Ndoto inayonisikitisha, msaada please!

Ndoto inayonisikitisha, msaada please!

hakuna chochote hapo mkuu we ipotezee ila usiisahau mapema ili kama utaota tena kama hiyo au inayoendana na hiyo.
pia mwombe Mungu ili ikiwa kuna baya lolote akuepushe nalo.

Tawile kamanda, nitalifanya hilo
 
mzee, wenzio wanakufariji na kukuficha, mimi nitakwambia ukweli wote.

ndoto yako ina maana kwamba, mtoto wako atakabiliwa na hatari ambayo inaweza kupoteza uhai wake kabisa, lakini ataponea chupuchupu. kitu cha muimu ni kwamba, uliona hajafa yaani wale mamba waliokuwa wanamfukuza hawakufanikiwa kumkamata, ni mamba mdogo ndio aling'ata tu gauni hiyo ina maana kwamba atakuwa attacked na kitu kitakachomuumiza kwa kumkwarua tu hatadhurika. tarajia hilo.

ndoto hizi huwa ukiota leo inaweza kutokea ndani ya wiki moja au mbili au mwezi au miezi. hivyo nakushauri anza kuomba Mungu na kukemea na kuvunja ndoto hiyo mbaya kwa Jina la Yesu Kristo lazima itasambaratika.

siku nyingine ukiota ndoto, palepale usiku utakapostuka usisubiri, ujue unapoota ndoto inamaana maadui zako ndio wako kwenye kikao cha kupanga mipango hiyo (maadui wanaweza kuwa wachawi au hata mapepo/mashetani tu huko kuzimu) na Mungu ni mwaminifu huwa anawaonyesha ndoto wabaya na wema. ukistuka tu palepale we kemea na sambaratisha, usipofanya hivyo ujue kuanzia kesho yake wale jamaa wanaanza kuitekeleza kwa kuweka mitego na kutuma mapepo, hivyo wawahi kabla hawajaanza kuitendea kazi wasambaratisha palepale usiku na huwa inafutika na haitatokea. kwasababu haujasambaratisha, jaribu kusambaratisha sasaivi kwamba mitego waliyoitega au maadui waliokaa tayari wasambaratishwe kwa Jina la Yesu, kama hautafanya hivyo itatokea kama ulivyoota. hayo maji ni ni dunia yaani mitaani huko, kuogelea kwenye maji ni kutembeatembea duniani na hayo mamamba inaweza kuwa hatari yeyote ambayo mashetani yametumwa kuja kufanya either ajali, ugomvi, magonjwa etc.

Ushauri mzuri, ufanyie kazi mleta uzi.
 
ukilala unekunja miguu lazima ndoto iwe ya kutisha. jitahidi kutokukunja miguu wakati unapoenda kulala.

Haha ha ha haaaaa!!! Ngano hizi bwana! Eti ukiota ya kutisha unashindwa kujinasua mathalan kukimbia?
 
Pole sna Ndugu jarbu kukemea kwa sababu anachokiota mtu syo kiti cha uongo kumbuka nafsi yako ndo inayofanya hicho kitendo katka ulimwengu wa roho
 
Usisumbuke hakuna anayejua tafsiri yake ila Mungu mweza wa yote na usitake kujua tafsiri yake maana itakupa kuweweseka cha msingi vunja kabsaa kwa jina la Yesu hyo ndoto na haitarudiiiii tenaaaaaaa!
 
Ukiota ndoto unafukuzwa na wanyama kama simba, ng'ombe, nyoka, mamba nk na wakati wanakukimbiza ukawazidi mbio na kuwaacha mbali bila kukufikia au ukapigana nao na ukawashinda; maana yake ni kuwa katika ulimwengu wa roho wabaya wako walifanya jaribio na walituma silaya zao kukuangakamiza, lakini walishindwa kwani kiimani upo imara.

Ukiota ndoto unafukuzwa na wanyama na wakakupata kwa kukung'ata au nyoka akakung'ata na kuingia mwilini mwako;maana yake ni kuwa wabaya wako wametuma silaya zao za kichawi na wamekupata. Kinachofuata ni aina gani ya manuizo yaliyopewa hayo majini lakini ukweli ni kuwa lipo jambo baya tayari limeshafanyika katika ulimwengu wa roho litatimia na kudhihirika katika ulimwengu wa mwili saa, siku na mahali kama yalivyoagizwa yakumalize.
 
kama ni uongo au ukweli, yeye ataleta feedback ktk hili. nina uzoefu na hizo makitu na hakika yake kitu kilichoko mbele yangu huwa nakiota kabla hakijatokea. kuna hatari inamkaribia huyo mtoto wake lakini hatakufa pamoja na kwamba anaweza kukwaruriwa walau kidogo ila hatapata madhara makubwa mtoto wake ataendelea kuishi. kuna siku atakuja kuleta feedback hapa.
Miezi michache baada ya ndoto ile ajira yangu iligoma, nikasota miezi kibao tu, kwa sasa niko job tena, ni kweli uliyosema.
 
mzee, wenzio wanakufariji na kukuficha, mimi nitakwambia ukweli wote.

ndoto yako ina maana kwamba, mtoto wako atakabiliwa na hatari ambayo inaweza kupoteza uhai wake kabisa, lakini ataponea chupuchupu. kitu cha muimu ni kwamba, uliona hajafa yaani wale mamba waliokuwa wanamfukuza hawakufanikiwa kumkamata, ni mamba mdogo ndio aling'ata tu gauni hiyo ina maana kwamba atakuwa attacked na kitu kitakachomuumiza kwa kumkwarua tu hatadhurika. tarajia hilo.

ndoto hizi huwa ukiota leo inaweza kutokea ndani ya wiki moja au mbili au mwezi au miezi. hivyo nakushauri anza kuomba Mungu na kukemea na kuvunja ndoto hiyo mbaya kwa Jina la Yesu Kristo lazima itasambaratika.

siku nyingine ukiota ndoto, palepale usiku utakapostuka usisubiri, ujue unapoota ndoto inamaana maadui zako ndio wako kwenye kikao cha kupanga mipango hiyo (maadui wanaweza kuwa wachawi au hata mapepo/mashetani tu huko kuzimu) na Mungu ni mwaminifu huwa anawaonyesha ndoto wabaya na wema. ukistuka tu palepale we kemea na sambaratisha, usipofanya hivyo ujue kuanzia kesho yake wale jamaa wanaanza kuitekeleza kwa kuweka mitego na kutuma mapepo, hivyo wawahi kabla hawajaanza kuitendea kazi wasambaratisha palepale usiku na huwa inafutika na haitatokea. kwasababu haujasambaratisha, jaribu kusambaratisha sasaivi kwamba mitego waliyoitega au maadui waliokaa tayari wasambaratishwe kwa Jina la Yesu, kama hautafanya hivyo itatokea kama ulivyoota. hayo maji ni ni dunia yaani mitaani huko, kuogelea kwenye maji ni kutembeatembea duniani na hayo mamamba inaweza kuwa hatari yeyote ambayo mashetani yametumwa kuja kufanya either ajali, ugomvi, magonjwa etc.

Bora umesema ukwel kuliko ungemfariji kwa uongo.

Ana uwezo wa kubatilisha alichoota pia
 
Back
Top Bottom