Ndugu January Makamba - New website

MKuu nakuunga mkono, kwa kweli ameandika kama mtoto wa miaka 10 essay.... sorry! (shrug ya Simon Cowell) :wink2:
ON a very serious note... dogo hayuko serious kabisa! Anaandika kwa lugha ya kitoto na anajiona anajua anachokifanya ... hizi technique zenyewe ni za kizamani na za kitoto... not impressed!
 


Nadhani hatumtendei haki Kijana Makamba. Lugha kuu ya mawasiliano kati ya Compyuta na Binadamu ni Kiingereza. Huwezi ukakuta window at log on ikakuelekeza kwa kiswahili kuingia ndani na kufanya mavitu yako. tusichanganye mawasiliano yetu na lugha ya computer kama kitendea kazi. Nadhani January alifikiri yote hayo. Alijua Mwananchi atakayekuwa na uwezo wa kutumia Computer atakuwa lugha ya malikia inapanda. Kwa wale isiyopanda wanapata vionjo vyake live kwenye majukwaa n.k. Lakini naamini kipo kitu anaandaa kwa ajili ya level yao. tatizo liko wapi. Jiulize mara kumi hoja uitoayo ina mizani? haina chuki wala husda. haina ushabiki? then toa maoni yako
. Great thinkers they think. Lakini humu janvini sometimes kuna ushabiki badala ya hoja.
 

Jamani, hata ukimchukia sungura wakati mwingine inabidi ukubali kwamba anaweza kukimbia!!! Na mimi pia nimeipitia website yake na sidhani kama mnamtendea haki mnapomponda hivo. Website imetulia, ukiacha typos kidogo sana. Na amesema it is still work in progress na kwamba version ya kiswahili iko mbioni. I am not his fan na wala si mwana CCM lakini inatubidi vijana tufike mahali tutambue kujituma kwa wenzetu hata kama tumepishana kiitikadi. Kijana amejitahidi, tumpongeze na inapobidi tumuunge mkono. Maana ya upinzani siyo kupinga tu hata mazuri.
 


 
Hebu nisaidie mkuu... sasa hii inawafaidisha vipi wananchi wake wa Bumbuli kama si kuji-promote ye binafsi? Kama angekuwa celebrity kama actor/ model/ basketball player ningeelewa maana ndo kazi yake inamtaka awe anaji-market .. kama mbunge kazi yake si kuuza sura bali kuwasaidia wananchi wake ambao hata umeme hawana. Ni upuuzi kumpongeza kwa poor attempt at self promotion that does not benefit his constituency. FACT!
 
If you think the role of a website is limited to only "celebrity kama actor/ model/ basketball player" then You are an id!0t. FACT.

Kaka Objective ya hiyo site ni nini? Targeted readers ? I'm confused.
 
If you think the role of a website is limited to only "celebrity kama actor/ model/ basketball player" then You are an id!0t. FACT.

Asante mkuu kwa matusi....
Let's get a few things straight: sijasema kokote kuwa website is limited to celebrity only. Hebu soma vizuri nilichoandika. I was talking about self promotion. Hebu nijibu, kuandika kwa lugha ya kitoto maisha yake inasaidaje wananchi wa Bumbuli?
Jibu hoja kwa hoja na si kwa matusi.
 

Kumradhi kama umeona umetusiwa. Angalia tena website vizuri, kuna section zinazoongelea Bumbuli as a place, her people, and issues (Economy, Education, Agriculture, etc). There is also a link to the book about Bumbuli development plans. U need partners in development who will be willing to invest in your constituency. These people need a platform and that is where a website become a very good place to start. Also there is Bumbuli Development Corporation... Coming Soon! in progress as well. You can check it out.

You are allowed to hate, it is okay. we all need haters in our life, but just be explicit about your hating endeavor, sio kuja na visababu vya kichovu. Au sio baana.
 

Sasa ni kitu gani kilikuzuia kuleta hoja at the first place? Matusi hayafai mkuu!
Section kuhusu Bumbuli is well and good pamoja na kuwa ni copy and paste tu nothing creative, ila sijaona bado hiyo Development Cooperation itafanyaje kazi - it is again the rich and educated going to take advantage of the poor?

Ila mi naomba nirudi kwenye mada yangu ya kwanza ambapo nasema hii website is not about Bumbuli but about January Makamba. Je unakubali hilo? Sababu:
1. Iko kwa jina lake na siyo bumbuli.org au kitu kama hicho
2. Opening page ni kuhusu yeye, picha zake, wasifu wake ( the leader.. the father.. etc)
3. Mission ya website imeandikwa nia yake ya kuwa mbunge. Hebu cheki alafu lugha iliyotumika, "
Jamani kama angekuwa smart na alikuwa mwandishi wa rais hawezi kuandika kwa lugha nyepesi hivi nia na malengo yake ya kuwa mbunge.

So hii website haihusu Bumbuli, inachosema ni kuwa ye kama mbunge anatafuta watu waje wawekeze KUPITIA YEYE.. ye ndo atakuwa coordinator na ndo atapokea pesa zote kwa niaba ya wananchi au siyo? Kwa hiyo ni lazima ajionyeshe kuwa ndo tumaini pekee la BUmbuli na all investors waonane nae, si mwingine.. Its all about him na kujinufaisha narudia tena.

Sasa unasema mi ni hater lakini tunatoa mawazo yetu. Kama mheshimiwa hakutaka kupata mawazo basi kulikuwa hakuna haja ya kui-promote website hapa, kwani hatuko hapa kusifia tu.
BTW huyu dogo tuna data zake tukianza kuzianika utaweza kuona vizuri kwa nini tumemsoma siku nyingi nia na malengo yake .. na believe me he does not have the interest of Bumbuli at his heart. I rest my case.
 

Tukubaliane kutokubaliana.
 

Hapana sijui leo kuna nini .. mbona warembo wote wa JF mko hivyo??:rain:
 
jamaa amejitahidi na kama livyosema bado ipo marekebishoni........ataweka na kiswahili pia, shake of the haters............
kizungu sawa hakina mtiririko mzuri na hakivutii kusoma kinaboa kidogo maana, 'I' ni nyingi mno hana mtirirko mzuri wa kusimulia lakini alichoeleza hivyo hivyo tumuelewa. msisahau background yake ya elimu ya msingi jamani.....it affects the ability ya yeye kuongea english ya dictionary mnayoitaka nyie.
website ya Mo imeenda shule ...........nimeipenda kweli www.mohammeddewji.com
 

sasa cha kushangilia kipi? mtu kuandika historia yake?
 
okay hapa tatizo ni nini haswa mbona nashindwa kuelewa ni JM kuanzisha website au JM kuandika hii website kwa kingereza?....
 
okay hapa tatizo ni nini haswa mbona nashindwa kuelewa ni JM kuanzisha website au JM kuandika hii website kwa kingereza?....
Tatizo hapa ni ubunge wa kununua na baada ya hapo kutaka kuufanya umaskini wa wana-Bumbuli kuwa mtaji wa kujikweza kisiasa na kijamii. Tujadili kuanzia hapo tafadhali.
 
Tatizo hapa ni ubunge wa kununua na baada ya hapo kutaka kuufanya umaskini wa wana-Bumbuli kuwa mtaji wa kujikweza kisiasa na kijamii. Tujadili kuanzia hapo tafadhali.


Abdulhalim,

Mimi sina tatizo na January Makamba. Nina matatizo ya wanasiasa vijana katika vyama vyote vya siasa ambao hawana experience ya kazi. Na ambao hawana track record ya mafanikio. Tusipoangalia itafikia miaka mia moja ya uhuru na nchi itakuwa inaendeshwa na watu wasio na mafanikio yoyote.
 

Kaka wa 'Mtoni'

Hapa tunajadili kuhusu performance na track record zipi? maana siasa za Tz ni makundi sio mtu mmojammoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…