kucheka. Akacheka akakusalimu na mdomoni kuitika. Japo kweli maneno yake matamu lakini ndani ni nyoka, ana sumu kali. Na heri sumu ya nyoka maana inaweza kutibiwa. Sumu ya binadamu haitibiki.


  Wengine kati yetu wana tamaa, na tamaa huzaa sumu”. Anasema Mwenyekiti wa Kijiji.


  Ndugu zangu wanakijiji wenzangu wa mjengwablog, ngojeni ’ Mwenyekiti ’ wenu niendelee na uhondo wa kitabuni.


  Wikiendi Njema.


  Maggid
  Iringa,
  Ijumaa, Mei 20, 2011.
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
   
 2. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #2
  May 20, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Mjengwa una chuki na Mwakyembe na Sitta, maana hata walipopewa uwaziri, uliandika makala ya kuwakebehi. Ukweli ni kwamba hao watu wana ushawishi mkubwa wa kisiasa, ndio maana wakapata hata ujasiri (ndiyo, ni ujasiri kwa mwanaCCM anayekula utamu kufikiria kuhama) wa kutaka kuachana na CCM na kuanzisha CCJ. Ktk zama hizi, watu wa kariba hiyo wamebaki wachache sana CCM. Ili kujua kama wao ni nyoka au mjusi, wangeachwa waanzishe CCJ.... mbona ilihujumiwa?
   
Loading...