Necta kupandishwa mahakamani zanzibar

Status
Not open for further replies.

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
WALIMU wa Shule za Sekondari na wazee wa watoto waliofutiwa matokeo ya mitihani ya kidato cha nne Zanzibar, wanakusudia kulishitaki mahakamani Baraza la Mithani la Taifa (Necta) kwa kutoa adhabu ya ujumla kwa wanafunzi ambayo ni kinyume na sheria za nchi.

Wazee hao pamoja na walimu walitoa msimamo huo katika ukumbi wa Baitul-Yamin karibu na Hoteli ya Bwawani, Zanzibar, ambapo palikuwa na mjadala wa wazi kuhusiana na kadhia hiyo ya kufutiwa watoto wao mitihani.

Bila ya kutaja kifungu gani katika sheria za makosa ya jinai, washiriki wa mjadala huo walieleza kuwa kwa mujibu wa sheria hiyo ni kosa kutoa hukumu za jumla.

Walisema Necta hawezi kuwafutia watoto wote kwakosa la mtu mmoja na pia kuwazuia kufanya mitihani kwa muda wa miaka mitatu.

“Wanaovujisha mitihani ni wao halafu wanakwenda kuwafutia watoto wetu matokeo na uzembe ni wao, kwa hili hatuwezi kukubali,” alisema mzee Ali Hassan ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kati.

Mzee Hassan alifahamisha kuwa mtoto wake yeye alikuwa anashika nafasi za mwanzo katika matokeo ya mitihani darasani lakini Necta wanasema hana uwezo.

“Hawezi mtu na akili zake kuandika nyimbo za bongo fleva wakatumia fursa hiyo kuwakandamiza wengine, hiyo ni mipango yao katika kuwafelisha watoto wetu,” alieleza mzee Hassan.

Wazee na walimu hao waliitaka Necta kupeleka katika shule zote ushahidi wa karatasi za mitihani zilichafuliwa kwa kuandika mambo ambayo hayahusiani na majibu.

Kwa upande wao, waalimu ambao washiriki katika kusahihisha mitihani walisema walimwambia Katibu wa Necta, Dk Joyce Ndalichako kuwa mitihani imevuja lakini yeye alikataa.

“Tulimwambia mithani imevuja ni vyema ikarudiwa kulikoni kuwafutia matokeo kwa baraza halitotenda haki hapo,” alifahamisha mwalimu wa shule ya Laurent, Hemmed Soud.

Alisema wanachofanya Necta ni kuua maendeleo ya elimu katika visiwa vya Zanzibar ili ionekane kuwa hukuna wataalamu.

Mwalimu huyo alidai suala la kutembelea katika mikoa tofauti Katibu huyo wa Necta ni kuweka kiini macho tu.

Tangu kutangazwa kwa matokeo ya mitihani hiyo zaidi ya wiki moja sasa, kumekuwa na mijadala mizito kufuatia watoto 3,301 kufutiwa matokeo yao kwa kile kinachodaiwa kwa kufanya udanganyifu
 
"Wanaovujisha mitihani ni wao halafu wanakwenda kuwafutia watoto wetu matokeo na uzembe ni wao, kwa hili hatuwezi kukubali," alisema mzee Ali Hassan ambaye aliwahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kat
offcourse huyu mzee hapa kaongea point..uzembe wao halafu sisi tuteseka na wao waendelee kula bata kwenyeviyoyozi.
 
Hivi necta siku hizi wanatunga maswali kutoka kwenye biblia? kama ndio hivyo basi wapandishwe kizimbani maana hawa watoto watakuwa wameonewa tu.

Tena ya katoliki.maana shule za KKT ,wasabato , ziro tupu
 
nawaunga mkono kwa asilimia mia hao wanataka kulishtaki baraza la mitihani.hili baraza limekuwa likiumiza watu kwa muda mrefu bila kufikishwa popote.nadhani hii itakuwa fundisho kwa siku za usoni
 
nawaunga mkono kwa asilimia mia hao wanataka kulishtaki baraza la mitihani.hili baraza limekuwa likiumiza watu kwa muda mrefu bila kufikishwa popote.nadhani hii itakuwa fundisho kwa siku za usoni

Inasemakana mama huyu anataka ubunge huko kwao. kwao kapeleka div 1 kwengine kapeleka o. Matokeo ya f4 siku hizi yanapngwa nyumbani kwa Ndalichako, na sio ofisini tena
 
wewe mji mkongwe umeleta thread hapa halafu umeanza mwenyewe kuichakachua ...itafugwa sasa sijui itakuwa ni faida ya nani...ukileta thread usilete udini au kashfa
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom