Ndoto hii ina maana gani?

TAECOLTD

JF-Expert Member
Mar 2, 2013
1,051
1,835
Habari za wakati wanajamvi?! Usiku wa kuamkia Jana asubuhi nimeota ndoto moja ambayo nimeshindwa kuielewa kabisa.

Nilikuwa nimekaa eneo moja mtaani kwetu nkitafakari mambo mengi mengi wakati natafakari nikawa nautazama mti wa muembe uliokuwa umeanguka nikaunyooshea mkono ghafla ukaanza kusimama na kuwa imara tena.

Nikashangaa sana nikajaribu kuzungusha mkono wangu mti nao ukawa unaenda vile mkono wangu unaenda. Nikanyanyuka pale na kunyoosha mkono eneo lenye bustani napo maua yakachipua na kutoa maua yanayovutia.

Nikaondoka nikiwa na furaha sana nikakuta kijana mmoja mlemavu miguu yake imepinda pinda hawezi kutembea nikamnyooshea mkono nikiwa mbali ghafla miguu yake ikanyooka akanyanyuka na kuanza kutembea kwa furaha.

Nikafanya mambo mengi sana ya ajabu kutumia mikono yangu
Nikapandisha mlimani nikakuta vijana wakiwa wanabeba magogo mengi sana nikawaambia niwasaidie hivyo nikanyanyua mikono juu na magogo yote yakapaa hewani nikayaelekeza yaende mahali na kujipanga vyema.

Lakini Nilikuwa na katoto kangu kadogo nikawaambia wamshike wakati nawasaidia lakini nikaona katoto kangu kakipigwa na katoto kao bila wao kuamulia basi nikawaambia kama wameshindwa kumuangalia mtoto wangu mpaka akapigwa siwasaidii tena.

Nikayabwaga magogo yao chini kwa nguvu za mikono yangu kisha nikakabeba katoto kangu nikawa nakabembeleza kisha Nikaondoka na ghafla nikashtuka usingizini saa kumi na moja kasoro asubuhi.

Ila niliposhtuka mkono wangu wa kulia ulikuwa unatetemeka halafu umechoka kuliko wa kushoto.

Nimetafakari sana nikakosa tafsiri ya ndoto hiyo, bila Shaka nitapatiwa ufafanuzi hapa, Asanteni na karibuni sana.
 
Unapokuwa na uwezo mzuri na ukawapenda watu si lazima wakupende nawe usiwalazimishe fanya wema nenda zako umeeleewa linganisha maneno haya na maisha yako kwenye na kwenye ndoto hiyo amen
 
Sio ndoto zote zinatoka kwa Mungu zingine zinatoka kwa shetani. Kwa nguvu ipi ulikua unaamuru hayo yote yatendeke? Na hiyo haikua ndoto ilikua real thus y ukaamka ukakuta mkono unauma. Ngoja waje wajuao ndoto
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom