NECTA yawasihi wananchi kuendelea kuwapa taarifa kuhusu watumishi walioghushi vyeti

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,295
3,950

Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) linaendelea kuwatangazia wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine.

Tangazo hilo limetolewa na NECTA kupitia mtandao wake www.necta.go.tz hatua ambayo inaendeleza juhudi za kuwafichua watumishi ambao wanatumia vyeti ambavyo sio vyao.

Kwa mujibu wa tangazo hilo NECTA imewataka wananchi wenye malalamiko au taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine kuwasiliana nao kupitia barua pepe esnecta@necta.go.tz au simu namba +255 742 484 955.

Wananchi wametakiwa kufikisha malalamiko au taarifa hizo kwa kuzingatia muda wa saa za kazi kuanzia saa 2:30 Asubuhi hadi 10:30 jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Aidha, tangazo hilo limesisitiza kuwa kwa msaada zaidi wananchi wawasiliane nao kupitia barua pepe helpdesk@necta.go.tz au simu namba 0658 116 644 kwa saa za kazi.

Tangazo hilo linaendelea kutoa msisitizo kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa Machi 15, 2016 la kuhakiki watumishi wa Umma na kuwaondoa watumishi hewa ambao wamekuwa mzigo kwa Serikali yake.

Eleuteri Mangi, MAELEZO
 
upload_2017-3-6_14-25-53.jpeg
 
Hawa wanafiki tu.
Kwann wasilete uthibisho wa Daudi Bashite na Paul Christian?
Halafu kwann zoezi lao ni kwa wafanyakazi wa ngazi ya chini km walimu na madaktari? Sijasikia kuhusu majeshi na viongozi wa nchi.
Siwez kufanya hivyo. Zoezi si bado linaendelea? Watawapata huko huko kwenye zoezi lao
 
Mi namjua mmoja kafoji vyeti... Anaitwa daud bashite... Anzeni na huyo kama nyie wanaume kweli... Mnatuletea umbeambea wenu hapa...Kwan toka lini anatajwa mmenyamaza au mnataka malaika ashuke ndo awape taarifa... @@@@mbafu @@@
 
Nitareport watu watano wanaotumia vyeti feki endapo wataanza na bashite na kutupa mrejesho wa watakayobaini juu ya tuhuma hizi.
 
jaman maj ya shngo kwa daudi analia tu, cjui zuga au nin!, by the way naunga mkono vita dhd ya powda, ila ile stail ya daud kutaja taja majna ya watu tena wenye majna bila upelelez na kuwa na uhakika naikemea. Pole daudi punguza kujpendekeza kwa mkulu, fanya kaz, publicity nayo sio nzur
 
Hili tangazo halina nia njema na yule jamaa.......natamani Mimi ndio ningekuwa napokea hizo simu.
 
Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) linaendelea kuwatangazia wananchi kuendelea kuwapa ushirikiano kwa kutoa taarifa mbalimbli ikiwemo taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine.

Tangazo hilo limetolewa na NECTA kupitia mtandao wake www.necta.go.tz hatua ambayo inaendeleza juhudi za kuwafichua watumishi ambao wanatumia vyeti ambavyo sio vyao.

Kwa mujibu wa tangazo hilo NECTA imewataka wananchi wenye malalamiko au taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine kuwasiliana nao kupitia barua pepe esnecta@necta.go.tz au simu namba +255 742 484 955.

Wananchi wametakiwa kufikisha malalamiko au taarifa hizo kwa kuzingatia muda wa saa za kazi kuanzia saa 2:30 Asubuhi hadi 10:30 jioni kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa.

Aidha, tangazo hilo limesisitiza kuwa kwa msaada zaidi wananchi wawasiliane nao kupitia barua pepe helpdesk@necta.go.tz au simu namba 0658 116 644 kwa saa za kazi.

Tangazo hilo linaendelea kutoa msisitizo kufuatia agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alilolitoa kwa Wakuu wa Mikoa Machi 15, 2016 la kuhakiki watumishi wa Umma na kuwaondoa watumishi hewa ambao wamekuwa mzigo kwa Serikali yake.

Eleuteri Mangi, MAELEZO
mimi namjua mmojakwa sasa , MAKONDA tupeni ukweli tutawataja wengine, tunayo majina mengi tu, ila tuanze na huyo please
 
Kwa mujibu wa tangazo hilo NECTA imewataka wananchi wenye malalamiko au taarifa kuhusu watumishi walioghushi au kutumia vyeti vya watu wengine kuwasiliana nao kupitia barua pepe esnecta@necta.go.tz au simu namba +255 742 484 955.
ili tuamini kama NECTA watafanyia kazi taarifa zetu za kufchua wahalifu wenye vyeti feki au walionunua vyeti, tunataka kuona kwanza NECTA ikilifanyia kazi hili sakata la huyu mhalifu Bashite aliyetenda uhalifu wa kununua vyeti
 
Tuliwaambia fuatilieni mapolisi mmekaa macho kodo.
Kuna huyo Bashite mnaguna bado mnatuletea hadithi hapa.
Acheni utani fanyeni kazi.
 
What a shame! habari ya Bashite imeshasemwa kwa zaidi ya wiki mbili sasa, huku baadhi ya watu wakitoa ushahidi wa majina ya watu na shule walizosoma, ikiwa ni pamoja na matokeo ya mitihani yao. What else do you want? NECTA wangekuwa wa kwanza kusema kama taarifa hizo ni za kweli au za uongo. This is all political gimmicks.. my foot!
 
Back
Top Bottom