NECTA imeficha ukweli?

b191

JF-Expert Member
Jul 24, 2016
742
1,031
Amani na Upendo viwe nanyi nyote.

Jana BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA lilitangaza matokeo ya KIDATO CHA PILI 2016 na kuonyesha ufaulu umeongezeka kwa 2% ya ule wa Mwaka Juzi 2015.

Naomba nianze kwa ufafanuzi kidogo.

ALAMA MPYA ZA UFAULU.
A = 75-100 > ALAMA 1
B = 65-74 > ALAMA 2
C = 45-64 > ALAMA 3
D = 30-44 > ALAMA 4
F = 00-29 > ALAMA 5

DIVISION POINT
I 7 - 17
II 18 - 21
III 22 - 25
IV 26 - 33
0 34 - 35

Mfano:
Mwanafunzi anayeitwa: KILAZA MKUBWA amepata alama zifuatazo;
SOMO ALAMA GRADE
CIVICS 30 D = 4
HISTORY 30 D = 4
GEOGRAPHY 30 D = 4
KISWAHILI 45 C = 3
ENGLISH 40 D = 4
PHYSICS 20 F = 5
CHEMISTRY 20 F = 5
BIOLOGY 15 F = 5
B/MATH 11 F = 5

>KWA NJIA YA WASTANI.
JUMLA YA ALAMA NI 241
GAWANYA KWA MASOMO 9
WASTANI 26.7..

• KWA KUTUMIA WASTANI HUYU MWANAFUNZI AMEFELI (WASTANI WA KUFAULU NI 30)

>KWA NJIA YA DIVISION
POINT = 29 (YANAHESABIWA MASOMO 7 ALIYO FAULU VIZURI ZAIDI)
DIVISION = IV

• KWA KUTUMIA MFUMO HUU HUYU MWANAFUNZI AMEFAULU (KWA SABABU HAJAPATA DIVISION ZERO)

NECTA wametumia mfumo wa POINTS na DIVISION kutoa Matokeo ya Kidato Cha Pili badala ya mfumo wa WASTANI uliozoeleka ili kuongeza Asilimia ya Waliofaulu.

Ungetumika mfumo wa Wastani uhalisia ungejidhihirisha.

TAZAMA MFANO PALE JUU kama mwanafunzi mwenye POINTS 29 na DIVISION IV ambaye amefaulu. Lakini kwa kutumia mfumo wa Wastani anaonekana amefeli. Je mwenye POINTS 30, 31, 32 na 33 hali ikoje?

Ninachojiuliza, Je NECTA imeamua kuficha ukweli wa ufaulu wa Kidato Cha Pili kwa kuamua kutumia mfumo wa DIVISION na siyo WASTANI?

Nawasilisha.
 
Huyu bibi atafukuzwa kama enzi za Kikwete. ...ngoja aendeleze Uzombie wake ...ila kwa uongozi huu wa Pomb@ anaweza kupewa sifa yaan full Bange. ..
 
Watu wengine tulisoma kuanzia form 1 mpaka 4 bila kushika simu tena mpaka pesa ya nauli ya kurudia kwenu unaiacha getini umeandikisha.......

Watoto Wa siku hizi nao ni vilaza sana....

Kazi ya kufundisha ni ngumu sana hiki kizazi cha 4G.....

Matoto ya miaka 12 unakuta wameshikilia iPad wanaangalia picha za ngono uje ufaulu Kwa ufasaha sangapi?......

Ndalichako ana Kazi sana kuinyoosha elimu maana tatizo kubwa lipo Kwa wanafunzi wenyewe.......
 
Nimerudi tena,
Sasa mkuu tutakuamini vipi,
Weka hapa matokeo ya 2015 na 2016 tulinganishe ilikupata uhakika
 
Amani na Upendo viwe nanyi nyote.

Jana BARAZA LA MITIHANI LA TANZANIA lilitangaza matokeo ya KIDATO CHA PILI 2016 na kuonyesha ufaulu umeongezeka kwa 2% ya ule wa Mwaka Juzi 2015.

Naomba nianze kwa ufafanuzi kidogo.

ALAMA MPYA ZA UFAULU.
A = 75-100 > ALAMA 1
B = 65-74 > ALAMA 2
C = 45-64 > ALAMA 3
D = 30-44 > ALAMA 4
F = 00-29 > ALAMA 5

DIVISION POINT
I 7 - 17
II 18 - 21
III 22 - 25
IV 26 - 33
0 34 - 35

Mfano:
Mwanafunzi anayeitwa: KILAZA MKUBWA amepata alama zifuatazo;
SOMO ALAMA GRADE
CIVICS 30 D = 4
HISTORY 30 D = 4
GEOGRAPHY 30 D = 4
KISWAHILI 45 C = 3
ENGLISH 40 D = 4
PHYSICS 20 F = 5
CHEMISTRY 20 F = 5
BIOLOGY 15 F = 5
B/MATH 11 F = 5

>KWA NJIA YA WASTANI.
JUMLA YA ALAMA NI 241
GAWANYA KWA MASOMO 9
WASTANI 26.7..

• KWA KUTUMIA WASTANI HUYU MWANAFUNZI AMEFELI (WASTANI WA KUFAULU NI 30)

>KWA NJIA YA DIVISION
POINT = 29 (YANAHESABIWA MASOMO 7 ALIYO FAULU VIZURI ZAIDI)
DIVISION = IV

• KWA KUTUMIA MFUMO HUU HUYU MWANAFUNZI AMEFAULU (KWA SABABU HAJAPATA DIVISION ZERO)

NECTA wametumia mfumo wa POINTS na DIVISION kutoa Matokeo ya Kidato Cha Pili badala ya mfumo wa WASTANI uliozoeleka ili kuongeza Asilimia ya Waliofaulu.

Ungetumika mfumo wa Wastani uhalisia ungejidhihirisha.

TAZAMA MFANO PALE JUU kama mwanafunzi mwenye POINTS 29 na DIVISION IV ambaye amefaulu. Lakini kwa kutumia mfumo wa Wastani anaonekana amefeli. Je mwenye POINTS 30, 31, 32 na 33 hali ikoje?

Ninachojiuliza, Je NECTA imeamua kuficha ukweli wa ufaulu wa Kidato Cha Pili kwa kuamua kutumia mfumo wa DIVISION na siyo WASTANI?

Nawasilisha.
serikali ilifundishwa uongo tangu tumboni mwa mama yake.
hivyo haiwezi kukuambia ukweli
 
Nimerudi tena,
Sasa mkuu tutakuamini vipi,
Weka hapa matokeo ya 2015 na 2016 tulinganishe ilikupata uhakika
Nimejaribu kuweka mchanganuo mdogo hapo juu. Nadhani umeuelewa.
 
Mfumo wa madaraja ni mzuri tu, tena watoto wanapata ka feeling jinsi matokeo yao yatavyo kokotolewa form 4. Hivi kwanini watu ni walalamishi sana??? Au mngependa aache zile GPA na div 5??? Mama wa watu anajitahidi ku balance mambo pamoja na ukata uliopo lakini ninyi hamlioni hilo. Pengine akili zenu ni ndogo hamuvezi hata kutafakati vitu kwa kina!!
 
Asante mkuu kwa kuliona hilo.
Wangetumia wastani yakuwa majanga, ingawa bado ni majanga hadi sasa.
Shida ni kwamba, watoto hawa (walioko gvt schools) wamenyimwa nafasi ya kufundishwa masomo muda wa ziada kwa sababu ya elimu bure. Walimu tunafundisha muda wa kawaida tu. Labda niamue kujitolea mara chache chache.
Kwa hiyo muda mwingi watoto wanarandaranda mitaani(wale wa shule za day)
Kuificha aibu hii inayoletwa na ubure wa elimu wakaamua kubadili mfumo wa kuwakaririsha watoto kidato.
Katoto kana D mbili kanaingia fm 3. Ngoja tusubiri matokeo yao tena 2018/2019
 
Mfumo wa madaraja ni mzuri tu, tena watoto wanapata ka feeling jinsi matokeo yao yatavyo kokotolewa form 4. Hivi kwanini watu ni walalamishi sana??? Au mngependa aache zile GPA na div 5??? Mama wa watu anajitahidi ku balance mambo pamoja na ukata uliopo lakini ninyi hamlioni hilo. Pengine akili zenu ni ndogo hamuvezi hata kutafakati vitu kwa kina!!
Mbona hujatafakari kwa kina ukapendekeza wastani ungekuwa 30?
Mleta mada ameweka mfano vizuri tu we unakuja na mashambulizi kama haya.
Kupata wastani chini ya 30 ni wastani wa F. Huyu mtoto unategemea makubwa kutoka kwake?
 
Nimerudi tena,
Sasa mkuu tutakuamini vipi,
Weka hapa matokeo ya 2015 na 2016 tulinganishe ilikupata uhakika
Matokeo ya fm 2 kabla ya 2016 yalikuwa yanatumia wastani wa masomo aliyofanya mwanafunzi. Wanaweka alama za kila somo na kuutafuta wastani.
Mwaka 2016 wametumia divisions. Ili upate div, unahesabia masomo 7 aliyofanya vizuri mwanafunzi. Div Zero mwanafunzi amefeli.
Kwa hiyo sio rahisi kulinganisha matokeo ya miaka miwili wakati ukokotozi wake ni tofauti.
Nakaribisha kukosolowa
 
Chini ya Waziri Ndalichako sidhani kama kuna njama za kuficha ukweli hasa linapokuja suala la ufaulu wa wanafunzi. Kwenye Mengine anaweza akawa kaboronga.
Ndalichako keshalishwa unga wa ndele(kaharibiwa) na mfumo si yule tena
 
Chini ya Waziri Ndalichako sidhani kama kuna njama za kuficha ukweli hasa linapokuja suala la ufaulu wa wanafunzi. Kwenye Mengine anaweza akawa kaboronga.
Kha! Wee umeisoma vzr hiyo post! Ndalichoko ni binadamu lolote linawezekana kwake.
 
Matokeo ya fm 2 kabla ya 2016 yalikuwa yanatumia wastani wa masomo aliyofanya mwanafunzi. Wanaweka alama za kila somo na kuutafuta wastani.
Mwaka 2016 wametumia divisions. Ili upate div, unahesabia masomo 7 aliyofanya vizuri mwanafunzi. Div Zero mwanafunzi amefeli.
Kwa hiyo sio rahisi kulinganisha matokeo ya miaka miwili wakati ukokotozi wake ni tofauti.
Nakaribisha kukosolowa
Asante mkuu kwa kunielewa.
 
Kwa haya matokeo ya kupikwa ili ionekane ufaulu umeongezeka wakuu wa mikoa wawe wanachapa barua za kuachisha wakuu wa shule nyadhifa zao kabisa kwa mwaka kesho,Kwan matokeo ya form 4 mwakan huenda yakawa kichekesho_Onyo achen siasa kwenye elimu ya wadogo zetu,siasa mahali pake jukwaani.
 
Back
Top Bottom