Loh! Inasikitisha kuwa watu hawana kumbukumbu hata kidogo. Jamaa ahadi aliyoitoa ilikuwa kwamba mwaka 2006 barabara ndipo ingekamilika. Sasa ni miaka kumi baadaye. Kwa mwendo huo wa konokono tutafikia lini kwenye maendeleo tunayoyatamani? Hata kobe akiahidi kuizunguka dunia ukimpa miaka sabini (maana huishi miaka mia na ushee) anaweza kutimiza ahadi yake.
Ukonokono wa serikali ya FISI WENU (mgombea wa kitengo Magufuli akiwemo) ni moja ya vichocheo vya kuindoa madarakani.
Kuhusu mgombea wa UKAWA, huwezi kuzungumza lolote kuhusu sekondari za Kata bila kutaja jina lake. Maji ya Ziwa Victoria kufika Shinyanga, Kahama, Mwadui, jina lake limeandikwa humo. Mkuu kama ulikuwepo kulikuwa na kampuni moja inaitwa City Water ambayo ilivurunda kazi na kutetemesha jiji la Dar. Alifuta mkataba na walipokwenda mahakamani serikali ikashinda (sio samaki wa Magufuli ambapo tulipigwa bao). Waliokuwepo zamani enzi za Ruksa wanakumbuka kuwa bila huyo mgombea wa Wananchi, sasa hivi eneo la Mnazi Mmoja lisingelikuwa wazi tena. Lingeshayoyoma! Hayo ni machache tu. Mengi subiri muda ukifika wananchi wenyewe wenye mgombea wao watakujulisha.
Haya kwani 2006 Magufuli alikuwa wazir wa ujenzi? Alafu kuhusu samaki wa Magufuli ile meli ilikamatwa kwa mujibu wa sheria kwa hiyo swala la kushindwa kesi sio suala la Magufuli.Hivi wewe hujui kuwa leo hii serikali inashindwa kesi kila kukicha.? Hujui kuwa kwenye mahakama kuna uhozo mkubwa?