Ndoto za marehemu Regia, alivyosaidia jamii | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ndoto za marehemu Regia, alivyosaidia jamii

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Saint Ivuga, Jan 17, 2012.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,779
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Ndoto za marehemu Regia, alivyosaidia jamii
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Monday, 16 January 2012 20:42 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 0digg

  Waandishi Wetu
  KIFO cha Mbunge wa viti maalumu (Chadema) Regia Mtema kimefuta ndoto nne kuu za mbunge huyo wa upinzani alizopanga kuzitekeleza katika kipindi cha miaka mitano ya ubunge wake inayoishia 2015.

  Regia aliyefariki dunia Januari 14 mwaka huu kwa ajali ya gari mkoani Pwani, alipanga kuwakusanya yatima na walemavu na kuwahifadhi kwenye nyumba aliyoinunua eneo la Mbezi Makabe kisha kuendelea kuwafadhili kwa mambo mbalimbali.

  Mbali na kuwafadhili watu wanaoishi kwenye mazingira magumu, Regia pia alishaiambia familia yake kuwa angegombea ubunge wa jimbo, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kisha kutumia sehemu kubwa ya mshahara wake kwa yatima.
  Katika mahojiano maalumu na gazeti hili jana, mama mzazi wa Regia, Catherine Kihaule alisema kifo cha binti yake huyo, kimeacha simanzi sio tu kwa wanafamilia bali jamii kubwa ya watu aliokuwa akiwasaidia.

  Matarajio ya Regia
  Akielezea matarajio ya mwanaye, Catherine alisema "Regia aliwahi kuniambia kwamba anatamani uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 agombee ubunge wa kuchaguliwa na wananchi na sio kupitia viti maalumu."

  “Nakumbuka maneno ya mwanangu aliyowahi kuniambia kwamba mama sasa nimekuwa kisiasa natamani uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2015 nigombee ubunge kwa njia ya kuchaguliwa na wananchi na sio viti maalumu tena.”

  Mama huyo anaeleza kuwa Regia alikuwa anaishi na watoto wawili waliotoka katika mazingira magumu, ambao alikuwa anawalea kama wanaye. Kati ya hao mmoja alikuwa miongoni mwa watu ambao alipata nao ajali iliyomsababishia kifo, alisema.

  “Regia alikuwa analea watoto wawili waliotoka katika mazingira magumu ambapo mmoja aitwae Rojas Abdalla alikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwamo katika gari ambalo alipata nalo ajali na kumsababishia kifo,” alieleza.

  Alieza kwamba katika matarajio yake mengine yalikuwa kujiendeleza kielimu huku akiwa na lengo la kupata shahada ya uzamili na kutaka kujenga nyumba ya kuishi yeye binafsi ambapo nyumba aliokuwa anaishi awali alitaka kuwaachia watoto wanaoishi katika mazingira magumu.

  “Regia alikuwa na lengo la kuwakusanya watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili awahudumie kwa kuhakikisha wanapata elimu itakayowawezesha kuendesha maisha yao bila shida,” alieleza.

  ...Ulemavu wake sio wa kuzaliwa
  Catherine anasema ulemavu aliokuwa nao Regia hakuzaliwa nao bali ulitokana na michezo ya utotoni. Alisema mwaka 1987 akiwa na umri wa miaka saba, alipata ajali alipokuwa anacheza 'rede' na kusababisha akatwe mguu wake wa kulia.

  "Mwanangu alipata ulemavu kutokana na mchezo wa watoto wa kike unaojulikana kama rede. Siku moja akiwa anacheza na wenzake alipata mshtuko katika paja la kulia hali ambayo ililazimu kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ludewa mkoani Iringa kwa matibabu," anasema Catherine na kuendelea:
  “Tatizo aliolipata mwanangu lilikuwa kubwa kutokana na mishipa ya eneo aliloumia kushindwa kupitisha damu ipasavyo.”

  Alieleza kwamba hali hiyo ilitokana na kufungwa plasta baada ya kumfikisha katika Hospitali ya ya Wilaya ya Ludewa mwaka 1987 bila madaktari kufahamu ukubwa wa tatizo lake.

  Aidha alieleza kwamba baada ya kuona hali inakuwa mbaya walimhamisha katika Hospitali ya Peramiho ambako alikutana na madaktari bingwa wa mifupa walioshauri akatwe mguu.

  Alieleza kuwa baada ya hapo Regia alikatwa mguu wa kulia na kuanza kutumia mguu mmoja wa kushoto ambapo hali hiyo aliizoea na kujiona kama yupo sawa na wenzake
  .
  ...ajali ya Lindi
  Catherine alisema ajali iliyomwua Regia sio ya kwanza katika maisha yake. Miaka mitano iliyopita, Regia alishawahi kupata ajali mbaya akiwa anatoka Dar es Salaam kuelekea Lindi na kupata majeraha makubwa.
  “Mwanangu alishawahi kupata ajali mbaya na akaumia vibaya, lakini leo tena anapata ajali na kufariki dunia, inaniuma sana nikiwa nakumbuka matukio haya,” alieleza mama huyo huku akibubujikwa machozi.

  ...Elimu na harakati za siasa
  Akizungumzia historia ya Regia mama huyo anasema alizaliwa Aprili 21, 1980 na kupata elimu ya Msingi mwaka 1989 na 1995 alijiunga na Shule ya Sekondari Forodhani, Dar es Salaam mwaka 1996 hadi 1999 na kuhitimu Kidato cha nne.
  Aliendelea na kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa ambako badaye alihamishiwa katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Machame, mkoani Kilimanjaro.

  Mwaka 2003 hadi 2006, Regia alisoma Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (Sua) na kupata shahada ya maarifa ya Nyumbani na Lishe.

  Baada ya hapo Regia alifanya kazi katika taasisi mbalimbali kabla ya kujiunga na Chadema na kuteuliwa kuwa Ofisa Mwandamizi katika kurugenzi ya vijana ya chama hicho.
  Badaye aliteuliwa kuwa Ofisa Mwandamizi katika kurugenzi ya mafunzo ya chama hicho nafasi ambayo aliishikilia hadi mwaka 2010 alipoteuliwa kuwa Mbunge.

  ...aliowafadhili wamlilia

  Familia ya walemavu iliyokuwa inafadhiliwa na aliyekuwa Mbunge wa (Chadema)viti maalumu Regia Mtema aliyefariki mwishoni mwa wiki imeelezwa kushtushwa na kifo cha ghafla cha mbunge huyo.

  Mbunge huyo alikuwa anawapatia kiasi cha Sh100,000 kila mwezi kutokana na mapato yake ya Bunge mama na mtoto ambao wote ni walemavu wanaoishi mjini Bukoba na aliahidi kufanya hivyo katika kipindi chote cha maisha yake bungeni.

  Marehemu Regia Mtema alifahamiana na mama huyo akiwa na mtoto wake wakitembea kwa kutambaa wakati alipofanya ziara ya kuhamasisha shughuli za chama chake mwanzoni mwa mwaka jana.

  Akihojiwa na Mwananchi nje ya kituo cha mabasi mjini Bukoba mwanamke huyo Edna Kalinga ambaye hufanya biashara ya kuuza chumvi ya paketi akiwa na mtoto wake Kakuru Johanes alisema kifo cha Regia ni pigo kubwa kwake na mwanaye.

  Alisema alipewa taarifa za kifo cha Mbunge huyo siku ya Jumapili jioni akiwa katika kituo chake cha kazi na kuwa kila mwezi alitumiwa kiasi hicho cha fedha kama alivyowaahidi.

  "Nilijisikia vibaya baada ya kupata taarifa za kifo cha mfadhili wetu alitutumia Sh100,000 kila mwezi angekuwa mtu wa hapa karibu ningehudhuria mazishi yake," alisema Edna.

  Alisema marehemu Regia alionyesha upendo mkubwa hasa kwa watu wenye mahitaji kama yeye na kuwa kiasi cha fedha alizokuwa anatumiwa zimemsaidia kukidhi mahitaji mbalimbali yeye na mtoto wake.

  Alisema matarajio yake kwa baadaye ilikuwa ni kununua pikipiki ambayo ingekuwa inamsafirisha kila siku hadi mjini kutokana na umbali mrefu uliopo kati ya Mji wa Bukoba na Kijiji cha Kitendagulo ambacho kipo kilometa kadhaa nje ya mji.

  Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Wilaya ya Bukoba Victor Sherejei alithibitisha kuwa mbunge huyo alikuwa akituma kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kumsaidia mlemavu huyo na mwanaye.

  Alisema chama kilimsaidia kufungua akaunti katika Benki ya CRDB Tawi la Bukoba na kuwa hadi mwishoni mwa mwaka jana, Legia Mtema alikuwa akituma Sh100,000 katika akaunti hiyo kutokana na mapato yake kama mbunge.

  Akizungumzia hatima ya mlemavu huyo Sherejei alisema kwa vyovyote vile mchango huo utakuwa umekoma baada ya kifo cha Legia Mtema na kuwataka watu kujitokeza kuendeleza juhudi alizoanzisha kama njia ya kuenzi mchango wake wa kutambua watu wenye mahitaji mbalimbali wakiwemo walemavu.
   
  Habari hii imeandaliwa na Phinias Bashaya, Bukoba na Aidan Mhando na Shakila Nyerere[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jan 17, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Inasikitisha na kutia moyo kwa wakati mmoja.
  May her soul rest in peace.
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,435
  Likes Received: 19,779
  Trophy Points: 280
  kweli Lizyy mimi imenifariji sana hasa hayo mambo ambayo alikuwa anafanya na plan zake
   
Loading...