Ndugu wanashinikiza amrudie......

Ndugu wanashinikiza amrudie......

Uda

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2010
Posts
811
Reaction score
623
Ushauri wenu utasaidia sana kutatua tatizo hili ikiwa ni kisa cha kweli.

Kaka huyu alikutana na binti huyu miaka kama 7 iliyopita wakaanza kujivinjari na hatimaye kupata watoto wawili.kwa kipindi chote hiki hakukuwa na ndoa rasmi bali binti huyu alihamia kwa kaka huyu na familia ya kaka huyu ilimchukulia kama mke,wifi au shemeji.

Maisha yalisonga ingawa yalikuja kubadilika kwani jamaa alizidiwa na vijiwe vya kwenye bar akawa mlevi chakari na mara nyingine kutoa kichapo kwa my wife wake na hatimaye binti akaamua kusepa au kusepeshwa!

Cha kushangaza haikupita miaka miwili binti huyu akaibukia kwa dume jingine nalo bila masikhara likamuachia mbegu na kwa sasa mtoto ana kama miezi 10 hivi hakuna matunzo.

Kama kawaida binti anaendeleaga kwenda kwa kaka lengo likiwa ni kuwaona watoto wake wa kwanza na pia kuwapa hai mawifi na wakwe halafu kwa mbaali anaonesha nia ya kutaka kurudi kwa kaka huyu!

Sasa hebu mpeni ushauri kaka huyu je amrudie binti huyu?maanake ndugu wanamshawishi eti binti huyu asingepata mtoto wa nje kama yeye asingekuwa mlevi!

Kwa sasa kaka kaokoka na hagusi kilevi ila ndio hivyo tena mawazo juu ya mawazo amrudie binti au vipi?
 
Asimrudie.Kama jamaaa wa kwanza alikua mlevi wa pombe,haina maana mwanamke kuamua kuwa mlevi wa dushe mpaka kuzalishwa.
 
Akirudi, huyo baba kichanga nae atakuwa anakuja kumuona mwanae
mmmh hapo ni kama futari sasa viazi, mihogo, maharage, nazi na karanga humo humo
 
kwanza kumbuka hawa ni wazazi tayari. hivyo mwanamme kama ataamua kuoa mwanamke mwingine bado atapata taabu sana hasa kuwakubali hawa watoto wawili. nadhani wanaweza kuendela kuishi pamoja kama kawa, mtoto siyo ishu sana maana huwezi jua katika maisha atakuja kuwa nani mbele ya safari. kuna mifano mingi ya watoto waliolelewa na baba wa kufikia wakaja kuwa na mafanikio makubwa mfano ni raisi wa marekani Bill Clinton.
 
Amrudie walee watoto,madhila ya ulevi uliokithiri na vipigo enzi hizo havikumbuki??
Aliyasababisha mwenyewe,
mwanamke katulia umezaa nae watoto 2 leo unajiuliza umrudie au la? Wakati tabia zako ndo zilimkimbiza?..
 
Amrudie kwa kigezo cha watoto.. wangekuwa hawana watoto ningesema hakuna kurudiana.....
 
Back
Top Bottom