Ndoto "mpya" ya kakobe yaitesa ukawa!

Mustakabali wa taifa hautegemei ''NDOTO'' ,unategemea UWAJIBIKAJI wa kila mwenye WAJIBU ili kujenga taifa bora. NDOTO ni maluwe-luwe tu ambayo humtokea mtu yeyote hata mwenda-wazimu.

Angesema kuwa kaoteshwa ndoto ya "Serikali 3/Nchi 3" ungemshangilia na kurukaruka kwa furaha! Tatizo la ndoto yake ni pale inapokuwa tofauti na mawazo yako!
 
Mwaka 1995 kakobe alisema mrema asipo shinda hataingia tena kanisani maana alikua mpambe wa mrema na akashindwa uchaguzi;kwa sasa kakobe anaongoza kanisa mpaka leo
 
Ukawa ni kikundi cha wanasiasa wenye lengo moja, sasa anataka Mrema awe pamoja nao wakati yeye ana malengo tofauti na wenzake? Kisa ni muanzilishi wa upinzani? Kobe kasha zeeka sasa

Mimi nijuavyo watu wote hawawezi kuwa na mawazo sawa milele, wewe subiri anguko kubwa la UKAWA! Tundu Lissu alituaminisha kuwa "hakuna ndoa ya waume wengi na haitakuwa" yaani CHADEMA vs CUF! All of a sudden tumeona hiyo ndoa tuliyoambiwa haiwezekani imewezekana bila kutoa ufafanuzi wa kauli zao za mwanzo! Hapa hakuna umoja wa dhati na wakikosa kile walichokuwa wakitafuta, yaani "Serikali 3/Nchi 3" watasambaratika kwa kuwa hawatakuwa na "Common Cause!"
 

Ushauri wangu kwa Kakobe:Shughulika na wito wako (mambo ya kiroho) ni vigumu kutumikia mabwana 2.
 
Babu wa loliondo nae awaite UKAWA wakanywe kikombe ili wapete kufanikiwa katika harakati zao za kutetea wanyonge,,,,,kwikwikwi
 
Ushauri wangu kwa Kakobe:Shughulika na wito wako (mambo ya kiroho) ni vigumu kutumikia mabwana 2.

Mbona Kakobe alisifiwa sana alipotetea "Serikali 3/Nchi 3" na hatukusikia story za wito?
 

Huu ni uzushi wa mchana kweupe!Hakuna kitu cha namna hiyo kilichozungumzwa na Askofu Kakobe leo kwenye ibada.Askofu Kakobe ni mtu makini sana sana! hazungumzi ilimradi azungumze.Mtu anapozungumza uongo wakati maelfu ya watu walikuwepo leo kwenye ibada FGBF Mwenge na asifahamu kwamba watakuja kukanusha sijui anawaza nini?Sikuzote uongo haulipi na mwisho wake huwa ni fedheha.
 
Moderator, Mtoa mada ameandika hapa UONGO WA MWAKA. Mimi nilikuwepo katika Ibada ya leo kwa Kakobe, na Askofu Kakobe hakuzungumzia hata neno moja la siasa au lenye "implication" ya kisiasa. Muda wote amezungumzia umuhimu wa Wakristo kuhubiri pia Injili mahali pengine mbali na eneo la nyumbani kwao walikozoea kuhubiri. Kichwa cha somo kilikuwa "NIPATE KUHUBIRI HUKO NAKO" na Neno la Msingi lilitoka katika MARKO 1:35-38. Moderator ondoa uchafu huu hapa, kwa sababu kila aliyekuwako katika ibada ya leo atashikwa na mshangao mkubwa kuuona uongo huu hapa!
 
Last edited by a moderator:
Kumbe Kakobe hajasema jambo lolote kuhusu UKAWA...Maccm sijui yakoje
 

Kweli kabisa, mimi ni mshirika wa Kanisa la FGBF, na leo nilikuwepo katika ibada Mwenge, huu ni uongo wa kutisha. Askofu Mkuu Zachary Kakobe amezungumza kwamba pamoja na wajibu wetu kuhubiri pale tulipo katika eneo la nyumbani, hatuna budi kufuata kielelezo cha Yesu Kristo cha kuhubiri pia mahali pengine mbali na eneo la nyumbani - MARKO 1:35-38. Baadaye aliwapandisha madhabahuni watu 174 ambao jana walikwenda kuhubiri Kisarawe, Mlandizi, Mkuranga na Kibaha, na wakaeleza yaliyojiri katika mahubiri yao huko.
 

Wewe BK7 acha porojo zako! UMEME HAUPITI PALE. Period!

 

Attachments

  • Gazeti.jpg
    178.6 KB · Views: 392

He he he ! UKAWA na Baraza la Mawaziri kivuli, vimewashika magamba pabaya. Sasa wanaanza kutunga uongo! Mrema na UKAWA, wapi na wapi, Kibaraka mkubwa huyu wa Chama cha Mafisadi! Mwaka huu mtaisoma namba ya UKAWA! Lumumba BK7 ninawapa pole kubwa, kwa kujipanga "full team" kushabikia uongo wa Interahamwe mwenzenu uliowekwa hapa.
 

Uongo mwingine bhana! Mleta mada hii hapa, amebandika uzi huu hapa, saa 5:39 asubuhi, na kuzungumzia eti aliyosema Kakobe katika ibada, wakati Askofu Kakobe aliingia Kanisani katika Ibada Kuu mnamo saa 7:30 mchana, yaani saa mbili nzima baada ya uzi huu kuwekwa hapa! Mimi pia nilikuwepo katika ibada, na Kakobe alihubiri tu juu ya MARKO 1:35-38, hakugusia hata kidogo jambo lolote la kisiasa.
 
Mwaka 1995 kakobe alisema mrema asipo shinda hataingia tena kanisani maana alikua mpambe wa mrema na akashindwa uchaguzi;kwa sasa kakobe anaongoza kanisa mpaka leo



Mungu ni wa Haki,sio wa dhulma.!!
Mwaka 1995 Mrema alishinda na alimuacha mbali sana Ben.
Kumbuka Mrema alikua ni Kipenzi cha wanawake na vijana wakati huo.
Wizi wa kura ulikua mkubwa mno na Nyerere aligoma kumkabidhi mpinzani nchi ,tena kutoka Kaskazini!!!
Na baada ya Nyerere kukataa chaguo la watanzania na Mungu ndipo taifa lilipoangukia kwenye ufisadi mkubwa ulioshamiri mpaka leo,na Nyerere alipojaribu kukemea alipelekwa Uingereza na kurudishwa Butiama(rip)(rejea kauli ya Vincent Nyerere kule Arumeru)
 
Huu ni uongo uliopitiliza, jumapili nimekuwepo kanisani, yaani hata kitu ukawa hakijatamkwa, wewe mleta thread, una hila tu na pengine unataka kuoanisha mambo kwa akili zako mwenyewe, kama yamekushinda kalale sio kuleta habari za kizushi. JF is the home of great thinkers, wewe naona umevamia
 
Unajua mpaka hapo kutokana na maelezo yako we mleta mada sijaona ambapo hiyo ndoto ya Kakobe inavyowatesa Ukawa,kweli akili ni nywele!
 
Walianzia sangara,m4c.magamba. Sasa ukawa.usanii wa upinzani
 
Mkuu tuwekee ushahidi,maana kakobe alipoiandikia ikulu waraka uliwekwa hapa,na wewe ili hoja yako iwe na mashiko tuwekee hapa clip ya ujumbe wa kakobe kwa ukawa.
my take:U
KAWA ni umoja ulioundwa kwa hiari ya waliojiunga nao,si rahisi /vema kumuhusisha mbowe na Mrema kujiunga au kutojiunga na ukawa,kwani jambo hilo liko kwenye uhiari wa mrema mwenyewe.Labda tuambiwe kuwa mrema alitaka kujiunga na ukawa Mh.Mbowe akakataa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…