mara nyingi nimekuwa nikijiuliza kwa nini baraza la mitihani la Taifa linaonesha majina ya watahiniwa wakati wa kutoa matokeo. mimi kwa mtazamo wangu naona matokeo ya mtahiniwa ni siri kati yake na baraza (au mwalimu na mwanafunzi) au pia mtu/watu ambao mtahiniwa ameridhia au anawajibika kwake/kwao. kwenye vyuo, zamani kabla ya kuenea kwa huduma za mawasiliano ya internet walikuwa wanaweka matokeo ya wanafunzi kwa karatasi zenye kuonesha namba tu za watahiniwa na matokeo yao, ambapo kwa sasa mwanafuzi anakuwa na account yake kwa internet ambapo huweza kuangalia matokeo yake popote pale alipo kwenye huduma hiyo. baraza la mitihani linaweka matokeo kwenye website yake ambayo yana majina ya watahiniwa, nadhani wangebadilisha utaratibu na kuweka namba tu ya mtahiniwa na matokeo yake, na hiki kitu walikifanya kama miaka 3 iliyopita (sina uhakika), sasa sijui kwa nini warerudia tena huu mfumo wa kuanika majina ya watahiniwa, anayefahamu anaweza kunielewesha. hii inachochea watu kufatilia hata matokeo ya watu yasiyowahusu kwenye mitandao kisa tu wanaishi mtaa mmoja au sababu nyingine za kijinga, na pia inasababisha mateso ya kisaikolojia na aibu kwa familia hasa kwa wale wanafunzi wenye matokeo mabaya. wangesambaza vitabu vyenye majina na matokeo huko mashuleni kisha kwenye website waweke namba na matokeo tu, mwanafunzi mwenye wasiwasi na matokeo yake anaweza kuwasiliana na shule yake kwa uthibitisho.
utaratibu wa sasa ni sawa kwani umeturahisishia sisi wazazi na walezi kufuatilia matokeo ya watoto wetu kwa urahisi. Awali tulikuwa tunadaganywa kwa kupewa namba za uongo na hivyo kutojua matokeo. Njia nzuri ya kuondokana na aibu ni kujitahidi katika masomo.
Utaratibu huu wa sasa ni mzuri na uendelee.
Kuna watu hapa nilipo wanafanya mtihan wa taifa,,,,,lakin ukimuuliza wewe INDEX NO:YAKO NGAPI HAKUMBUKI,,,,JE WAKIWEKA NAMBA KWENYE MATOKEO,,,,UNADHAN ITAKUWAJE????na wapo ambao wanajikuta wanaandika namba si zao,,,so mfumo wa majina uko palepale,hata wakitoa kwa namba still utaona tu
utaratibu wa sasa ni sawa kwani umeturahisishia sisi wazazi na walezi kufuatilia matokeo ya watoto wetu kwa urahisi. Awali tulikuwa tunadaganywa kwa kupewa namba za uongo na hivyo kutojua matokeo. Njia nzuri ya kuondokana na aibu ni kujitahidi katika masomo.
Utaratibu huu wa sasa ni mzuri na uendelee.