Ndugu yangu Humphrey Polepole, ukatae uDC ili uisimamie rasimu uliyopendekeza

Mbowe ~~ Lowasa ni dhaifu na fisadi hawezi kuwa rais wa nchi yetu(June ,2015)

Mbowe ~~ Lowasa ni kiongozi shupavu ,tunamkaribisha UKAWA agombee urais ( August, 2015)
jamani hivi hizi statement alitoa mtu mmoja kweli. mtu wa namna hii hawezi kuwa mzalendo kamwe. ni mchumia tumbo tu
 
Taifa langu ni taifa la wanafiki wengi, hawana uzalendo na hawajui wasimame wapi kuutetea uishi na utashi wao.

Ndugu yangu Humphrey Polepole nakuomba ujione wa thamani na kuijenga upya haiba yako mbele ya jamii, mimi huko nyuma nilishakataa kuwa mnafiki nikamueleza mheshimiwa yule kuwa mimi siyo wa aina yake, nikatengua. Mimi ningefarijika sana kama ungejitokeza na kuukataa ukuu wa wilaya kwa kuonyesha dhahiri kuisimamia rasimu uliyopendekeza, hiyo ndiyo siasa safi na kujitambua.

Humphrey Polepole kwa kweli ukienda kuapa tena nitakufutilia mbali kwenye watu wangu wa karibu na sitokupa ushirikiano wowote ndani ya uongozi wako. Nitakuwa mpinzani wako mkubwa na kukupinga kwa kila jambo kiuchumi, kisiasa na kijamii. Nachukia sana undumilakuwili na sitaki kukuona tena kwa mara nyingine ukirudia kosa hilo la undumilakuwili.

Nausubiri kwa hamu kubwa msimamo wako ili nikuheshimu au kukupuuza kama ambavyo nimewapuuza wengine ndani ya chama chako.

Ndoto njema utakayoishi itakufanya kuwa mkuu mbele ya mataifa siku za usoni!
Mkuu G Sam naona huu ulio mpa ni mtihani mgumu sana kwa huyo polepole kwani kwa utamaduni wetu waafrika kukiwachia kitumbua kikutoke kwa makusudi bado sana
 
Mbowe ~~ Lowasa ni dhaifu na fisadi hawezi kuwa rais wa nchi yetu(June ,2015)

Mbowe ~~ Lowasa ni kiongozi shupavu ,tunamkaribisha UKAWA agombee urais ( August, 2015)
Wewe hata ukikesha unachangia nafasi yako ya kupewa upendeleo wa udc bado sana,kama kaka yako lizaboni kaukosa itakuwa wewe?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom