Zero IQ
JF-Expert Member
- Dec 21, 2016
- 13,917
- 24,674
Nakumbuka nilikuwa na Ndoto moja tu katika Maisha yangu nayo ni siku Moja nije Kuwa padre,
Umaskini ndio ulifanya nisitimize Ndoto zangu na leo Nimekuwa Mchakataji.
ilikuwa hivi wakati Nasoma nilikuwa mtumishi kanisani, nilianza kuwa Mtoto wa yesu, nikaja kuwa minsrati(wale watumishi wa padre pale mbele), nikamalizia na kuwa kwaya master (yule anayeongoza waimbaji pale mbele ),
Kutokana na kutumikia kanisa tangu nikiwa mdogo nilitamani sana siku moja nije kuwa padre na nilijiwekea Nadhiri kabisa sitoweza kukutana na mwanamke mpaka kifo changu ikitokea nikatimiza Ndoto zangu,
Nilikuwa na Wivu kila nilipokuwa nawaona mapdri walivyokuwa wanamtumikia Mungu kwa unyeyekevu mkubwa vile,
Picha lilianza nilivyofika darasa la saba, nilijitahidi kumuweka mzee sawa akanilipia hela ya mtihani wa seminary, Nakumbuka tulikuwa zaidi ya watu 60 kutoka tarafa moja tuliofanya mtihani ule na majibu yalipotoka tulifaulu watu 10,
Hapo bado kulikuwa na interview ya kupunguza tulivyofanya tulichaguliwa watu 4 tu nikiwa mmoja wapo,
Mimi na mwenzangu mmoja tulipangiwa tukasome Seminary ya Kasita,(KASITA SEMINARY) iko inapatikana wilaya ya mahenge/Ulanga,
Na wengine 2 waliobaki mmoja alipangiwa ST PETER SEMINARY MOROGORO, na mwingine DON BOSCO SEMINARY.
Kitu sitoweza kusahau ni kwamba mwezi mmoja kabla ya kwenda kujiunga na shule mzee aliyumba kidogo kiuchumi, kilimo alichokuwa anategemea kikagonga mwamba mambo hayakuwa mambo hivyo alikosa pesa ya kunisomesha,
Ada kwa wakati huo ilikuwa imefika laki 6,na michango mingine midogo midogo ilikuwa inafikia laki 4, hivyo ilitakiwa kama milioni 1 tu, na ilipwe kwa awamu nne lakini ndio hivyo Umaskini bwana ni kitu kibaya sana mzee alishindwa kabisa("sitomlaumu mzee kwa nini Alishindwa ila nazidi kumuombea tu nachojua ni kwamba alijitahidi sana ila ndio hivyo" )
Baada ya kukosa Ada nilienda kusoma shule ya kata,
Mwishoni mwa kidato cha kwanza kuna shangazi yangu flani dada wa kwanza wa mzee wangu ofcourse alikuwa na pesa ninavyosema pesa namaanisha(wakati huo alikuwa anamiliki gari 2 za kutembelea, Nyumba moja kubwa dar, nyumba 2 kubwa morogoro mjini, shule ya ushonaji na kiwanda kidogo cha ushonaji pale Morogoro, Gest moja na ukumbi mkubwa huko wilayani kwetu maduka ya nguo na reja reja , pia alikuwa anamalizia kujenga hotel ya ghorofa tatu hapo morogoro kabla ya kifo chake R.I.P, na biashara nyingine nyingi tu)
Alisema atanisomesha hivyo nifanye tena mtihani, kwa kuwa nilikuwa na Ndoto nikakubali nikafanya tena wakati huo niko kidato cha kwanza nikafaulu na kuchaguliwa tena pale pale KASITA SEMINARY, Lakini ilipofikia wakati wa mimi kwenda shule alikataa kata kata kunisomesha
"Hakika mtegemea cha ndugu hufa maskini" yule shangazi yetu alikuwa na kila kitu lakini hakuweza kusaidia Ndugu yake ata mmoja zaidi ni kwamba alikuwa anasaidia watu baki na wengi wamefaidikia kupitia yeye lakini Ndugu ata mmoja hakuna aliyepata msaada wake au ata kumsogeza mahala(hapa niwape kongole wachanga wanajua kusaidiana) lakini baadhi ya makabila kama hili la kwetu ni ovyo tu,
Niliumia sana siku ile and that was a day Ndoto yangu ilibaki kuwa ndoto ambayo haikuweza kutimia,
Baada ya kushindikana kwa mara ya pili tena kwenda kujiunga na Seminary ambayo ingeniwezesha kutimiza ndoto zangu niliendelea tu kusoma pale shule ya Kata, shule ya serikari ambayo leo hii imenipelekea mimi kuwa Mchakataji.
Cc Zero IQ