Ndugu Yangu anahitaji msaada, Kifua...

Katavi

Platinum Member
Aug 31, 2009
41,983
12,702
Dada yangu anasumbuliwa na kifua na tatizo la kupumua. Kifua kikimbana anapumua kwa shida, na anakuwa anatupatupa mikono kama vile anakata roho. Mwanzo tulidhani ni PUMU lakini hospitalini walisema hana tatizo hilo, anapewa tu dawa za kifua. Tatizo hili huwa linajirudia mara kwa mara....
Naomba msaada wa kujua ni tatizo gani na sehemu tunayoweza kupata madaktari bingwa wa hili tatizo.
 
Kama hospital wameona hana tatizo basi nakushauri umpeleke kwenye maombi. Najua watu wengi huwa wanatabia ya kudharau MAOMBI lakin ukweli ni kwamba maombi ni njia pekee ya uponyaji.
 
Kama hospital wameona hana tatizo basi nakushauri umpeleke kwenye maombi. Najua watu wengi huwa wanatabia ya kudharau MAOMBI lakin ukweli ni kwamba maombi ni njia pekee ya uponyaji.
Asante sana kwa ushauri..
 
Kabla hujaenda kwenye maombi angalia ni hospitali ipi mnayompleleka. Isijekuwa ni hivi vizahanati pesa vilivyojaa mitaani. Kama ni hivyo nakushauri kwanza mumpeleke kwenye hospitali kubwa na muweke appointment na madaktari bingwa wa fani yao. Hao ndio watakushauri pia kama uende kwenye maombi ama wanaweza kukushauri uangalia mambo ya sayansi jamii.
 
Back
Top Bottom