Ndugu/wazazi kwanini mnakuwa hivi?

Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
13,096
22,627
Unakuta ukiwa bwana mdogo kipindi bado bikra wa maisha, Wazazi na ndugu wanakuwa na shinikizo la kukukazia utafute maisha kwa ugumu.

Kama ni mzazi utamuomba pesa ya mtaji atakwambia katafute au anzia chini ukue kidogo kidogo ( sio wazazi wote wapo hivi).

Utahitaji pesa za mavazi au mahitaji yako madogo madogo ili uweze kumudu maisha ukiwa bado tegemezi lakini utakuwa unachezea upinzani mkubwa sana ukiambiwa maneno ya kufedhehesha na kukudhaliliisha kwa dharau kuwa wewe ni mzembe na mvivu na goigoi.

Ukienda kukaa kwa ndugu utapata misuko suko ya kukupa joto ya jiwe ili utoke hapo kwao na uache kuwaegemea.

Sawa haya yote ni namna sahihi ya kumkomaza kijana ili aanze kujitegemea na kusimama mwenyewe na kujijenga.

Sasa swali linakuja, mbona huyu kijana akifanikiwa kimaisha na kuanza kujitegemea bila msaada na kuwa vema, ndugu wale wale wanakuwa mstari wa mbele kuomba sapoti mbali mbali za kifedha.

Je, vijana mliofanikiwa na kupitia mazingira ya namna hii, hamuoni kuwa ni wakati muafaka wa kuwahoji hawa ndugu kuwa kwann hawajiwekei akiba ya maisha na uzee ili kuweza kupata uwezo wa kujikimu badala ya kutegemea kusaidiwa na vijana ambao wao waliwapotezea na kuwa wajibisha kipindi wakiwa wadogo na hawajui lolote kuhusu maisha.

I mean si tulikubaliana kuwa maisha ni kupambana na kujikaza kiume na kutopenda kubebwa na kusaidiwa kizembe. Sasa mbona kama mnarudia kosa lile lile ambalo tulikubaliana kuwa si sawa kufanya?

Wembe ni ule ule ila upande wa kukata sasa ni tofauti.

Naandika uzi huu baada ya kumpa makavu ndugu yangu ambaye alikuwa akimpa kauli dogo mtoto wa ndugu yake na malkia(mama).

Akimind dogo kuwa katoka mkoa baada ya kumaliza form six halafu anang'aa macho tu hajishughulishi. Me nikamuhoji kuwa wewe umempatia msaada gani alipokwama zaidi ya kusema maneno ya kumuumiza ukiamini unampa nguvu ya kutoka akapambane?!

Why usitumie lugha kurupushi ila ambayo ni rafiki?! Badala ya kumlaumu why usimuongoze na kumuonyesha vya kufanya halafu umfunze kujisimimia. Huyu akitoka kesho na kesho kutwa atakukumbuka kama mentor wake na kiongozi kama utakwenda nae kwa upendo na urafiki.

Ukimlaumu na kumfedhehesha atakukumbuka kama mnyanyasaji na mfedheheshaji wake.
 
Mimi wajomba zangu wengi wakiniomba huwapa makavu, huwauliza tokea udogoni kwangu waliwahi kunisaidia nini hata leo niwasaidie wao?.


Lunatic
 
Mi nakwambia mo kama angezaliw buguruni yule angekuw mweusi tiii pamoja na uhindi koko wake. Familia zet hiz zinazalosha chuki sana ukitoboa watkutegemea ila sasa!!! Kuna ndug zako wew mwenyew wnaomba usitoboe

Mimi kuna kaka angu mmoja mwanajeshi aliwahi kunipa darasa.. Akanmbia dogo ukitoboa usimpe mtu hata mia nkaona ndo mana kumbe hanisapoti
 
IPOJE
IPO HIVI
HIVYOJE ??

hawapendi ufanikiwe na ukifanikiwa wanataka uwasaidie .

NARUDIA TENAHawapendi ufanikiwe na ukifanikiwa wanataka uwasaidie.

UKIPEWA USISAHAU NA UKITOA TOA BILA KUKUMBUKA.

NARUDIA TENAukipewa usisahau na ukitoa toa bila kukumbuka.
 
Juu umetoa jibu la maswali uliyouliza chini.

Complacency ni kitu kibaya sana. Yani hao wazazi na ndugu walikuwa wanakukumbusha usijisahau ukaona kula kulala ndio maisha.

Kutokana na akili zako kuwa hazija pevuka ukaona kama unanyanyaswa lakini hiyo ilikuwa ni kama alarm call kwako ukaamka ukapambana ukatoka kimaisha.

Sasa nadhani ni vyema ungewashukuru hao waliokuamsha ndotoni ukaanza kupambania maisha yako na ukafanikiwa. Usiwalaumu kwakuwa wangekulelea kimayai kula kulala bure usingekuwa hapo ulipo sasa.

Ila sometimes kuna ile hauna mwanga kabisa unaambiwa tu pambana nayo huwa inaumiza lakini unajilipua tu unapambana na unatoka. So mda mwingine tunapitia changamoto na majaribu kama hayo ili ukifungwa mlango fulani ufunguke mwingine wenye neema zaidi.

Kikubwa ni kutokukata tamaa.
 
Back
Top Bottom