Ndugu zetu wa Arusha: Mmeletewa Arnold Schwarzenegger kama mlivyoahidiwa na Makonda kwenye kampeni?

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Posts
1,559
Reaction score
3,953
Paul Makonda ambaye kwa sasa ni Naibu Waziri wa Michezo nchini na Mbunge wa Arusha Mjini alitoa ahadi ambayo kwa kweli ilikuwa ni ya ajabu sana.

Septemba 19, 2025 alipotembelea soko la Samunge na kuzungumza na wafanyabiashara aliahidi kuwa katika kusherehesha shamrashamra za mkesha wa mwaka mpya (2026) angemleta muigizaji maarufu duniani Arnold Schwarzenegger jijini Arusha.

Sasa mkesha ulikuwa jana kuamkia leo, ndugu zetu wa Arusha tupeni updates, Arnold Schwarzenegger ameshaonekana huko?

Pia soma: GE2025 - Makonda: Nikishinda Ubunge nitamleta Schwarzenegger mwaka mpya Arusha
 
Mmeharibu wenyewe msingeandamana labda angemleta kweli
 
Pesa za kumleta Shoziniga walizila nyama
 
Ndo kaomba Visa anodi inapitiwa na mtaalam mafwele kuona km ana chembembe za ubeberu asije kuiba uranium yetu. Sio kwa yale mateke yani nani atamuweza? Makomando wetu wapo busy kufyatua matofali ya kuvunja siku ya mapinduzi ya Unguja
 
Kuna siku Gwajima alisema jamaa ni zero brain
 
Atasema yuko busy kuipatia stars ubingwa, c Mnajua ameenda Morocco Kuongeza nguvu ya ushindi 😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…