Ndoto ya Magufuli yatimia

Ndoto ya Magufuli yatimia

Controversial

Member
Joined
Mar 8, 2015
Posts
42
Reaction score
6
Ni ile ya kutoka Mtwara mpaka Bukoba kupita katika barabara ya lami. Ni mwaka 2005 alipotoa maneno hayo;

Mkapa na Magufuli mwaka 2005 Jiwe la Msingi Nangurukuru – Mbwemkuru (Lindi) km 95.

Rais Benjamin Mkapa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli mwaka 2005 walipoweka Jiwe la msingi Barabara ya Nangurukuru - Mbwemkuru (Km 95). Ujenzi wa barabara hii ulikamilika Januari, 2008.

WANANCHI wataweza kusafiri kutoka Mtwara hadi Bukoba kwenye barabara ya lami,hayo yalisemwa Bungeni Mjini Dodoma wakati Waziri wa Ujenzi John Magufuli alipokua akijibu swali la Martha Mlata (Viti Maalum-CCM), swali lililohoji juu ya ahadi ya Serikali katika kipindi cha awamu ya nne na ahadi hiyo iliyosema wananchi wataweza kusafiri kwa taxi toka Mtwara hadi Bukoba. Waziri Magufuli alisema kuwa nia ya msemo huo ni kuonesha kwamba wananchi wataweza kusafiri toka Mtwara hadi Bukoba kwa lami na kuongeza kuwa lengo hilo limetekelezwa kwa mafaniko makubwa hadi kufikia asilimia 99 ya barabara yote kutokea Mtwara hadi Bukoba.

Hata hivyo ahadi ya Magufuli imetekelezwa kwa kuwa sasa barabara yote kuanzia Mtwara – Dar es Salaam- Dodoma-Singida- Nzega-Tinde-Usagara pamoja na Geita-Bwanga-Kyamyorwa hadi Bukoba yenye urefu wa kilometa zipatazo 1,989 imejengwa kwa kiwango cha lami.

Serikali ya awamu ya nne imetimiza ahadi ya wananchi ya kusafiri kwenye barabara ya lami kutoka Mtwara hadi Bukoba imetekelezwa kwa asilimia mia moja (100%).

Last edited by a moderator:
Hatutaki rais atakae deal na barabara peke yake kwani sisi watanzania tuna mambo mengi kama vile maji,umeme,afya n.k hivyo rais pekee wakututoa ktk matatizo yote hayo ni LOWASSA.
 
Hiyo ndo machine yenyewe na sasa tunampeleka Ikulu ili aendelee kujenga na nyingine kibao, sahiv Barbara kama unateleza vile
 
Ni bora kumpima mgombea uraisi ambaye tumekaa nae Serikalini akatufanyia kazi zikaonekana na mwisho wa siku tunampa pakubwa zaidi. Alijitahidi katika Wizara ya Ujenzi na rekodi nzuri ya uchapakazi.
 
Hajanishawishi, huyo Apewe wizara tu, taasisi ya urais ni zaidi ya magufuli

Kikwete mwenyewe kashindwa kuvaa viatu vya Mkapa
 
Kweli ametimiza na hata akisema October atakwenda magogoni kwa vingora pia inakuja kua kweli.
 
Hiyo ndo machine yenyewe na sasa tunampeleka Ikulu ili aendelee kujenga na nyingine kibao, sahiv Barbara kama unateleza vile

Mwaka huu mnalo na limeng'ang'ania kwel kwel hamchomoi haki ya nan nawaambia
 
Ni ile ya kutoka Mtwara mpaka Bukoba kupita katika barabara ya lami. Ni mwaka 2005 alipotoa maneno hayo;

Mkapa na Magufuli mwaka 2005 Jiwe la Msingi Nangurukuru – Mbwemkuru (Lindi) km 95.

Rais Benjamin Mkapa na Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli mwaka 2005 walipoweka Jiwe la msingi Barabara ya Nangurukuru - Mbwemkuru (Km 95). Ujenzi wa barabara hii ulikamilika Januari, 2008.

WANANCHI wataweza kusafiri kutoka Mtwara hadi Bukoba kwenye barabara ya lami,hayo yalisemwa Bungeni Mjini Dodoma wakati Waziri wa Ujenzi John Magufuli alipokua akijibu swali la Martha Mlata (Viti Maalum-CCM), swali lililohoji juu ya ahadi ya Serikali katika kipindi cha awamu ya nne na ahadi hiyo iliyosema wananchi wataweza kusafiri kwa taxi toka Mtwara hadi Bukoba. Waziri Magufuli alisema kuwa nia ya msemo huo ni kuonesha kwamba wananchi wataweza kusafiri toka Mtwara hadi Bukoba kwa lami na kuongeza kuwa lengo hilo limetekelezwa kwa mafaniko makubwa hadi kufikia asilimia 99 ya barabara yote kutokea Mtwara hadi Bukoba.

Hata hivyo ahadi ya Magufuli imetekelezwa kwa kuwa sasa barabara yote kuanzia Mtwara – Dar es Salaam- Dodoma-Singida- Nzega-Tinde-Usagara pamoja na Geita-Bwanga-Kyamyorwa hadi Bukoba yenye urefu wa kilometa zipatazo 1,989 imejengwa kwa kiwango cha lami.

Serikali ya awamu ya nne imetimiza ahadi ya wananchi ya kusafiri kwenye barabara ya lami kutoka Mtwara hadi Bukoba imetekelezwa kwa asilimia mia moja (100%).

So what.., umburura huo we huoni upande mwingine wa shilingi mambo yalivyoharibiwa na CCM? Thamani ya pesa yetu vip? mfumuko wa bei? ufisadi - escrow, epa, richmond? tembo wetu...? Muwe na akili nyie mazuzu
 
Last edited by a moderator:
Barabara, cjui hospital na Huduma nyingine za kijamii n jukumu la serikali. Na kiongozi anayeomba kura kwa hoja za kujenga barabara kwangu mm n sawa na mwanafunzi wa form iv anaandika essay ya civics au n baba anayeomba shikamoo kwa watoto ndo atoe chakula. Tunamtak kiongozi atakayesimamia mgawanyo sawa wa rasilimali zetu ili tupate hizo Huduma za kijamii. Magufuli mfumo ushamkosesha sifa maana atasimamia yaleyale ya hati ya dharura
 
Kwahiyo angeshindwa kujenga barabara akiwa waziri wa ujenzi mgesemaje? Wengine walitaka eti ajenge na hospitality,bandari ,na viwanda , alafu eti apambane na majangiri uku akiwa waziri wa ujenzi.....hahaa...watu wengine wanachekesha sana.
 
Magufuli hajawahi kuwa na ndoto za urais wala vision huku n kukurupushwa hivyo tusitegemee mapya zaidi tuendelee kuumia
 
Tujadili kwa hoja kwani mgombea wenu wa CHADEMA alifanya mazuri yapi akiwa waziri.?
 
Loh! Inasikitisha kuwa watu hawana kumbukumbu hata kidogo. Jamaa ahadi aliyoitoa ilikuwa kwamba mwaka 2006 barabara ndipo ingekamilika. Sasa ni miaka kumi baadaye. Kwa mwendo huo wa konokono tutafikia lini kwenye maendeleo tunayoyatamani? Hata kobe akiahidi kuizunguka dunia ukimpa miaka sabini (maana huishi miaka mia na ushee) anaweza kutimiza ahadi yake.

Ukonokono wa serikali ya FISI WENU (mgombea wa kitengo Magufuli akiwemo) ni moja ya vichocheo vya kuindoa madarakani.

Kuhusu mgombea wa UKAWA, huwezi kuzungumza lolote kuhusu sekondari za Kata bila kutaja jina lake. Maji ya Ziwa Victoria kufika Shinyanga, Kahama, Mwadui, jina lake limeandikwa humo. Mkuu kama ulikuwepo kulikuwa na kampuni moja inaitwa City Water ambayo ilivurunda kazi na kutetemesha jiji la Dar. Alifuta mkataba na walipokwenda mahakamani serikali ikashinda (sio samaki wa Magufuli ambapo tulipigwa bao). Waliokuwepo zamani enzi za Ruksa wanakumbuka kuwa bila huyo mgombea wa Wananchi, sasa hivi eneo la Mnazi Mmoja lisingelikuwa wazi tena. Lingeshayoyoma! Hayo ni machache tu. Mengi subiri muda ukifika wananchi wenyewe wenye mgombea wao watakujulisha.
 
Back
Top Bottom