Ndugu yangu Humphrey Polepole, ukatae uDC ili uisimamie rasimu uliyopendekeza

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Taifa langu ni taifa la wanafiki wengi, hawana uzalendo na hawajui wasimame wapi kuutetea uishi na utashi wao.

Ndugu yangu Humphrey Polepole nakuomba ujione wa thamani na kuijenga upya haiba yako mbele ya jamii, mimi huko nyuma nilishakataa kuwa mnafiki nikamueleza mheshimiwa yule kuwa mimi siyo wa aina yake, nikatengua. Mimi ningefarijika sana kama ungejitokeza na kuukataa ukuu wa wilaya kwa kuonyesha dhahiri kuisimamia rasimu uliyopendekeza, hiyo ndiyo siasa safi na kujitambua.

Humphrey Polepole kwa kweli ukienda kuapa tena nitakufutilia mbali kwenye watu wangu wa karibu na sitokupa ushirikiano wowote ndani ya uongozi wako. Nitakuwa mpinzani wako mkubwa na kukupinga kwa kila jambo kiuchumi, kisiasa na kijamii. Nachukia sana undumilakuwili na sitaki kukuona tena kwa mara nyingine ukirudia kosa hilo la undumilakuwili.

Nausubiri kwa hamu kubwa msimamo wako ili nikuheshimu au kukupuuza kama ambavyo nimewapuuza wengine ndani ya chama chako.

Ndoto njema utakayoishi itakufanya kuwa mkuu mbele ya mataifa siku za usoni!
 
Mbowe ~~ Lowasa ni dhaifu na fisadi hawezi kuwa rais wa nchi yetu(June ,2015)

Mbowe ~~ Lowasa ni kiongozi shupavu ,tunamkaribisha UKAWA agombee urais ( August, 2015)
 
Wewe mwenyewe mbona mnafiki tu.

Hupendi undumilakuwili halafu ni mpiga debe wa mandulakuwili.
 
Uanaharakati wa Nchi hii , hautokani na kile wanaharakati kama Polepole wanachoamini, Bali wanachosukumwa kufanya au kunena ILI mkono uende kinywani.

Polepole huyu wa leo , kwa lugha ya kanisani tungesema, Amekata Shauri,
"Tazama ya kale yamepita na yamekuwa mapya"!
 
Kukataa post ya mkuu wa nchi kwa sababu za kisiasa ni kumkosea heshima, inapendeza kama utaitumikia kwanza then utafute namna ya kujiuzulu ikiwa hukukubaliana na uteuzi huo. The president is above all except the laws.
 
Aliteuliwa na Rais kuwe mjumbe wa Tume ya Katiba mpya, wakafanya kazi waliyopewa wakaiwasilisha Rasimu ya Katiba, Ameteuliwa tena na Rais kwa awamu nyingine kuwa mkuu wa wilaya sasa hapo tatizo likowapi? Rais kaona anafaa kwa kazi mpya aliompangia na si kazi aliojipangia kwa kutuma application letter!!
 
Lema 2013 "ni hekima na utukufu kwa mwenyezi Mungu kumtukana mtu fisad kama lowaxa". Lema 2015 "lowaxa ni chaguo la Mungu"
 
Mbowe ~~ Lowasa ni dhaifu na fisadi hawezi kuwa rais wa nchi yetu(June ,2015)

Mbowe ~~ Lowasa ni kiongozi shupavu ,tunamkaribisha UKAWA agombee urais ( August, 2015)
Nchi imewashinda kuongoza, mmebaki kufany maigizo tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom