Ndugai amtaka Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA) aliyewasha kipaza sauti bila kuruhusiwa akidai kudhalilishwa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM), atoke nje

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mbunge wa Viti Maalum (CHADEMA), Yosepher Komba amelalamika kudhalilishwa wakati Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Jackline Msongozi akitoa ushauri kuwa Msajili wa Vyama aingilie kati CHADEMA kutokana na tuhuma zinazotolewa juu ya chama hicho ikiwemo za Wabunge kukatwa fedha na baadhi ya Wabunge Wanawake kulalamika kudhalilisha Kingono

Wakati Msongozi anaongea, Komba aliomba kutoa taarifa na alipopewa nafasi alisema “Anachokifanya Mbunge Jackline ni kuzidi kuwadhalilisha Wanawake na nimuombe awashauri hao wanaolalamika waende kwenye Vyombo vya Dola”

Spika Ndugai alipokea na kusema “Ndicho anachokifanya. Hivyo kaa chini tuweze kumsikiliza.” Na kisha kumuambia Mbunge Jackline achukue ushauri huo aliopewa

Hata hivyo, Mbunge Jackline alijibu na kusema “Huyu anayeongea (Yosepher) pia aliwahi kunifuata, kama dada yake maana naye anatoka Ruvuma na akaniambia naye ana tatizo hilo hilo. Hivyo Spika, naomba nikuambie katika hilo wenzetu wamekuwa wakiteseka sana”

Wakati Mbunge Jackline akiendelea kutoa hoja yake Mbunge Yosepher aliwasha kipaza sauti na kuanza kuomba utaratibu huku akisema hayupo tayari kudhalilishwa. Spika Ndugai alimtaka kukaa chini na kumuambia asiongee kwani hajaruhusiwa kusema na anafanya fujo

Baada ya kuambiwa hivyo, Yosepha aliwasha kipaza sauti na kusema atashughulika na Mbunge Jackline nje ya Bunge. Spika Ndugai alisema "Umewasha kipaza sauti na kila ukielekezwa husikii, naomba kwa usalama na amani utupishe."

Aidha,Mbunge Jackline alimalizia kusema chama kama hivyo (CHADEMA) vinabidi vifute kwani mbaya zaidi Mwenyekiti wa CHADEMA amefanya vitu vya hovyo kabisa. Amesema "Ameenda kustarehe halafu anasema amepigwa na watu gani? Sisi tunaishi pale Medeli tumemsikia kabisa akienda kwa nyumba ndogo yake"
 
Huyo spika na baadhi ya wabunge wa CCM ni watu wa ovyo kabisa.Waache kuzungumzia chadema, bali wazungumzie mambo ya kitaifa.
 
Madaraka hulevya kwa kitambo kifupi sana, lkn historia na uovu humwandama mtu popote pale alipo baadaye ama ktk ulimwengu wa mwili au roho.
 
Nimeangalia clips za baadhi ya matukio ya Bungeni Leo na jinsi Ndugai anavyo liendesha bunge kwa uonevu wa aibu namna ile na kuona hakuna haja tena ya kuwarudisha wabunge wajinga hawa was CCM tena Bungeni.
Bunge in chombo chetu tunacho kiendesha kwa gharama kubwa sana, iweje mambo ya uongo, utoto, na ujinga yafanywe na spika was CCM na wabunge wa CCM lakini wenzao wakipewa dakika hizo chache wanatema madini, wanahoji na kuelekeza serikali ipasavyo?
Kwani wabunge wa upinzani wanalipwa zaidi kuliko hao wa CCM mpaka wao wanatumia muda kufanya research na kuzungumzia matatizo yetu?
Mfano mtumishi mstaafu anahitaji maslahi yake yazungumziwe, hizo habari kuwa mbunge ni wa CCM au upinzani inamsaidia nini zaidi ya kutekelezewa shida zake?
Hakika kuchagua tena ccm ni kuhujumu maisha yako binafsi

Madaraka hulevya kwa kitambo kifupi sana, lkn historia na uovu humwandama mtu popote pale alipo baadaye ama ktk ulimwengu wa mwili au roho.

Sawa kabisa. Kwani Pierre Nkurunziza yupo wapi!
 
We nae umetokea wapi? Unadhani kutokuipenda hiyo CCM au uchungu wa kutumbuliwa kwako au kuminywa mianya ya pesa mlizozoea siku zote hasira zako ndo zitawabadirisha wananchi wengine?mlio wengi mko watu wa aina tatu tu..wenye uchu wa kuongoza serikali kisiasa,vyeti feki,au wale waliokua wamezoea kujichukulia tu pesa za wananchi ovyo ovyo na sasa wamebanwa. Makundi hayo matatu lazima utakuwepo sasa usilazimishe uma mzima ufuate mawazo mgando,najua utachukia lakini huu ndo ukweli,yule mzee hata mumchukie vipi ni MUNGU ndo aliamua awe mkuu,hiyo ni mamlaka ya ki MUNGU,mapungufu kadhaa ya watu wake hayawafanyi na ninyi ndo muwe hamna shida,mna shida pia..nyingi tu.
 
Kale kadada kalipewa bomba la kichwa,nkaona kwa muda mfupi kapoteza network mara akae,mara aamke,mara avue barakoa pumzi imekata yani kalikosa uvumilivu...ila ni kamboga kazuli tu kimuonekano.
 
Hao wote hua wanajuana,mnatengenezewa movie tu,jitahidi kufanya yako uache ya watu?hamsitukagi tu?kaa nao karibu baada ya hapo ndani ili waonekane kwenye tv utawaona wote wanakula meza moja wakicheka
 
Back
Top Bottom