Ndoto ya Mauti kwa Mwanao

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,930
4,893
Wakuu nini maana ya ndoto Inayohusu wanga wakitaka kumdhuru Mwanao ..imenitokea Mimi tena nimeota mara mbili.... ya kwanza ilikuwa saa kumi na dk 40 ambapo nilitewa chumbani na mwenzie anayelala naye kuwa baba fulani kuna jitu linamkandamiza kifua na linataka kumuaa.

Basi walipohamia kwangu huku nikiwa nimemkumbatia mwanangu ndipo likaja lijinamizi likitaka kuninyanganya mwanangu nikalishinda basi ikabindi niangushe moja ya sala ya kukemea roho yoyote mbaya kwa mwanangu pamoja na familia nzima.

Basi nikiwa chumbani mnamo saa kumi na moja na dk kadhaa niliota kuwa kuna mtu yupo dirishani anachungulia , nikainuka nikamuangalia, kweli akawepo, sasa kila nikisogea karibu ya dirishani kumtazama vizuri anarudi nyuma na kujificha pembeni,ikabidi nivae nguo faster nitoke nje kumuona vizuri akawa naye ametoka faster nje ya fence.

Basi ile narudi tu ndani nikafika sebuleni nikamkuta yule na kumkuta yule Aliyekuwa analala na mwanangu yupo kwenye kochi nikamuuliza ili anieleze vizuri kilichikuwa kinatokea ndipo akanisimulia kuwa kweli alikuwa anakandamizwa na kuna muda alipoteza kuhema. Nilimjibu kuwa ni kweli Nimeona akaniuliza umejuaje nikamwambia nimeonyweshwa ndotoni.

Basi ile narudi chumbani namkuta mwanangu ndiyo yupo karibu the last stage nikambeba nikaja naye sebuleni nalia Namwambia usife mwanangu akaongea maneno machache akalegea.
Aisee nimekemea roho ya Mauti sana na nilipomaliza nikipooangalia muda ukawa saa kumi na moja na dk 50.

Kwa nini ndoto hii ....na nini maana yake..... na kwa nini awe mwanangu. ....nimejiuliza mengi mno...nipo confused.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom