Nemo kwa wanaume

Nemo kwa wanaume

kidE Meshack

Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
92
Reaction score
7
Kadiri wanawake wanavyopambana kujikwamua kiuchumi ndivyo ndoa nyingi zinazidi kuingia matatizoni.

Tatizo sio wao kupambana bali problem iko hapa:

Wanapambana kwa madhumuni gani? Wanawake wengi hawapambani kwa maana ya kuwasaidia waume zao [kama Mungu anavyotaka] bali kwa maana ya kutoka kivyao; ndio maana utawasikia wanaongea kauli zao za kiuanaharakati, "Usimtegemee mume", "wanaume hawaaminiki", "bora mwanamke niwe na uchumi wangu n.k".

Kama mume ni kichwa maana yake mke ni kiwiliwili; bahati mbaya ni kwamba macho na ubongo viko kwenye kichwa na sio kiwiliwili.

Kiwiliwili kisipokiamini kichwa "automatic" kitaielekeza miguu kokote na kwa kuwa hakuna macho kuna mawili; mwili(ndoa) kuumia kutokana na kujikwaa ama kufa kabisa kwa kutumbukia shimoni.

Ngoja niwambie; ndoa yeyote ambayo mwanamke amekaa kiuanaharakati uwe na uhakika ilishajifia siku nyingi ama iko njiani kufa na ukiona wanandoa wanaendelea kuishi pamoja basi ujue ni kwa "kujilazimisha".

Sijakutana na mwanamume yeyote duniani ambae anaweza kuishi kwa furaha nyumba moja na mwanamke anaeleta elements za uanaharakati ndani ya ndoa.

Ukiruhusu mwanamke ndani ya ndoa ajione anaweza kusimama bila wewe(mumewe) basi, ujue unacheka na nyani na muda wowote tutakuja tukusanye mabua tukalishie ng'ombe wetu.

Kuishi na mke hakuhitaji DEMOKRASIA, kunahitaji AKILI, ujinga unaofanywa na wanaume wengi siku hizi ni kuruhusu DEMOKRASIA kutawala ndoa badala ya AKILI.

Wewe kama unadhani demokrasia ndio uzungu na mapenzi kwa mkeo, shauri yako; hao wazungu unaowaigilizia ndoa zishawakimbiza siku nyingi.

Ninawaonya mapema ili nisije kusikia eti mtu ananiambia mke aliemtafuta na kumuoa mwenyewe, eti amemshinda.
 
Wanawake lazima tujikwamue kiuchumi hatutaki kupelekeshwa na maonevu ya wanaume kwenye mifumo dume. Ukiwa tegemezi lazima uonewe tu. Nawapongeza wanawake wachakarikaji wote.
Hafu mleta mada una inferiority complex inakusumbua tu hyo democracy yako haina uhalisia sema wanaume wengi mkizidiwa na wanawake hamjiamini. Hata utumie akili gan wanawake wa karne hii si wale wa dark ages
 
Tatizo mshakua wachoyo sana bana yani hata kijiko tu utasimangwa ndo maana wengine wanaamua kuwa na vyao......
Af kumradhi babu hayo maandiko yamesema tuwe wasaidizi kiuchumi?
 
Huo ni uongo tu.Hao wanawake unaowaita wachakarikaji huwategemea sana wanaume wawafanikishie mambo yao kwani wenyewe peke yao hawawezi kitu.Unakutana na mwanamke eti ni mfanyabiashara na anakwenda Dubai kuchukua mzigo lakini ukimfuatilia kwa makini utagundua kuwa Mtaji wake,nauli ya ndege, Malazi na chakula vyote anapewa na mwanaume/Wanaume, sasa hapo uchakarikaji upo wapi? Pia wanawake wanaowania nafasi za kisiasa kama ubunge na Udiwani wengi wao wamezipata kwa kuwezeshwa na wanaume, sasa uchakarikaji upo wapi hapo? Kwa ujumla wanawake wangekuwa wachakarikaji hasa kama unavyosema mbona basi hatuwaoni katika orodha ya juu ya matajiri duniani inayotolewa na jarida la FORBES? Any way wapo wanawake wachache sana wanaosimama kwa miguu yao wenyewe (Pongezi kwao) na idadi yao haizidi 2/100. Huu ni uchambuzi huru na wala hautawaliwi na mfumo dume/Jike.
 
Tatizo mshakua wachoyo sana bana yani hata kijiko tu utasimangwa ndo maana wengine wanaamua kuwa na vyao......
Af kumradhi babu hayo maandiko yamesema tuwe wasaidizi kiuchumi?

Sio uchumi tu bali kila kitu!
 
Ningewashauri tu vijana ambao bado hawana lifetime committments wasipitepite hili jukwaa.

Zimejaa frustration tu na vitisho...
 
Halafu wanawake wengi wakiwa na mapatp (Fedha) makubwa kuliko waume zao huwadharau sana na mwisho ndoa huvunjika kwani hulalamika kuwa wamechoka kuishi na wanaume mizigo. Ninazo takwimu nilizokusanya mwenyewe ambazo zinaonesha kuwa kuna wanaume wengi sana walio oa wanawake wasiofanya kazi za kuwaingizia kipato na wanaishi vizuri tu bila masimango wala nini.Lakini kuna wanawake wachache saaaana wanaofanya kazi na kuishi na wanaume wasio na kazi za kuwaingizia kipato, Kwa nini?
 
Unaelewa maana ya kula kwa jasho?
Cc Kaboom kwa ufafanuzi zaidi

Naelewa ila jasho la mwanamke linatakiwa liwe jembamba na chache kuliko la mwanaume, na ndiyo maana ya msaidizi! Kama uliwahikupata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya JKT utaelewa kwa urahisi ninachokisema hapa.
 
Huo ni uongo tu.Hao wanawake unaowaita wachakarikaji huwategemea sana wanaume wawafanikishie mambo yao kwani wenyewe peke yao hawawezi kitu.Unakutana na mwanamke eti ni mfanyabiashara na anakwenda Dubai kuchukua mzigo lakini ukimfuatilia kwa makini utagundua kuwa Mtaji wake,nauli ya ndege, Malazi na chakula vyote anapewa na mwanaume/Wanaume, sasa hapo uchakarikaji upo wapi? Pia wanawake wanaowania nafasi za kisiasa kama ubunge na Udiwani wengi wao wamezipata kwa kuwezeshwa na wanaume, sasa uchakarikaji upo wapi hapo? Kwa ujumla wanawake wangekuwa wachakarikaji hasa kama unavyosema mbona basi hatuwaoni katika orodha ya juu ya matajiri duniani inayotolewa na jarida la FORBES? Any way wapo wanawake wachache sana wanaosimama kwa miguu yao wenyewe (Pongezi kwao) na idadi yao haizidi 2/100. Huu ni uchambuzi huru na wala hautawaliwi na mfumo dume/Jike.

Wanawake wapo tu wachakarikaji hizo fursa wanazopewa ni kwa sababu ya jinsia zao na ndio mana mwanaume huwezi huwezi jilinganisha na mwanamke kwa mambo mengi. Sasa Mimi napata msaada rahisi ka tiketi niukatae kisa nini? Wanaume siku hizi mambo yenu yamekua magumu na wanawake si lazima wawe Forbes ndo waonekane wachakarikaji .
Na mtazidi sana kupitwa na wanawake mkitaka kujilinganisha labda mjigeuze jinsia mana nyie wabinafsi wakubwa.
 
Tatizo mshakua wachoyo sana bana yani hata kijiko tu utasimangwa ndo maana wengine wanaamua kuwa na vyao......
Af kumradhi babu hayo maandiko yamesema tuwe wasaidizi kiuchumi?
Teh teh..Nyie ndo wachoyo na wabinafsi..
 
Naelewa ila jasho la mwanamke linatakiwa liwe jembamba na chache kuliko la mwanaume, na ndiyo maana ya msaidizi! Kama uliwahikupata fursa ya kuhudhuria mafunzo ya JKT utaelewa kwa urahisi ninachokisema hapa.

Jasho la mwanamke liwe jembamba??? Na kazi ya kuzaa tunagawana?
 
Kwakweli hata aje nani sielewi, Mpendwa kuna wanaume wabinafsi wewe acha tu
Mpendwa kama unamwona mwanaume ni mbahili/mbinafsi unakubali kuolewa nae wa nn??..Hilo ni janga ofcoz..Ila kama mwanaume hakuwa mbahili kipindi cha mahusiano yenu ila akaanza tabia hiyo baada ya kuoana jua kuna uwezekano mke ndo kachangia tabia hiyo
 
Mpendwa maisha ya uboifrend na ugelofrend ni tofauti na maisha ya ndoa, ugelofrend na uboifrend mara nyingi ni fekelo life ukimwambia Bae nletee chips kuku analeta hata kama ni saa sita usiku, ila ndoani unaeza sema tu nna hamu na chips kuku ukajibiwa "qummmamae"
 
Back
Top Bottom