Ndugu yangu kila siku anaingiza wanawake chumbani, nimechoka naombeni ushauri wa haraka

Mpwayungu Village

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
14,304
29,835
Poleni na misukosuko ya maisha, nina mwezi wa Sita sasa tangu nihame Buguruni saizi nipo Magomeni mapipa mtaa wa dosi

Nilikuja huku baada ya kaka yangu kuniambia tuchange pesa tuchukue chumba ambacho kwa mwezi ni 60000 pesa za kitanzania, nikasema swadakitah! Buguruni panakera ni uswahilini, madanguro ya makahaba na machimbo ya sewa na kimboka sitaki kuyaona tena, mapilau mabovu tunavyokula buguruni shell usiku mpaka tunaumwa matumbo, masupu ya mapupu na mangozi ya ng'ombe sasa hayataniona teenaa.

Tukachanga mm na kaka angu tukalipa kodi ya miezi kumi kila mtu Laki Tatu sasa tangu nianze kukaa hapa nakosa hata mda namm wakukaa chumbani, kwasababu kila akija na mademu zake tena kila siku anabadilisha, Ananiambia dogo toka nje nipige mzigo, namm huwa natii ili kuepusha fedheha kwa yule msichana.

Kumwachia chumba ili apate asali ya Tabora sio shida, shida ni kwamba akiingia na yule mwanamke saa mbili usiku anakuja kumtoa saa saba usiku huko mimi nakuwa nje tu nimelewa na usingizi, nipo kama mkiwa tena kwa makusudi hatandiki kitanda akishamakiza kufanya madhambi

Ndugu zangu nimechoka kuishi maisha haya maana nakuwa nimetoka kazini Kariakoo kazi zinachosha, nikifika geto mwili unahitaji kurelax lakini nikifika tu saa zingine unakuta mlango umefungwa kwa ndani unajiuliza kulikoni, unaona ananitumia text ikisema "dogo tulia niko na shemeji yako". Hapo ndonachoka kabisa tena siku za Wikiend ndokabisa unakuta a naenda kutafuta Malaya huko akiingia nae kwanzia mchana anamtoa usiku.

Ndugu zangu mficha maradhi kifo humuumbua, naombeni mnishauri nifanyeje maana kuongea nae naogopa namuheshimu sana ndomana hata mm kuchukua mwanamke siwezi kwakua naona sio vizuri nije nae mwenye chumba ambacho tupo wawili, sitaki tufanane tabia

----katiba mpya sio ya chadema, ni takwa la wananchi - - - - -.

Sent from my Infinix X606D using JamiiForums mobile app
 
Kazi unafanya na hela unapata na uwezo wa kupanga unao lakini umechagua kwenda kukaa na kaka yako kwakuwa umechoka kula supu ya mapupu Buguruni.

Unashindwa nini kupanga chumba chako mwenyewe?


Hata kama mimi ndio bro wako ningekupiga exile kila siku maana akili huna.
Sikai Bure, hiki chumba tumechanga kila mtu Laki Tatu tena kitanda ni changu

Sent from my Infinix X606D using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom