Hossam
JF-Expert Member
- Feb 10, 2011
- 3,548
- 2,180
Usiku wa kuamkia leo nimeota ndoto.
Ilikuwa yapata majira ya jioni wakati mimi, mke wangu na mtoto wangu wa miaka sita tulipokuwa tukitembea tembea darajani huku mwanangu akiendesha baskeli ndogo.
Daraja hilo lilikatisha mtoni na kwa upande wa kushoto kulikuwa na sehemu ambapo maji yake yalikuwa safi na hayakuwa yakitembea kwa spidi. Ghafla mtoto wangu akasimamisha baskeli kingoni mwa daraja na kuruka hadi chini na kuanza kuogelea kwa madaha. Nilistuka sana japo mama yake alinijulisha kwamba mwanae anapenda kuogelea jambo ambalo nililipinga na kuanza kumwita kwa hofu arejee tulipo kupitia ng'ambo ya pili.
Nilihofia mnaweza kuwa na mamba hivyo mwanangu angeraruliwa. Nikisema hayo nikatazama nyuma yake na kuomba mamba kama kumi hivi wakimwendea kwa kasi. Nilipiga kelele kumjulisha mwanangu naye bila kupoteza muda aliogelea kwa kasi kuelekea ukingo wa pili.
Alijitahidi sana lakini kuna mamba mmoja mdogo alimkaribia sana hadi mwanangu anatoka mtoni yule mamba aliambulia kuuma gauni lake kwa nyuma lakini mwanangu hakumdhuru. Nilichungulia kwa chini lakini sikumwona mwanangu.
Nisijue la kufanya, nikastuka ndotoni.
Mimi Pangu Pakavu nimeota, naomba wajuzi nipeni tafsiri.