NEC:Tutatoa maelezo mgombea ubunge Korogwe

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,957

TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imesema bado inaendelea kulifanyia kazi sakata la mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Jimbo la Korogwe Vijijini mkoani Tanga, Timotheo Mnzava kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi mdogo ujao. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk Athumani Kihamia, alilieleza Habari- Leo jana kuwa muda ukifika, watalitolea maelezo jambo hilo, lakini kwa sasa hawezi kusema lolote kwa vile linafanyiwa kazi.

Sakata hilo la Mnzava kuwa mgombea pekee wa ubunge kwenye jimbo hilo, limekuja baada ya fomu ya mgombea huyo kuwa pekee iliyorudishwa kwa wakati katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo saa 10 jioni Agosti 20, mwaka huu. Wagombea wengine kutoka vyama vya upinzani kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walidaiwa kushindwa kurejesha fomu zao ndani ya muda huo.

Wagombea walioshindwa kurejesha fomu zao kwa wakati na vyama vyao kwenye mabano ni Amina Saguti (Chadema), Abdulazizi Abdallah Mahamoud (AAFP), Josephine Mpalahingwe (DP), Shabani Karata (ACT), Nurdin Mshangama (CUF), Catherini Mpalahingwe (SAU) na Juma Gao (ADA-TADEA). Wakati Dk Kihamia akisema kuwa suala la Mnzava kupita bila kupingwa litatolewa maelezo baadaye, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Kwame Daftari, alinukuliwa na gazeti hili juzi akisema kuwa wagombea hao, wana nafasi ya kufuata ngazi za kisheria ili kuwasilisha malalamiko yao. Kwa mujibu wa Daftari, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, ilipofika saa 10 jioni ya Agosti 20, mgombea aliyekuwa amerejesha fomu alikuwa ni mmoja tu, ambaye ni Mnzava wa CCM.

HABARI LEO
 
huyu Dr .Athumani Kihamia aliteuliwa kwa mkakati maalumu, tangu ateuliwe mwenyekiti wa tume ni kama kawekwa benchi na mambo ya ajabu yameshamiri NEC, inatia aibu na kwakweli.
 
TUME ya Taifa ya Uchaguzi nchini (NEC) imesema bado inaendelea kulifanyia kazi sakata la mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Jimbo la Korogwe Vijijini mkoani Tanga, Timotheo Mnzava kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi mdogo ujao. Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk Athumani Kihamia, alilieleza Habari- Leo jana kuwa muda ukifika, watalitolea maelezo jambo hilo, lakini kwa sasa hawezi kusema lolote kwa vile linafanyiwa kazi.
Sakata hilo la Mnzava kuwa mgombea pekee wa ubunge kwenye jimbo hilo, limekuja baada ya fomu ya mgombea huyo kuwa pekee iliyorudishwa kwa wakati katika ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi wa jimbo hilo saa 10 jioni Agosti 20, mwaka huu. Wagombea wengine kutoka vyama vya upinzani kikiwemo Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), walidaiwa kushindwa kurejesha fomu zao ndani ya muda huo.
Wagombea walioshindwa kurejesha fomu zao kwa wakati na vyama vyao kwenye mabano ni Amina Saguti (Chadema), Abdulazizi Abdallah Mahamoud (AAFP), Josephine Mpalahingwe (DP), Shabani Karata (ACT), Nurdin Mshangama (CUF), Catherini Mpalahingwe (SAU) na Juma Gao (ADA-TADEA). Wakati Dk Kihamia akisema kuwa suala la Mnzava kupita bila kupingwa litatolewa maelezo baadaye, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Kwame Daftari, alinukuliwa na gazeti hili juzi akisema kuwa wagombea hao, wana nafasi ya kufuata ngazi za kisheria ili kuwasilisha malalamiko yao. Kwa mujibu wa Daftari, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, ilipofika saa 10 jioni ya Agosti 20, mgombea aliyekuwa amerejesha fomu alikuwa ni mmoja tu, ambaye ni Mnzava wa CCM.
HABARI LEO
Inaoneka Dkt Mzava ni CCM kindaki ndaki!
 
Tunajua Maelezo watakayo toa Tume huo Wakati ukifika hayata tofautiana na Hali ilivyo kwa sasa ,mwendo wa sasa ni kupita bila ya kupingwa.Tuna endelea kuweka tu kumbukumbu sawa.
 
Wagombea walioshindwa kurejesha fomu zao kwa wakati na vyama vyao kwenye mabano ni Amina Saguti (Chadema), Abdulazizi Abdallah Mahamoud (AAFP), Josephine Mpalahingwe (DP), Shabani Karata (ACT), Nurdin Mshangama (CUF), Catherini Mpalahingwe (SAU) na Juma Gao (ADA-TADEA). Wakati Dk Kihamia akisema kuwa suala la Mnzava kupita bila kupingwa litatolewa maelezo baadaye, Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Kwame Daftari, alinukuliwa na gazeti hili juzi akisema kuwa wagombea hao, wana nafasi ya kufuata ngazi za kisheria ili kuwasilisha malalamiko yao. Kwa mujibu wa Daftari, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, ilipofika saa 10 jioni ya Agosti 20, mgombea aliyekuwa amerejesha fomu alikuwa ni mmoja tu, ambaye ni Mnzava wa CCM.
HABARI LEO
Hapa ni maigizo tu, labda utokee muujiza. Yaani wagombea wote 7 wa upinzani hawajui wapi pa kurudisha fomu wakiwa eneo husika kwa masaa zaidi ya 4, lakini wa CCM pekee ndiye alikuwa na taarifa sahihi. Fikiria ina maana walisahau hata offisi waliyopewa fomu na pia aliye wapa fomu. Huyu Kwame Daftari na Bosi wake Kihamia wanatufanya sisi wengine wajinga kabisa. Kihamia alishatuambia jamaa wanacheza filamu na sasa anatuambia wanachunguza. Itakuwa muujiza kama atakula matapishi yake. Wote walitakiwa wachunguzwe na kamati huru na wakikutwa na kosa watimuliwe.
 
Kuna vitu vingine vinatakiwa vifanywe na mtu ambaye uwezo wake wa kufikiri unashida kubwa (mental disability)! Pale tume pamejaa wasomi wa sheria na uongozi waliobobea lakini implementations ya walichokisoma ni minus zero!
Hebu mamlaka zinazomsimamia yule das wa korogwe wampe semina elekezi kwani rafu anazocheza ni za wazi mno ambazo kila mwenye uelewa anaziona na kuikebehi na kuidharau tume! Natamani wale majaji waliopo pale wajiuzulu ili kuzilinda heshima zao!
 
..yaani wagombea wa vyama saba wote wapotee njia na kukosea ofisi wanapotakiwa kurudisha fomu?

..lakini wagombea haohao siku ya kuchukua fomu hawakuwa na tatizo lolote lile, walifika bila kupotea ktk ofisi husika.

..Yaani mtu apotee kwa muda wa masaa zaidi ya manne ktk mji mdogo huko Korogwe Vijijini?
 
Kuna vitu vingine vinatakiwa vifanywe na mtu ambaye uwezo wake wa kufikiri unashida kubwa (mental disability)! Pale tume pamejaa wasomi wa sheria na uongozi waliobobea lakini implementations ya walichokisoma ni minus zero!
Hebu mamlaka zinazomsimamia yule das wa korogwe wampe semina elekezi kwani rafu anazocheza ni za wazi mno ambazo kila mwenye uelewa anaziona na kuikebehi na kuidharau tume! Natamani wale majaji waliopo pale wajiuzulu ili kuzilinda heshima zao!

Mkuu watajiuzulu wakale wapi? Hao wanasheria wanatumikia matumbo hivyo weledi umefutika.
 
Mimi binafsi sifurahii mkurugenzi wa halmashauri kuhusika katika chaguzi zetu, ukweli ulio wazi kuwa hawezi kutenda haki. Na pia NEC du ni majanga........

Sent from my Infinix-X551 using Tapatalk
 
Back
Top Bottom