Nduguye shahidi Lema naye afariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nduguye shahidi Lema naye afariki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Limbukeni, Apr 7, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. L

  Limbukeni Senior Member

  #1
  Apr 7, 2009
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nduguye shahidi Lema naye afariki

  2009-04-05 11:50:08
  Na Mwandishi Wetu, Jijini


  Raphael Mtaki ambaye ni ndugu wa karibu wa yule shahidi muhimu katika kesi ya akina Zombe, Rashidi Lema, aliyefariki jana katika Hospitali ya Ocean Road ya Jijini Dar es Salaam, naye amepoteza maisha katika hali ambayo inazua utata mkubwa.

  Taarifa ambazo Alasiri imezipata zinadai kuwa ndugu huyo wa marehemu Lema, Raphael Mtaki alipoteza maisha baada ya kupigwa risasi na watu wasiofahamika.

  Kwa mujibu wa taarifa hizo, mauaji hayo ya kimya kimya yalitokea huko Kimara Kibanda cha Mkaa alikokuwa akiishi marehemu.

  Inadaiwa kuwa Mtaki aliuawa wiki iliyopita kwa kupigwa risasi na watu walioonekana kukusudia roho yake tu.

  Chanzo cha gazeti hili kimedai kuwa ndugu huyo wa marehemu Lema, alikuwa mbioni kumalizia masomo ya shahada ya kwanza ya sheria katika Chuo Kikuu Huria, OUT.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu, ni kwamba ndugu huyo wa Lema alivamiwa na watu wasiofahamika usiku wakati akiwasili na gari nyumbani kwake, huku akiwa amempakia mkewe.

  ``Hao jamaa walitokea ghafla, wakampiga risasi yeye tu na kisha, bila kuchukua chochote kile, wakatokomea kusikojulikana,`` kikadai chanzo hicho.

  Aidha, imedaiwa kuwa mwili wa ndugu huyo wa marehemu Lema ulisafirishwa Jumanne iliyopita kwa ajili ya kwenda kuzikwa.

  ``Huyu Mtaki alikuwa jamaa wa karibu sana wa marehemu Lema.

  Na inasemekana kuna baadhi ya mambo aliwahi kumsimulia kuhusiana na matatizo yake ya kesi hiyoÂ…huenda hicho ndicho kikawa kimemponza,`` kimedai chanzo hicho.

  Hata hivyo, Alasiri ilipojaribu kuwasiliana kwa simu na Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mark Kalunguyeye ili athibitishe habari za tukio la kuuawa huko kwa Raphael Mtaki, hakuweza kupatikana.

  Jana, Koplo Lema alifariki dunia alfajiri katika Hospitali ya Ocean Road ambako alikuwa amelazwa.

  Koplo Lema alikuwa shahaidi muhimu katika kesi iliyokuwa ikimkabili yeye na maaskari wenzie, wakiwa pia na aliyewahi kuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dare Salaam, ACP Abdallah Zombe.

  Katika kesi ya msingi, Zombe na wenzake 12 wanadaiwa kuwa Januari 14 mwaka 2006, huko Mbezi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, waliwaua wafanyabiashara wa madini Sabinus Chigumbi, Ephraimu Chigumbi, Mathias Lukombe na dereva taksi Juma Ndugu, wakidai kuwa ni majambazi.

  Aidha, Katika hatua za awali za kesi hiyo, aliyewahi kuwa shahidi wa 35, Omar Mohamed, aliwahi kuieleza Mahakama Kuu kuwa mshtakiwa wa 11 (marehemu Lema) alitoa maelezo ya ungamo yaliyoeleza kuwa alishuhudia jinsi wafanyabiashara hao watatu wa madini na dereva teksi mmoja wa Jijini walivyouawa katika Msitu wa Pande uliopo Mbezi Luis Jijini.

  Mohamed ambaye ni Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni, alitoa maelezo ya ungamo ya Lema katika Mahakama Kuu, akidai kuwa aliyapokea toka kwake wakati akiwa katika Mahakama ya Mwanzo Kinondoni.

  Kwa mujibu wa maelezo hayo ya ungamo , ni kwamba Lema (marehemu) alishuhudia watu hao wanne wakiwa wamekamatwa hai na kulazwa kwenye gari aina ya pick-up huku wakia wamefungwa pingu.

  Pia katika baadhi ya maelezo hayo ya ungamo, Lema amedaiwa kusema kuwa alishuhudia watu hao wakipelekwa katika msitu huko Mbezi Luis na kuuawa mmoja baada ya mwingine kabla yeye hajaamrishwa kuingia kwenye gari na kuipeleka miili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Aidha, Lema aliwahi kusema katika maelezo ya ungamo kuwa maelezo ya awali aliyokuwa ametoa, yakiwemo ya mbele ya Tume ya Jaji Kipenka ni ya uongo na kwamba alifanya hivyo baada ya kushinikizwa na viongozi wa juu.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...