Ndoto kama hii INA maana gani?

makelejasitta

Member
Jan 25, 2017
24
3
Wapendwa katika BWANA,habari za asubuhi,BWANA wetu asifiwe sana.wapendwa katika harakati za kimaisha nimejifunza hili jambo japo sijalifanyia ufumbuzi

Kwamba katika Maisha usipuuzie ndoto.

Nimejaribu kuangalia wakuu na wafalme katika BIBLIA shida walizozipata baada ya kupuuzia ndoto,hivyo nikajifunza kutozipuuzia kabisa katika Maisha yangu

Sasa Leo nimeota nikiwa safarini na Jamaa yangu niliyewahi kuishi nae mahara Fulani,tukiwa tunaenda mahari Mara akaanza kukimbia Mimi nikaachwa na mshangao sana pale,lakini Mimi nikaongoza nikaenda mpaka kwa mama yangu mzazi nikamkuta anaishi kijijini amejenga nyumba kuwa za nyasi kama mbili kubwa upande wa kaskazini na kusini,na miti mikubwa sana yenye kivuri mingi sana pale nyumbani ila nikaona zile nyumba kama hazijakamilika upande wa mashariki,nikaamka


Mara ya kwanza niliona kama ndoto nzuri lakini ikabidi nitafakari tena,nikakumbuka siku moja nilikutana na habari kwamba eti,ukiota unahesabu hela eti maana yake nyota yako imeibiwa na wachawi.

Nimeona niirejeshe kwenu wapo wenye karama mbalimbali tusaidiane,

Bwana awabariki na asubuhi njema
 
hakuna naeweza kutafsiri ndoto katika enzi hizi, uwezo wa kutafsiri ndoto walikua nayo mitume na manabii enzi hizo. kutafsiri ndoto inahitaji intuition ya hali ya juu. so ni vyema tu ukiota kitu usiki sambaze hadharani, kaa nacho mwenyewe. wengine watakudanganya, wakutushe na pia watatumia fursa hiyo kukutapeli
 
Mtu akikijengea nyumba inaweza maanisha kuwa ni kufa na hivyo ataishi kwenye myumba yake ambayo ni kaburi
 
Back
Top Bottom