Mabibi na mabwana heshima kwenu na moja kwa moja kwenye mada.
Ninaamini kumekuwapo na kujizuia kwa hali ya juu wanazuoni wanaita subira kutoka kwa wanaoathirika moja kwa moja na maamuzi yenu na kwa muda mrefu tu.
Jamani tusiache subira hizi kufika ukomo.
NEC na ZEC mnayo sababu na uwezo wa kuiepushia shari nchi hii. Kinachoombwa kwenu mbona ni kidogo mno na cha msingi tu?
"Mnaombwa uchaguzi ulio huru na wa haki." Ni hivyo tu basi. Si zaidi wala si pungufu.
Haki huambatana na jitihada za wazi kuielekea kuonekana kuwa kweli zinafanyika. Hapa tulipo ni muhimu sana sasa mkawarejesha wale wagombea wote walioenguliwa na hasa wale wanaolalamika kutokutendewa haki.
Inafahamika kuwa wapo wagombea walionunuliwa ili waenguliwe. Hao kama takukuru kaona ni sawa waacheni takukuru watabeba mzigo wao wenyewe.
Hivi, mtapata hasara gani kwa kuchukua msimamo kama huo wa kuwarejesha wagombea wanaolalamika, ambao mh. Jaffo alipata kuutumia kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita?
Uchaguzi 2020 - Tume ya Uchaguzi ya uenguaji, somo la Jaffo haliwafai?
Pana vyama wagombea wao wako kwenye media zote muda wote na hata wakitumia lugha za makabila yao kutoa kejeli, vitisho na labda hata matusi. Yaliyotokea kanda ya ziwa na hata yanayoendelea hasa Tarime ni mfano mzuri wa hali ilikofikia.
Pana vyama vinaminywa na kunyimwa fursa zote. Majukumu yenu nyie kama wenye mamlaka na uchaguzi huu ni nini kama hamuwezi kutuwekea mazingira yaliyo sawa, huru wala ya haki?
Mbona Sirro amejitahidi na juhudi zake walau zinaonekana?
Pongezi Sirro, Mahakama na Tume ya Uchaguzi kazi kwenu
Nakazia - NEC na ZEC msiache tufikie kuwapa makavu tunapoendelea kujizuia tukitegemea haki kutoka kwenu.
Ninawasilisha.