hebu tujiulize watanzania. Mtu akikunyooshea kidole kimoja cha shahada huwa inamaanisha nini? Binafsi huwa ninaona ishara hiyo hutolewa na mtu akikasirika kwa maana ya kumtukana.
Kuna tofauti gani na kusema "wewe unatiwa nini?".
Ukweli Halima Mdee alifanya kitendo sawa na yule Mwenyekiti Mabumba aliyemwambia John Mnyika "Hivi unawashwa nini?"
Nakumbuka kuna wakati hapa nchini Hadija Kopa na Nasma walitunga taarabu iliyoleta sokomoko kwa wimbo usemao "wadudu wananyemvuanyemvua". Ndiyo yaleyale.
tatizo siku hiyo TV zote za Bunge zilikuwa zinamuonyesha Job Ndugai aliyekuwa amesimama anajibu swali hivyo hazikuwa zimemlenga Halima Mdee, kama jinsi kwenye fainali za kombe la dunia za Mwaka 2006 ambapo TV hazikumuonyesha Zinedine Zidane wakati anampiga kichwa Materazi na isingekuwa kutorudiwa kwa TV (replay) nbasi tusingeona alivyomtwanga kichwa.
Lakini katika kujitetea Zinedine pia alijitetea kama Job Ndugai kwamba alitukanwa matusi ambayo yalisikika kwa waliomo uwanjani tu na TV zisingeweza kuona au kusikia.
Hiyo inaitwa "Provoking".
Nina uzoefu binafsi hata kwenye magovmi ya familia, mtu huwezi kuja kuniambia kwamba fulani kamuua ndugu yake kwa ugomvi wa shilingi moja. Lazima nichunguze jambo kubwa lililojificha nyuma yake. Maana provoker hupenda kutumia public kama silaha yake kwa sababu sisi public hatukujua nini kilitokea nyuma ya pazia.
Lakini provoker naye hufanya hivyo akijua kwamba jamii inayomzunguka ni mazuzu ambayo hayatajikita kutafuta ukweli wa chanzo.
Jiulizeni, ni nini historia ya Halima Mdee kulingana na maadili? Je, kesi yake aliyoshitakiwa na James Mbatia ilikuwa na msingi gani? Je, haukuwa msingi wa matusi?
Je, kwa nini Halima Mdee huyohuyo na kwa Naibu Spika huyohuyo mwaka jana aliambiwa neno kubwa zaidi kwamba "Bungeni si mahala pa kuvutia bangi?" .
Tuache utani. Siwapendi CCM lakini tunaweza kuwaondoa CCM bila kuwatukana hata tusi moja.
katika kipindi cha Tuongee Asubuhi cha Star Tv leo akijibu swali nililouliza na kurudiwa na Uswe wa jF alijibu, 'Mdee alionesha dharau na kubinua vidole'
my take:
ungeomba radhi ingekuwa bora kuliko kumtusi. Na utetezi ni kujikosha tu kwani tuliona Live na pia hata body language yake na yako na pia wageni wa studio akina Lissu na Machali imeonesha kuwa unadanganya.
Ukweli utabaki kuwa unachukia upinzani na ndo maana hata umekosa uvumilivu katika studio za Star Tv leo
katika kipindi cha Tuongee Asubuhi cha Star Tv leo akijibu swali nililouliza na kurudiwa na Uswe wa jF alijibu, 'Mdee alionesha dharau na kubinua vidole'
my take:
ungeomba radhi ingekuwa bora kuliko kumtusi. Na utetezi ni kujikosha tu kwani tuliona Live na pia hata body language yake na yako na pia wageni wa studio akina Lissu na Machali imeonesha kuwa unadanganya.
Ukweli utabaki kuwa unachukia upinzani na ndo maana hata umekosa uvumilivu katika studio za Star Tv leo
ukiona mtu anatumia kauli za 'unawashwawashwa', 'kituko', ujuwe ameishiwa hoja, na sasa anajaribu kushambulia saikolojia, kitu ambacho huwa hakifanikiwi, hasa kama anayeshambuliwa ni strong. sina shaka na uimara(kifikra) wa John na Halima na Watanzania kwa wingi wao.
kabisa mkuu! Kazidi kujichafua na hata ile introduction yake ilionesha kuwa he did it deliberately.
Na Halima alikuwa anawashwa-washwa kama Mnyika?
it wasn't deliberate, but Ndugai won't say that kwa sababu tutamwambia aombe radhi/afute kauli.
alikua provoked (according to him) and his anger got the better off him, he acted out on impulse, without self-thought. . . but he will never accept kwamba he actually acted bila kufikiri
Mkuu, sikujua kama na wewe ni Mheshimiwa Mbunge, na ulikuwemo mjengoni na ukamuona Halima 'akibinua vidole'. Au wewe ni miongoni mwa wale askari waliomtoa nje Machali?tatizo siku hiyo TV zote za Bunge zilikuwa zinamuonyesha Job Ndugai aliyekuwa amesimama anajibu swali hivyo hazikuwa zimemlenga Halima Mdee,