Uchaguzi 2020 NEC imepokea rufaa 557 za mapingamizi, na imeanza kuzifanyia kazi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Katika Uteuzi wa wabunge na madiwani uliokamilika Agosti 26, 2020 wabunge kadhaa waliwekewa mapingamizi hali iliyofanya baadhi ya majimbo kuwa na wagombea wa chama kimoja tu

Agosti 28, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitangaza majimbo 18 ambayo wagombea wake wamepita bila kupingwa kutokana na sababu mbalimbali kwa kuzingatia Sheria ya Taifa ya Uchaguzi

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage amesema hadi sasa tume hiyo imepokea rufaa 557 za mapingamizi katika upande wa udiwani na ubunge

Rufaa hizo zimeanza kufanyiwa kazi kuanzia Septemba 01, 2020 kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizopo

#JFLeo #JamiiForums #Uchaguzi2020 #TZ2020
 
🛑BREAKING NEWS:

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC ) Jaji Semistocles Kaijage, amesema Tume imepokea Rufaa (mapingamizi) katika ngazi ya Ubunge na Udiwani 557 hadi sasa , nakusema kuwa Tume inaanza kusikiliza na kuzishughulikia Rufaa hizo mara moja kuanzia leo hii https://t.co/AtjrVGdDG9
 
BREAKING NEWS:

Baada ya kupokea maalekezo ili waweze kuyafanyia kazi kutoka ndani ya kikao cha hivi karibuni cha KK ya halmashauri kuu ya taifa ya CCM.
 
Ningependa kuwauliza Tume ya Uchaguzi, je fomu za wagombea zilizotumika 2015 zina tofauti kubwa sana na zilizotumika mwaka huu? Iweje mwaka huu tu ndio wapinzani wakosee kujaza fomu kwa kiwango kikubwa kiasi hicho na CCM wawezee?

Narudia, kosa kubwa lililofanyika ni kuwapa immigrants jukumu la kuongoza nchi hii!
 
BREAKING NEWS:

Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC ) Jaji Semistocles Kaijage, amesema Tume imepokea Rufaa (mapingamizi) katika ngazi ya Ubunge na Udiwani 557 hadi sasa , nakusema kuwa Tume inaanza kusikiliza na kuzishughulikia Rufaa hizo mara moja kuanzia leo hii https://t.co/AtjrVGdDG9
Hawana hata haya wafute zote watu waingie ulingoni kama ni kushinda washinde kwa kura za wananchi Haki huinua Taifa
 
Ngoja tusubirie maagizo ya kikao cha juzi kamati kuu ccm...maana NEC ni sawa tu na jumuia zingine za chama.
 
Back
Top Bottom