mitale na midimu
JF-Expert Member
- Aug 26, 2015
- 10,419
- 17,759
Kupiga majungu, kumuongea mwenzako pembeni mambo ambayo ulipaswa kumwambia moja kwa moja, Kusingiziana ili mmoja akandamizwe na mwingine atumie hiyo kama ngazi, kusambaza umbea, kuchongeana,Kutokusema ukweli kwa maslahi binafsi ili ukimya huo ukunufaishe kwa njia moja au nyingine, kumbomoa mwenzako kwa hila,etc tabia hizi hufananishwa na kula nyama ya watu (Cannibalism).
Lengo la maneno haya, huwa ni kumjeruhi muhusika kihisia,kisaikolojia na kijamii. Asilimia karibu 90 ya magonjwa tunayopata huanzia akilini. Matokeo yake watu wamekuwa na misongo ya mawazo na wengine hata kufariki. na hii ndiyo sababu vitendo hivi kifananishwa na kula nyama ya mtu hadi kuhakikisha umemmaliza na kumuua kabisa.
NINI UFANYE?
1: Usichangie kwa ushabiki kitu ambacho huna uhakika kama ni kweli kumuhusu mwenzako.
Kama hauna uhakika useme,
2:Watu wengi huwasema vibaya wengine ili wao waonekane au wajisikie vizuri. Ni vizuri kujua nia ya unachoongea, na kama unasukumwa na kisasi,chuki,kukomoa Muombe Mungu akupe nia nzuri.
3:Kuza tabia ya kuwa mzito kuongea na mwepesi kusikiliza.
4:Ikiwezekana kwepa kabisa kukaa meza moja na wala watu.
tabia hii ni maarufu sana makazini, mijumuiko ya kiimani na mijumuiko katika mambo ya kijamii.
:: Ndugu Msisingiziane... (Yakobo 4:11)
:: Speak not evil one of another, Bretheren (James 4:11,KJV)