mapara manne
Member
- Dec 27, 2016
- 10
- 9
Ni mda sasa umepita takribani miaka kama 7 tangu nianze kuiota ndoto hii.Usiku wa manane kabisa kuna ndoto huwa inanisumbuwa mara kwa mara.Ndoto yenyewe iko hivi huwa najikuta natembea peke yangu njiani na kuna sehemu nafika nakuta kuna njia mbili moja hinaenda kushoto nyingine kulia na mara nyingi sehemu nayoenda huwa siijui kwa hiyo hapo hunilazimu kuchagua njia mara nyingi katika kuchagua hujikuta nimechagua inayoenda mkono wa kulia na hapo natembea kama nusu saa nakutana na kijiji ambacho sikijui na kina nyumba za mabati tupu yaani kama unavyoona mabatini mwanza na mara nyingi nikishafika hapo nikaanza kuona zile nyumba na nashituka kutoka usingizini na huwa naonekana kama mtu mwenye mawazo mengi nikitafakari kile nilichokuwa nakiona mwenye ufahamu wa ndoto anifafanunulie maana ni miaka 7 imetimia tangu nianze kuiota