Ndugu zangu maombeni msaada WA dawa na ushauri kuhusu huu ugonjwa wa kuku

proskaeur

JF-Expert Member
Mar 8, 2017
1,562
4,899
Habari wakuu!!!

Nina kuku wana umri wa miezi mitatu, ni kuku wa kienyeji kwa muda kama wa wiki moja iliyopita nilianza kuona dalili za kuvimba macho kwa kuku

Kufikia leo ndio wamezidi kuvimba kiasi kwamba wengine macho yameziba kabisa,

Naomba msaada wa dawa kama kuna anaefahamu na pia ni ugonjwa gai huu kwa mwenye uelewa

Pia nina vifaranga vya wiki tatu navyo vinasinzia na machoni vinatoa vitu kama machozi hivi

Picha nimeambatanisha chini
IMG_20190927_111249.jpeg
IMG_20190927_111023.jpeg
IMG_20190927_111603.jpeg
 
1.Nianze na vifaranga kusinzia na kutoa machozi hizo ni dalili za mafua....chunguza pia dalili hizi kujithibitishia uwepo wa ugonjwa wa mafua

a. Ute ute mdomoni
b.mafua puani
c.kupumua kwa shida/kukoroma
d.kupiga chafya
e.mabawa kuchafuka kwasababu ya kuku kupangusa uchafu wa machoni maana huwa unawasha.

Wape kuku wako dawa ya mafua kwa muda wa siku 5...wanywe maji ya dawa tu.

Tumia Limoxin au Tylodox kuwatibu....Ukikosa mojawapo kati ya hizo unaweza kutumia Ganadex au Enrovet.

Asante
 
Dah ufugaji wa kuku wa kienyeji unataka ujasiri sana,nilichogundua kwa uzoefu ni bora uwaache wazurure wanakuwa salama kuliko ukiwafungia kwenye banda,wanaugua sana...
 
Kuvimba kwa macho kunaweza kusababishwa na mafua.....ila kesi ya mafua katika macho ndani yanakuwa na uchafu mweupe kama sabuni iliyolowa.....

Ninachokiona kwenye hizo picha ni NDUI...

JE KUKU WAKO ULIWACHANJA NDUI?

NDUI DALILI ZAKE

NI KUVIMBA USO

KUKU ANAPATA VIDONDA SEHEMU ZA USONI

UPANGA MACHO PUA VINAATHIRIKA NA SEHEMU ZA WAZI AMBAZO HAZINA MANYOA

VIDONDA VINAKUWA NA MADOA MEUSI MITHILI YA KUUNGUA KWA MOTO

Kama hukuwachanja ndui usitoe chanjo ugonjwa ukishaingia bandani kwako au maeneo jirani subiri ugonjwa uishe.

Fanya yafuatayo

Osha vidonda kwa maji ya chumvi na uwapake Iodine au mafuta ya mboga

Wape OTC kupunguza ukali wa ugonjwa
 
Asante sana mkuu,, tylodox niliwapa wakubwa Ila wadogo niliambiwa niwape extratetracycline ila naona bado tatizo lipo mkuu
 
Kuvimba kwa macho kunaweza kusababishwa na mafua.....ila kesi ya mafua katika macho ndani yanakuwa na uchafu mweupe kama sabuni iliyolowa.....

Ninachokiona kwenye hizo picha ni NDUI...

JE KUKU WAKO ULIWACHANJA NDUI?

NDUI DALILI ZAKE

NI KUVIMBA USO

KUKU ANAPATA VIDONDA SEHEMU ZA USONI

UPANGA MACHO PUA VINAATHIRIKA NA SEHEMU ZA WAZI AMBAZO HAZINA MANYOA

VIDONDA VINAKUWA NA MADOA MEUSI MITHILI YA KUUNGUA KWA MOTO

Kama hukuwachanja ndui usitoe chanjo ugonjwa ukishaingia bandani kwako au maeneo jirani subiri ugonjwa uishe.

Fanya yafuatayo

Osha vidonda kwa maji ya chumvi na uwapake Iodine au mafuta ya mboga

Wape OTC kupunguza ukali wa ugonjwa
Asante Sana mkuu,, dalili ulizozitaja za NDUI naona zote wanazo na pia sijawahi kuwachanja chanjo ya NDUI
 
Dah ufugaji wa kuku wa kienyeji unataka ujasiri sana,nilichogundua kwa uzoefu ni bora uwaache wazurure wanakuwa salama kuliko ukiwafungia kwenye banda,wanaugua sana...
Yaani mpaka Mimi mwenyewe naanza kuhisi ni bora uwaachie, maana kuku wa majirani wanaoachiwa wenyewe wako poa tuu Ila wa kwangu ninaowaweka bandani ndio tatizo limewakumba
 
Dah ufugaji wa kuku wa kienyeji unataka ujasiri sana,nilichogundua kwa uzoefu ni bora uwaache wazurure wanakuwa salama kuliko ukiwafungia kwenye banda,wanaugua sana...
npo pamoja na wewe, hasa kama upo sehem ambayo huingilian na watu wengine n vyema wazulule japo risk n kubwa,
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom