Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Waziri Kivuli wa Ofisi ya Waziri Mkuu- Bunge, Sera, Vijana, Kazi na Ajira kupitia ACT Wazalendo, Ndolezi Petro, ameitaka Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) kuhakikisha kuwa ugawaji wa majimbo unazingatia vigezo vya kisheria badala ya kuongozwa na maslahi ya kisiasa.
Akitoa kauli yake kwa umma siku ya Jumatatu Machi 17, 2025, amesema kuwa ugawaji wa majimbo katika Tanzania Bara haujazingatia uwiano wa uwakilishi kwa wananchi, huku maeneo yenye idadi kubwa ya watu na jiografia kubwa yakipewa majimbo machache, na maeneo yenye idadi ndogo ya watu yakitengewa majimbo mengi zaidi.
Akitolea mfano, amesema Mkoa wa Kigoma wenye wakazi 2,470,967 na ukubwa wa kilomita za mraba 45,066 una majimbo 8 pekee, wakati Mkoa wa Mtwara wenye wakazi 1,634,947 na ukubwa wa kilomita za mraba 16,710 una majimbo 10.
"Wilaya ya Uvinza pekee ina kilomita za mraba 28,901, lakini ina jimbo moja, huku Wilaya ya Masasi mkoani Mtwara yenye wakazi wachache zaidi ikiwa na majimbo matatu," amesema, akisisitiza kuwa kuna haja ya kugawa Jimbo la Kigoma Kusini na Jimbo la Kasulu Vijijini ili kuongeza uwiano wa uwakilishi.
Ndolezi pia ametolea mfano wa Jimbo la Pangani mkoani Tanga lenye wakazi 75,645 ambalo linapata mwakilishi mmoja bungeni, huku Kata ya Murungu katika Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma ikiwa na wakazi 84,449 lakini inawakilishwa tu na diwani. "Hali hii inaonesha kuwa hakuna usawa katika mgawanyo wa majimbo," amesema.
Aidha, ametaja mikoa mingine yenye mgawanyo usio wa haki, akieleza kuwa Jimbo la Madaba mkoani Ruvuma lenye wakazi 65,215 lina mwakilishi bungeni sawa na Jimbo la Bariadi lenye wakazi 644,312, na Jimbo la Lindi Mjini lenye wakazi 95,098 lina mwakilishi mmoja sawa na Jimbo la Dodoma Mjini lenye wakazi 765,179.
Kutokana na hali hii, Ndolezi amesisitiza kuwa ni muhimu kwa INEC kurekebisha mgawanyo wa majimbo ili kuhakikisha haki na uwakilishi wenye usawa kwa wananchi wote. Ametoa wito kwa tume hiyo kutumia takwimu sahihi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) ili kuhakikisha kuwa ugawaji wa majimbo unazingatia idadi ya watu, jiografia na mahitaji ya maendeleo.