Ndugu wa mgonjwa ampiga Daktari Mtwara,Madaktari waanzisha mgomo

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
Katika hali isiyotarajiwa, ndugu wa mgonjwa aliyepata ajali ya pikipiki wamempiga Daktari wa Hospitali ya Rufaa ya Ligula Mkoani Mtwara, aliyekuwa anamhudumia mgojwa wao.

Daktari huyo aliyekumbwa na mkasa huo ambaye hakutaka jina lake litajwe na vyombo vya habari alieleza kuwa alipokea kipigo kutoka kwa ndugu wa mgonjwa huyo baada ya kumuandia rufaa kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbini (MNH).

Alisema kuwa alichukua uamuzi huo baada ya vipimo kuonesha kuwa mgonjwa alikuwa amevunjika mfupa wa mguuni mara kadhaa na kwamba hospitali hiyo haina uwezo wa kumpa matibabu husika kulingana na madhara aliyoyapata katika ajali iliyotokea Jumamosi iliyopita, lakini alishangazwa na uamuzi wa ndugu hao kuonesha kupinga uamuzi huo kabla ya kuanza kumpiga.

Kutokana na hali hiyo, madaktari wa hospitali hiyo walianza mgomo na kukaa makundi madogomadodog wakiacha kutoa huduma kwa madai kuwa wanahofia maisha yao. Madaktari hao walilaani kitendo alichofanyiwa mwenzao.

Baadhi ya wagonjwa walilamika kutopata matibabu tangu walipowasili hospitalini hapo majira ya mchana hadi jioni huku wakiwasihi madaktari kuwaokoa wagonjwa ambao wanaweza kupoteza maisha yao kutakana na mgomo huo.

Hata hivyo, mwandishi wa gazeti la The Citizen alipata nafasi ya kuzungumza Mkuu wa Hospitali ya Ligula ya mkoa wa Mtwara, Dk. Shaibu Maarifa ambaye alieleza kuwa hakuwa na taarifa za kuwepo kwa mgomo hospitalini hapo kwa kuwa alikuwa nje ya ofisi.

Hivi karibuni, madaktari nchini walianza kulalama wakidai kunyanyaswa na wagonjwa katika hospitali za umma. Madaktari wa Hospitali ya Wilaya ya Butimba (Nyamagana) mkoani Mwanza pia waligoma hivi karibuni kwa saa kadhaa wakidai kunyanyaswa na wagonjwa, hali iliyopelekea aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mlongo kuingilia kati.

Chanzo: DAR24
 
Wananchi wamekuwa na hasira sana kutokana na wauguzi wetu kijisahau kutimiza wajibu wao
 
Tunapoelekea sisi wananchi sipo kabisa,hii sera ya uzembe na uwajibikaji isitufanye kuingilia utaalamu wa watu.Kuna wakati inabidi kukubali maoni ya wataalamu (watoa tiba)..

Na pia kumbukeni tunafanya kazi katika mazingira duni sana inawezekana labda huyo mgonjwa angeweza kutibiwa hapo kama vifaa vingekuwepo.
 
Sasa unapompiga daktari ili kushinikiza mgonjwa wako asipelekwe hospitali kubwa zaidi unamtakia mema mgonjwa wako kweli?, kwa mfano akibaki hapohapo wakamchoma sindano ya ukimwi utajua?, jamani madaktari nao ni binadamu na wanamachungu vilevile kama mtu yeyote yule
 
Mgonjwa/nduga wa mgonjwa kumpiga daktari sio sawa, na vile vile daktari kugoma kutoa huduma kwa wagonjwa wengine kwasababu ya matatizo ya mgonjwa mwingine sio sawa.
 
Habari haijabalance ni ngumu kujudge, madaktari wamejisahau sana ni vizuri kusikia upande wa mgonjwa, kumbuka mgonjwa amevunjika mguu kwenye bodaboda mara kadhaa hapo kumpeleka Muhimbili lazima uwe na nauli ya watu wawili/watatu kwenda Dar kwa ndege sio gari tena, hapo labda doc kamcheki na hajampa huduma za awali kabla ya kufikiria Muhimbili.
Kumbukeni Mwanza mwanamke alijifungulia chooni mapacha wakafariki baada ya wahudumu kukataa kumsaidia tena muuguzi mmoja alimfuata chooni akamchungulia then akaondoka zake bila msaada.
 
Habari inayoelezea upande mmoja sio habari ni upuuzi mkubwa.

Ilikuweka uwiano mzuri inatupasa kupata maelezo ya ndugu wa mgonjwa.

Kupiga dakitari nimaamuzi magum sana lazima kunasababu za hao ndugu kumtwanga mganga. Sometime madakitari wanaudhi sana.

Nitatoa mfano wangu.
2014 nilimpeleka wife kucheki afya hospitali flan. Hakuwa mgonjwa kwakweli, aliingia kwa dakitari akatoka amenuna kinyama nikamuuliza vipi....eti kaniandikia two days nilazwe .... nikamuuliza kwa vipimo gani? Wife kanambia ndo naenda maabala hii hapa fom... tulipopimwa maabala hapakuwa nalolote nilisoma vizuri yale maelezo kujithibitishia ukweli nikamuuliza jamaa wa maabala akasema hakuna kitu bro.

Nikapowa wife aliporudi kwa dokita na majibu ya maabala bado aliambiwa alazwe two days kutazamia hali yake.

Ndipo wife alipotoka akigomba sitaki unilete tena kwa huyu mshenzi, akanisimulia kilichoendelea....niliingia ndani kwa hasira usipime.

nikamuuliza unamlaza kwa vipomogani? hakuwa najibu lolote zaidi ya kujiumauma kidogo nimtwange aisee

Tuliondoka na wife yupo fiti mpaka leo, hawa jamaa siwaamini baadhi yao nimatatizo makubwa.
 
mmmh! jamani hii sekta ya afya inabidi iangaliwe kwa jicho la tatu. Mimi ilinitokea mwaka flan nilipotaka kupoteza maisha kwa uzazi. Nesi Daktari na nesi walinihudumia vibaya sana. matokeo yake baada ya siku mbili nilivimba na kubadilika rangi mwili ukawa mweusi tii. Nilinusurika kwa kweli. Ila pamoja na uzembe nilijifunza jambo.
tulikuwa wagonjwa 27 wodini halafu manesi wapo wawili tu. Daktari aliyetakiwa kutoka saa moja usiku alitoka saa tatu. na Labour ward huwa iko busy balaa. wahudumu wangemudu vipi? Ni kweli wanachoka sana na bado ratio ya nesi au daktari kwa wagonjwa haizingatiwi. Serikali ifanye jambo kunusuru maisha ya watanzania.
 
mmmh! jamani hii sekta ya afya inabidi iangaliwe kwa jicho la tatu. Mimi ilinitokea mwaka flan nilipotaka kupoteza maisha kwa uzazi. Nesi Daktari na nesi walinihudumia vibaya sana. matokeo yake baada ya siku mbili nilivimba na kubadilika rangi mwili ukawa mweusi tii. Nilinusurika kwa kweli. Ila pamoja na uzembe nilijifunza jambo.
tulikuwa wagonjwa 27 wodini halafu manesi wapo wawili tu. Daktari aliyetakiwa kutoka saa moja usiku alitoka saa tatu. na Labour ward huwa iko busy balaa. wahudumu wangemudu vipi? Ni kweli wanachoka sana na bado ratio ya nesi au daktari kwa wagonjwa haizingatiwi. Serikali ifanye jambo kunusuru maisha ya watanzania.
umekuwa na considerate mind!safi sana,pamoja na almanusra iliyokukuta lakini pia umeweza kubaini na linaloweza kuwa lilikuwa tatizo,am giving five to u mamafive
 
Utabibu unahitaji maadili ya pekee, na ikiwezekana tabibu awe na asili ya kumcha Mungu katika Roho na Kweli, aipende kazi yake asiwe mtu wa kutahayari na mwenye kuelewa wajibu wake na kuheshimu maamuzi ya matibabu atoayo, ikimpasa zaidi awe mwenye Roho ya uvumilivu. Kufanya kazi kwa mazoea sababu ya taaluma ni makosa, na kama binadamu awaye yote angekuwa na hofu ya Mungu ndani yake basi utabibu ingekuwa huduma pekee duniani. Poleni madaktari, jamii inawategemea sana, lakini pale mnapokutwa na mazito nje ya uwezo wako alika daktari mwingine akusaidie.........
 
Back
Top Bottom