Ndugai naye aambulia matusi kwenye simu

Ndugai naye aambulia matusi kwenye simu

Sumasuma

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2011
Posts
342
Reaction score
110
Naibu spika wa Bunge, Job Ndugai, amesema kuwa hatua ya viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutoa simu yake kwa wananchi kumemuathiri kwa kuwa amekuwa akitukanwa.

Ndugai amesema kuwa watu kadhaa wamemtumia ujumbe mfupi (SMS) ama kumpigia simu za mkononi na kumtukana baada ya CHADEMA kuwapa simu zake Jumapili iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jana nje ya viwanja vya Bunge jana, Ndugai alisema amekuwa akitukanwa na baadhi ya watu baada ya chama hicho kuzitamka hadharani.

"Nimejibu simu za mkononi nilizokuwa nikipigiwa na kutukanwa na hata ujumbe mfupi nao nimejibu wakinitukana. Mimi ninajibu kistaarabu kwa kuwa mimi ni kiongozi, siwezi kutoa maneno machafu," alisema.

Hata hivyo, Ndugai alisema kuwa ugawaji wa namba za simu za mkononi huo unaingilia uhuru wa mtu binafsi. Alisema suala hilo litafanya baadhi ya watu kuathirika kwa kuwa wakati mwingine imemlazimisha kuacha kupokea simu kwa kuwa anadhani ni wale wale ambao wanataka kumtukana.

Jumapili iliyopita, CHADEMA kilifanya maandamano jijini Dar es Salaam ya kuwapokea wabunge wake kutoka mjini hapa kuhudhuria mkutano wa Kumi wa Bunge na kuhitimisha kwa kufanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Temeke mwisho.

Katika mkutano huo, viongozi wa chama hicho waliwapatia wananchi waliohudhuria namba za simu za mkononi za Spika wa Bunge, Anne Makinda, na Ndugai, ili kuwashinikiza wang'oke wenyewe kwa madai ya kushindwa kuliongoza Bunge kwa kupendelea Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuukandamiza Upinzani.

Hoja yao kubwa ni kiti cha Spika kukalia rufani takribani 10 bila kuzitolea maamuzi na kutupa hoja binafsi za wabunge wa Upinzani.

Tayari Spika Makinda amepokea simu 200 na sms 400 ambazo zilikuwa zikimtukana.


CHANZO: NIPASHE
 
*******..atoe namba yake kwenye tovuti ya bunge..anadhani watanzania wa leo ndio wa enzi zake,..mbona mi nilishawahi kumchana kabla wakina zitto hawajataja namba yake
namba zao zimewekwa pale for public purpose waache kulialia kutaka huruma sababu hakuna wa kuwaonea huruma kwa upuuzi wanaoufanya bungeni!!!
 
Huyu alikuwa anawajibu so hakuna kesi......mbona hatuoni hizo sms zenyewe?
 
Mwenye namba za Kinana tafadhali.....
 
Wakati tulionao mtamu kwelikweli,wamejisifia oohh shule za kata tumejenga nyingi,sasa wanashangaa nani kawazibua macho watanzania au walifikiri ili mtu awe na upeo wa kutambua madudu yao ni lazima ufike chuo kikuu!waende na wakati waache blaablaa.
 
kila siku nilisema watanzania hawajakosa elimu tatizo lilikuwa kutumia hekima zao vizuri sasa wameona na wanaamka.pambazuko limejongea viva wamachinga kwa kuanzisha vugu vugu.
 
sasa pamoja na sms zote hizo Ngugai unangoja nini kujihuzuru? ndio ujue wananchi wamechoshwa na ubabe wenu wa kutumia kiti vibaya.. mjihuzuru tu na boss wako
 
Alijuaje kama ametukanwa?it seems na yeye ni mtumiaji mkubwa wa hayo aliyotumiwa mpaka aka declare ametukanwa!!
 
hana aibu kabisa huyu ndugai, yani umetumiwa sms zote hizo bado tu umeng'ang'ania? safari hii tutakufuateni huko huko dodoma. jamani hivi dodoma anapatikana maeneo gani huyu pimbi?
 
Anashangaa zakwake kugawiwa!!hata za rais nilazima raia tuwe nazo kwani hao ni vibarua wetu hawako hapo kwa ajiri ya familia zao,nakama hawataki tupate namba zao wakazibandue hapo bungeni au waondoke wawaachie wanao weza kuongoza nchi.wanadhani kua watakufa na kuzikwa na bunge! Hawa kweli vipofu,na wakibadili namba waende wakazibandike mjengoni ili raia wazipate shem on mbavu sana
 
Mimi nataka ya Lukuvi na mwanasheria mkuu !
 
Kwani hizo namba si zinapatikana kwenye website ya BUNGE??
Kwa nini walalame???
 
kiongozi makini haogopi kutukanwa. ndio challenge ya uongozi.kaza buti rekebisha kasoro zako
we ni kidume acha kulalamika. lazima ujue makosa yako,jenga heshima kwa kuwa mfano,jitofautishe na madam spika
wape wananchi imani kuwa hujawekwa kwenye hicho kiti kulinda mafisadi.kazi kwako
 
Mimi naomba za Werema,Lukuvi, Mtoto wa Mkulima(asiye mkulima)...maana nao wanalinda upuuzi ili niwape ushauri wa bure


Kweli tunaomba mwenye namba za hawa jamaa hasaaaaaaaa LUKUVIIIIIII....tafadhali mwenye namba zake atumwagie hapa.
 
Hapa ndiyo unawajua Pro-CHADEMA JF ni watupu.
 
viongo-zi kutoa namba zao za simu kwa public ni ishara njema ya uwazi na uwajibikaji! sasa Spuka Makinda na Ndungai waache kulia lia eti wanatukanwa! wakitaka wapokee simu za pongezi watende haki kwa wabunge wote kwa heshima ya watanzania! hiyo ndio dawa ya kutokutukanwa!
 
Back
Top Bottom