NECTA na mustakabali wa elimu-Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NECTA na mustakabali wa elimu-Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Brooklyn, May 11, 2009.

 1. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #1
  May 11, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Ni wiki moja hivi imepita toka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) litangaze matokeo ya kidato cha sita. Tukio hilo uambatana na wahitimu hao kukimbizana huku na kule katika harakati za kuhakikisha wana meet deadline za ujazaji na urejeshwaji wa fomu za maombi ya mikopo toka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) na maombi ya kujiunga na vyuo na taasisi mbalimbali za elimu ya juu ndani na nje ya nchi.

  Mmoja kati ya wahitimu hao ni binamu yangu mwenye umri wa miaka 42 anayeishi na kufanya kazi mkoani Shinyanga. Baada ya kukaa zaidi ya miaka 20 akaamua aongeze ujuzi na akajiunga na masomo ya kidato cha tano na sita. Baada ya mama Joyce Ndalichako (CEO-NECTA) kutangaza kutoka kwa matokeo hayo, huyu ndugu akakimbia kwenda kuangalia matokeo yake kwenye internet na kukuta ana Division Two point 10 (Hist C, Kisw D & Lang C). Jamaa akafurahi kupita kiasi na kunijulisha kuhusu matokeo hayo na kuniomba nimchukulie fomu za mikopo na fomu za kujiunga na vyuo walau vinne, huku akiahidi kuwa anajitahidi akopekope pesa kwa ndugu na marafiki ili apate nauli za kuja DSM kufuatilia Results slip na kulipia application fees za vyuo na bodi ya mikopo.

  Mungu akamsaidia akapata kama Tzs. 250,000, na kuwasili DSM siku ya Jumatano ya tarehe 6/5/2009. Alhamisi akaitumia kwenda benki kulipia hizo fees kwa ajili ya kusubmit filled forms ili ameet hizo deadline. Ijumaa akaenda kufuatilia result slip yake na cha kushangaza akakuta matokeo tofauti kabisa ktk slip hiyo. Matokeo yaliyoandikwa ktk slip ni Division four ya mwisho kabisa. Jamaa presha imepanda, deni ndo hilo tena inabidi lilipwe kutoka kwenye kijimshahara kidogo cha ualimu wa shule ya msingi.

  Sasa najiuliza hivi inakuwaje NECTA wafanye makosa kama haya ambayo yanaweza kuepukwa kabisa?? Kwenye makosa kama haya ni watanzania wangapi wanapewa matokeo ambayo si yao?? Kuhusu huu usumbufu na hasara wanayopata wahitimu na wazazi wao nani anawajibika?? Ni aina gani ya professionals tunaowatengeneza katika mazingira kama haya?? Kama baraza linashindwa na kumatch matokeo ya watahiniwa wake ambao hawazidi hata 60,000 je watawezaje kucontrol vyeti feki vilivyozagaa nchi nzima???

  Wakuu nauliza haya ndio maisha bora kwa kila mdanganyika???
   
 2. MmasaiHalisi

  MmasaiHalisi Senior Member

  #2
  May 11, 2009
  Joined: Jan 15, 2009
  Messages: 192
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo baraza la mitihani inabidi livunjwe,Dr Ndalichako hana jipya yeye anachojua kufukuza wafanyakazi na ameajiri watu Bogus kama Daniel Mafie(Director of Finance and Administration)na Kihanga (Human Resource Officer(sio raia wa tanzania ni mtusi) na wengine wengi ambao wameguza baraza la mitihani kama soko la kariakoo
   
 3. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #3
  May 11, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,868
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 160
  Kuna wakati ktk historia Tz hili baraza limewahi kukosa malalamiko?
   
 4. A

  August JF-Expert Member

  #4
  May 17, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Nini ubogus wa DF? maana umeweka taarifa nusu hyo mwingine angalau umesema sio raia
   
 5. A

  August JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  kwa tatizo kama hili na sisi tuwe waangalifu kabla ya kutoa huku, namba yake ukiiangalia na Matoke yake kwenye internet ni sawa na ya kwenye slip? maana katika kiwehuwehu cha kuangalia matokeo kwenye internet unaweza angalia ya mtu mwingine na inapofika kwenye reality namba yako ni nyingine, maana kama nikweli kuna makosa kama hayo mwambie nuduguyo aprint ya kwenye internet na alinganishe na hayo wa kwenye slip
   
Loading...