Ndugu kinana anajidanganya


Wimbo

Wimbo

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2012
Messages
417
Points
225
Wimbo

Wimbo

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2012
417 225
Ziaraza katibu Mkuu Kinana na wenzie zitatupa majibu mengi sana ya hatima ya Tanzania,katika ziara yake alipofika Sumbawanga tarehe 22 November alitoa matamko mazitomawili, wana CCM kuondokana na uheshimiwa na kuitana Ndugu, hilo halina ugonvi na limeshaanza kutumika mara baadda ya tamko lake. La pili alisema mafisadi na vigogo wa rushwa si wengi ni asilimia 0.001 ya wanaCCM na akaahidi kwambasamaki mmoja akioza hawaozi wote huyo aliyeoza atatolewa atupwe tenga libakisalama. Hapa ndipo ninaposema anajidanganya tena saaaaaana.Kwamahesabu ya CCM ambayo naamini ni sahihi 0.001 ya wanaCCM millioni tano nisawa na kusema mafisadi na wala rushwa wakubwa ni 5000 hawa si wachache. Kamailivyokuwa msingi wa World trade center ambayo msingi wake ulikuwa unajengwakutoka juu kwenda chini washambuliaji wa September 11 hawakupata taabu walijuasiri ya jumba hivyo walipokata msingi wa jumba lote lianguka. CCM iko hivyo hao 5000 ndiowameshikilia nguzo za CCM, hivyo lazima kuwe na tahadhari ya kuwatoa pamoja nauozo wao na kuwatupa, isije ikawa kama majuto ya Mwenyezi Mungu alipomtosashetani akamtupa duniani akasema ‘ole dunia" na hapa ndipo nami nisubutu kusema oleCCM.Hawa0.001 ndio waliotufikisha hapa tulipo, ndio wanahusika mikataba mibovu yamadini na gesi tunayopigia kelele, ndio walioua miundombinu ya reli ili freightzao za maelfu ya maloli yabebe cago kupeleka Nchi jirani, hawa ndio wameuakampuni yetu ya ndege ili makampuni yao yafanye biashara, hawa ndio wana hisa katika makampuni ya mabasi yanayo zunguka Nchi nzima, hawa ndio wameua shirika letu la umeme tanesco, ili wale pesa kupitia richmond, hawa ndio waliua kiwila ili ifirisike wainunue pesa ya nyanya, hawa ndio wameua shirika letu la Posta na simu ili hisa zao katika mitandao ya mawasiliano izae faida, hawa ndio wameua kilimo chaTanzania kulazimisha mbolea mbovu ya minjingu ambayo wana hisa na mwekezaji ili wapate faida, hawa ndio wameshikilia bandari na madhaifu yake yote, hawa ndiowanauza nyara za serikari na wanyama hai, ndio watoto wao na jamaa zao wameshikilia nyazifa mbalimbali katika chama chako na serikali, hawa ndio wenye mitandao ya madawa ya kurevya, na biashara za pesa chafu, hawa ndio waliojilimbikizia fedha kwenye mabenki ya ya Nje, hawa ndio wanaopanga safu za uongozi na kugharamia chaguzi hizo, lakini hayo yote tisa, kumi, hawa ndio wamepenyeza watoto wao kuingia kwenye NEC chombo cha maamuzi kwa zaidi ya asilimia 60%. We Kinana una jeuri gani ya kuwatoa na kuwatupa. Jaribu uone.
Nakutabiliakwamba kama kweli umeshafanya toba ya uliyoyafanya huko nyuma yanayofanana nawao na unataka kuwa sadaka ya ufufuo wa CCM na unatamani thawabu ya MwenyeziMungu katika maisha yajayo, ama utashidwa vibaya au utajiuzuru kabla ya miezisita uliyowapa mafisadi. Nimeweka sala maalum kwa ajiri yako ili kauli yako iwekwa vitendo Mungu akulinde na mafisadi hao na ufaulu kuifufua CCM ambayo harufuya uvundo wake inawatisha hata wabeba jeneza lake si ulisikia Sumbawanga hatamwenyekiti wa kitongoji anadai rushwa ya wino ili amwandikie barua yautambulisho mwanachi mwenye uhitaji;- hapo vipi?. Kidumu chama cha mapinduzi.
 
Ryaro wa Ryaro

Ryaro wa Ryaro

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2010
Messages
2,661
Points
1,225
Ryaro wa Ryaro

Ryaro wa Ryaro

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2010
2,661 1,225
Ni vema umempa caution ili aweze kujitadhimini kuhusu "gunia la misumali yenye ncha kari alilobeba kichwani". Surely the guy will fail miserably tumsubirie Chini kwani mifupa iliyowashida watangulizi wake anadhani na kujifariji kuwa ataitafuna...... pwaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa kabla ya miezi hiyo sita.
 
Tukundane

Tukundane

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2012
Messages
9,700
Points
2,000
Age
53
Tukundane

Tukundane

JF-Expert Member
Joined Apr 17, 2012
9,700 2,000
Apige ndenge2 kwa pamoja kwa kumng'owa lowassa atakuwa amefanikiwa kumng'owa na mwenyekiti wake.
 
K

Kirokolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2008
Messages
255
Points
250
K

Kirokolo

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2008
255 250
Asilimia 0.001 ya 5,000,000 ni 50 na siyo 5,000. Weka hesabu sawa, leta mada.
 
J

JAPHETtumpa

Senior Member
Joined
Feb 25, 2012
Messages
136
Points
195
J

JAPHETtumpa

Senior Member
Joined Feb 25, 2012
136 195
kinana haelewi uzito wa tatizo la chama chake nadhani hotuba za mnwenyekiti wake kwe mkutano wao zilimsisimua sana kiasi cha kutokuuona ukweli, nasikia aliambiwa tatizo la ccm ni baadhi ya vyombo vya habari na vyama vya siasa hasa cdm.
ushauri kwake hapaswi kumuamini kiasi hicho mwqenyeiti wake kwa sababu kuna tetesi aliingia ikulu kwa kusaidiwa na fedha za epa
 

Forum statistics

Threads 1,285,942
Members 494,834
Posts 30,879,945
Top