Neno La Leo: Baba Mobutu; Tikala libela, lokuta monene! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Baba Mobutu; Tikala libela, lokuta monene!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Apr 20, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Apr 20, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu Zangu,


  WAKONGO wa Kinshasa na kwengineko wanaujua wimbo huu; ”Papaa Mobutu ee, lokuta monene, oy'akanisaka, MPR ekokufaha, wayahaa, Tata Marechal, [FONT=&quot]tikala libela[/FONT], tata Mobutuee, [FONT=&quot]tikala libela[/FONT], ...!”


  Makala yangu ya juma lililopita imepekelea baadhi ya wasomaji wangu, na hususan vijana, kutaka kufahamu zaidi habari za Joseph Mobutu. Kuna aliyeniandikia akisema; kwa anavyoiangalia jamii yetu hii, kuna anaoyojifunza kutoka kwa yaliyomkuta Mobutu.

  Mobutu ni kielelezo kizuri cha hulka za watala wengi wa bara letu.
  Na Afrika utazionaje dalili za Chama cha siasa kinachokufa? Jibu; ni pale ’Kiongozi Mkuu’ anapoanza kujitenga na umma, kwa kauli na matendo. Kuna wenzake wachache pia ndani ya Chama watakaokuwa na hulka hiyo. Chama cha siasa huonekana kuwa mbali na watu. Hakikidhi matakwa ,mahitaji na matarajio, si tu ya wanachama wake, bali ya umma. Afrika chama cha siasa hutekwa kirahisi na wachache.


  Je, Mobutu huyu ni nani? Joseph Desire Mobutu. Baadae akaja kujiita, Mobutu Sese Seko Nkuku Ngbendu wa Za Banga. Inasemwa, kuwa Sese Seko ina maana ya milele, na Nkuku Ngbendu wa Za Banga ina maana ya mtu anayepita na kuacha nyuma yake alama za moto . Naam. Ni Mobutu wa milele na anayeacha alama za moto nyuma yake!


  Joseph Mobutu alizaliwa mwaka 1930 na alifia uhamishoni, Rabat, Morocco, mwaka 1997. Kwa matendo yake alipokuwa madarakani, Mobutu aliishia kuzikwa kama njiti ya kibiriti katika makaburi ya ughaibuni. Mazishi yake yaliudhuriwa na watu wachache sana. Hayakufanana na ufahari aliojijengea alipokuwa hai na mwenye madaraka.


  Kule Kongo Mobutu alishasikia kilio cha Wakongo cha kutaka mabadiliko, akapuuzia. Wakongo katika mitaa ya Kinshasa, Lubumbashi, Kisangani na kwingineko walianza kunong’ona, kuwa MPR, inakaribia kufa. MPR- Popular Movement Of The Revolution- kilikuwa ni Chama kilichoanzishwa na Mobutu na wenzake mwaka 1967. Hatimaye Wakongo wakaacha kunong’ona, wakawa wakiongea kwa sauti mitaani, sokoni na kwenye vilabu vya pombe, kuwa, “MPR inakufa!”


  Katika hali ya kujinusuru, Mobutu akawanunua hata wasanii ili wamuimbe yeye na Chama chake. Hiyo hapo juu ni moja ya nyimbo za kumtukuza Mobutu na Chama chake. Tafsiri yake; ” Baba Mobutu, utakaa udumu, wanasema sana , kuwa MPR itakufa, haiwezekani! Naam. Leo tunaona, kuwa Mobutu hakukaa akadumu, MPR imekufa, imewezekana! Na ndivyo wahenga wetu wanavyotwambia; ” Kila lenye mwanzo lina mwisho”. Na hilo ni Neno La Leo.  ( Hii ni sehemu ya makala yangu, Raia Mwema, leo Jumatano)


  Maggid
  Iringa
  Jumatano, Aprili 20, 2011
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
  0788 111 765
   
 2. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #2
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Nimeishia hapa kwa leo:

   
 3. Chuma Chakavu

  Chuma Chakavu JF-Expert Member

  #3
  Apr 20, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 1,524
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  just a spelling skip/mistake supposed to be 'watawala'
   
 4. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #4
  Apr 20, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  What do you mean? - We have skipped so many mistakes thus far - as human beings and as a Country!
   
 5. I

  IPECACUANHA JF-Expert Member

  #5
  Apr 20, 2011
  Joined: Feb 19, 2011
  Messages: 2,127
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Nauona ujumbe huu ni kama 'barua ya Mapenzi' kwa Wanaojivua Magamba kama wanaamini kwamba anayekuambia ukweli na kukuonyesha ulipoanguka/unapokosea anakutakia Mema. Nimeangalia kwenye ITV kilichokua kinaendelea Dodoma wakati NEC ya CCM ilipokua 'inajivua Magamba' waliimba ule wimbo unao hamasisha kujiamini katika mapambano unaosema... " Nani ajuaye....ni Mwenye? Aje Simba mtu..." Ni yale yale ya Mabotu kama asemavyo mtoa 'neno la Leo'.
   
 6. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #6
  Apr 20, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hii imenikumbusha Chama cha Magamba jinsi kinavyokuwa kinapigiwa debe na wanamuziki
   
Loading...