muhuni mpya
JF-Expert Member
- Apr 28, 2018
- 300
- 166
Ndugu zangu, kwa wenye uwelewa wa ndoto kama hizi naombeni mnijuze, nmekuwa nikimuota marehemu baba yangu kila mara lakini kwa muda tofauti tofaut lakini wiki hii tangu ianze nimekuwa namuota mara tatu mfululizo kwamba nipo nae, sasa ndoto niliyoota leo kwamba baba yangu mzima kabisa kakaa kwenye kiti napiga nae stori huku nikiwa napika mayai, nilipomaliza kupika nikamuwekea kwenye sahani nikamwambia kula na mimi uniachie kidogo.Akala akaniachia na mimi nikamalizia, tukawa tunaongea tu anasema sasa hivi sina hela hata kidogo yani nipo tuu, nikakumbuka nikamuuliza account zako zimefungwa baada ya wewe kufariki inakuwaje sasa umerudi na bado hazijafunguliwa, nikamwambia nimekumbuka kitu embu nielezee tulivyokuzika ilikuwaje na mpaka kurudi sasa, akawa anasema kipindi mnanizika nilikuwa nawaona ila kufanya chochote siwezi hadi kunifukia, nikashtuka ndoto ikawa imekatika hapo.
Naomba kwa yeyote anayefahamu au wazo lolote kuhusu ndoto kama hizi.
ASANTE.
Naomba kwa yeyote anayefahamu au wazo lolote kuhusu ndoto kama hizi.
ASANTE.